Whatsapp inapataje faida?
Jiunge MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Login MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Umesahau password yako?. Andika email yako hapo chini alafu bonyeza 'Reset'. Utapokea link katika email yako kwa ajili ya kutengeneza password mpya.
Tafadhali elezea kwa nini unahisi chapisho hili linapaswa kuripotiwa
Salim Jumbe
WhatsApp iligunduliwa mwaka 2009 na Brian Acton na Jan Koum na baadae kuamua kuiuza kwa Facebook, hivyo inamilikiwa na facebook ambayo pia inamiliki mesenger na instagram. Baadhi ya watu wanasema kuwa lengo kubwa zaidi la kuinunua whatsapp halikuwa kupata faida bali ni kuondoa kwanza ushindani kati yake na facebook messenger.
Kipindi cha nyuma whatsapp ilianza kuchaji kiasi cha 1$(kama 2300 za Tanzania) kwa kila mwaka baada ya mwaka mmoja wa bure, baada ya muda fulani waliamua kuachana na ilo.
Msemo fulani(sijui aliyesema) uliwahi kusema “kama haulipii huduma wewe sio mteja, wewe ni bidhaa inayouzwa” kwa kuangalia msemo huu inamaanisha nini? kuna uwezekano mkubwa whatsapp inatengeneza faida kwa kutumia data zinazotokana na chat za watu kwenye mtandao wao na baadaye kuzitumia kwenye mtandao wao wa facebook kuonesha matangazo.
Umewahi kujiuliza kwa nini ukiingia facebook unaona matangazo kutokana na vitu unavyovipenda? ilo linaweza kuwa jibu.