Yaliyoandikwa hapa ndio yanayotakiwa kufuatwa au kuzingatiwa wakati wa kushiriki chochote katika tovuti yetu. Ni vyema kila mtumiaji akasoma ukurasa huu kabla ya kushiriki au kujiunga katika mtandao wetu.
Mtu yoyote anaweza kushiriki kwa kuchapisha andiko lolote ikiwemo kuuliza swali, kujibu swali, kuandika makala au ku comment katika makala(posts) mbalimbali. MojaSky haihusiki na yale yanayoandikwa katika tovuti hii, japo machapisho yote yatapitiwa kuhakikisha kama yanafuata sheria.
Mambo yasiyoruhusiwa
1.Upotoshaji.
Mchango wowote wenye lengo la kufikisha ujumbe wenye kupotosha unapaswa kuepukwa.
2.Chapisho lisilo na maana
Kuweka chapisho lisilokua na maana kwa makusudi ni kosa. Hii inajumuisha kuweka chapisho ili kupata clicks au kuwasumbua wengine au kujifurahisha tu.
3. Hakimiliki
Kuwa makini unapoweka kitu chochote kinacholindwa na hakimiliki hasa kama sio wewe unaemiliki. Kuelezea kitu unaweza tumia maneno kadhaa bila kusahau kumtambua/kumtaja mmiliki halali.
4. Utawajibika kwa kile unachochapisha. MojaSky haitahusika na kile ulicho post.
Ukurasa huu utafanyiwa marekebisho mara kwa mara.