Wanaume wanahitaji nini katika mahusiano?
Jiunge MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Login MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Umesahau password yako?. Andika email yako hapo chini alafu bonyeza 'Reset'. Utapokea link katika email yako kwa ajili ya kutengeneza password mpya.
Tafadhali elezea kwa nini unahisi chapisho hili linapaswa kuripotiwa
Jose Mandingo
Mwanaume anahitaji mambo haya kutoka kwa mwanamke
Kutambuliwa uwezo wake
Kama unatamani mwanaume umpendaye aanze (aendelee) kuvutiwa na wewe, chukua hatua ya kubaini vitu vya pekee alivyonavyo na onesha kwa dhati kuwa unavitambua. Kwa kawaida kila mwanaume anayo maeneo yake anayoyaweza vizuri kuliko wengine.
Anahitaji kuheshimiwa
Kwa mwanaume hitaji la kuheshimiwa ni kubwa zaidi. Tunapozungumzia heshima kwa mwanaume, katika mazingira yetu, tunamaanisha hali ya kutamani kujiona yu na hadhi ya juu, yu na mamlaka zaidi pengine kuliko mwanamke. Kinyume chake ni kudharauliwa, kuwekwa katika mazingira ya kujiona hana hadhi, hana mamlaka, asiye na kauli wala uwezo kufanya lolote bila mwongozo wa mwanamke.
Anatamani kusikilizwa, sio kukosolewa
Wanaume wengi hawapendi kukosolewa hata kama hawasemi. Unapomkosoa mwanaume unamfanya apoteze hali ya kujiamini na hivyo hujisikia kama mtu anayeongozwa. Si wanaume wengi hufurahia kuongozwa. Kinyume na kumkosoa, ifanye sauti yake isikike.
Anahitaji uhuru, faragha
Uhuru na faragha kwa hakika ni kinyume kabisa na kile ambacho wanawake wanakihitaji kama tutakavyoona mbeleni. Lakini kwa mwanaume, ukweli ni kuwa anahitaji kujiona ni mtu mwenye uhuru wa kufanya mambo anayoyafurahia bila kuambiwa kingine cha tofauti anapaswa kukifanya.
Mbinafsi anayevutiwa na mwili
Ikiwa unataka kumwutia mwanaume, hakikisha unaendelea kumvutia kimwili. Fahamu kinachomvutia na jitahidi kujiweka katika namna anayoitarajia. Kosa kubwa wanalolifanya wanawake wengi ni kujisahau mara wanapoolewa. Unaposahau kuendelea kuwa vile ulivyokuwa kabla ya ndoa, unachochea ubinafsi wa mwanaume.
Mfanye ajione anahitajika
Jaribio lolote la kumwonesha mwanaume kuwa hata asipokuwepo, hata asipofanya chochote, hata asipotoa wazo lolote, hakuna kitakachoharibika linaweza kumfanya ‘akahujumu’ mahusiano. Kumfanya ajione hahitajiki, kunaathiri kiburi chake cha uanaume (ego) na inaweza kuwa mwanzo wa matatizo.
Hapendi kubadilishwa
Ukitaka mwanaume afuate yale unayotaka ayafanye, mkubali vile alivyo na ajue umempokea bila masharti. Kukubaliwa ni motisha ya kubadilika. Hiyo ndio kanuni. Mume wako anapojua pamoja na mapungufu yake bado umemkubali alivyo, kubadilika ni suala la muda.
Kama utapenda kusoma kwa urefu zaidi INGIA HAPA