Jiunge

Jiunge MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection

Unayo account ? Log In


Unayo account ? Log in

Log In

Login MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection

Jiunge Hapa


Umesahau Password?

Hauna Account, Jiunge Hapa

Umesahau Password

Umesahau password yako?. Andika email yako hapo chini alafu bonyeza 'Reset'. Utapokea link katika email yako kwa ajili ya kutengeneza password mpya.

Unayo account ? Log in

Tafadhali andika jina lako kamili.

Tafadhali andika E-Mail yako.

Please choose an appropriate title for the question so it can be answered easily.


Tafadhali elezea kwa nini unahisi chapisho hili linapaswa kuripotiwa

Sign InSign Up

1Sky

1Sky

1Sky Navigation

  • Blog
  • Wasiliana Nasi
  • Advanced Search
  • App

Mobile menu

Close
Uliza Swali
  • Home
  • Maswali
  • Points
  • Miongozo
  • Wasiliana Nasi
  • Advanced Search
  • App
Home» Maswali»Q 34789
In Process
Anonymous
Asked: January 25, 20202020-01-25T07:38:31+03:00 2020-01-25T07:38:31+03:00LAPF

Utaratibu wa kuwa mwanachama wa LAPF ukoje?

Utaratibu wa kuwa mwanachama wa LAPF ukoje?
  • 1
  • 250
  • 0
  • Share
    • Share on WhatsApp
    • Share on Facebook
    • Share on Twitter
Jibu
  • Report

Jibu 1

  • Kura
  • Zamani
  • Mpya
  1. Salim Jumbe

    Salim Jumbe

    • Dar es Salaam, Tanzania
    • 0 Questions
    • 132 Answers
    • 0 Best Answers
    • 474 Points
    View Profile
    Salim Jumbe Proffesional
    2020-01-25T07:45:29+03:00Jibu - January 25, 2020 saa 7:45 am

    Uandikishaji wa waajiri na wanachama ni jambo muhimu sana kwani linasaidia LAPF kuwa na takwimu na kumbukumbu sahihi za wanachama ikiwa ni pamoja na umri, jinsia, tarehe ya kustaafu, kiwango cha michango, wategemezi n.k. Katika mfumo wa pensheni ni muhimu sana kuwa na taarifa sahihi kwani zinasaidia katika kufanya tathmini ya Mfuko na kujua uwezo wake katika kutoa au kuboresha mafao.

    Uandikishaji wa Waajiri

    LAPF huwaandikisha Waajiri kwa kuwasajili kupitia fomu Na. LAPF/REG.l. Baada ya kujiandikisha mwajiri hupatiwa hati ya usajili ijulikanayo kama LAPF/REG.2 ambayo huwajibika kuiweka mahali panapoonekana katika ofisi yake. Baada ya usajili, mwajiri mchangiaji anawajibika kufanya mambo yafuatayo:

    • Kutoa kumbukumbu sahihi za watumishi ambazo zitatumika katika uandikishaji na ulipaji wa mafao;
    • Kuhakikisha kwamba watumishi wote walioandikishwa na LAPF wanachangia na michango yao inawasilishwa kila mwezi pamoja na       vielelezo vya michango hiyo (Deduction details);
    • Kuhakikisha watumishi wote waliojiandikisha na LAPF wanajaziwa data-sheet na kuwekewa deduction code No. 639 kwenye mfumo wa kompyuta wa LAWSON (kwa watumishi wa umma wanaolipwa mishahara kupitia Hazina);
    • Kupitia mara kwa mara payroll kwa lengo la kuhakikisha kuwa wanachama wote wa LAPF wanachangia;
    •  Kuiarifu LAPF juu ya mabadiliko yeyote yanayomhusu mtumishi kwa mfano kubadilika kwa majina na taarifa nyingine muhimu za mtumishi;
    • Kuwasilisha orodha ya wanachama wanaolipwa mishahara kutoka vyanzo vya ndani vya Mwajiri iIi kuweza kutambuliwa na LAPF.

    Uandikishaji wa Wanachama
    Jukumu la kuwaandikisha wanachama kwenye Mfuko linaihusu LAPF, mwajiri pamoja na wanachama wenyewe. Kwa mujibu wa Sheria ya LAPF, kifungu Na. 16 na 17 majukumu ya kila mmoja yameelezwa wazi. Aidha, Sheria Na.8 ya mwaka 2008 ya Udhibiti na Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii, kifungu cha 30 imetamka kuwa “Mfanyakazi ambaye hajawahi kujiunga na Mfuko wowote wa pensheni au anayeajiriwa kwa mara ya kwanza anao uhuru wa kuchagua na kujiunga na Mfuko wowote wa Hifadhi ya Jamii aupendao”. Kwa msingi huo LAPF kama ilivyo mifuko mingine ina jukumu la kuwaelimisha watumishi wapya iIi waweze kuamua mfuko wa kujiunga baada ya kuelewa huduma na mafao yanayotolewa. Wanachama wa LAPF wako katika makundi mawili ambayo ni wanachama wa lazima na wanachama wa hiari.
     

    Wanachama wa Lazima

    Mwanachama wa lazima ni yule ambaye yuko katika ajira ya kudumu au ya mkataba akipokea mshahara kila mwezi. Mwanachama katika kundi hili anawajibika kuchangia katika mfumo wa lazima hivyo atajaza fomu ya uandikishwaji wa LAPF ijulikanayo kama LAPFIREG.3A na kupatiwa nambari ya uanachama na kitambulisho (LAPFIREG.4) ambacho kitatumika kujitambulisha wakati wa mawasiliano na LAPF na baadae katika ulipaji wa mafao.

    Wanachama wa Hiari

    LAPF inao pia mpango wa akiba wa hiari ambao mwanachama wake ni mtu yeyote aliyeamua kujiwekea akiba. Kundi linalohusika katika mpango huu ni wale ambao wamejiajiri wenyewe (wakulima, wavuvi, waendesha pikipiki, wasanii, wafanya biashara ndogondogo n.k.) Watumishi wanaochangia katika mfumo wa lazima wanaweza pia kuchangia kwa ziada katika mpango huu. Chini ya mpango huu uanachama utakamilika baada ya mwanachama kujaza fomu ya LAPF (LAPF/REG.3B) na kupatiwa nambari ya uanachama na kitambulisho (LAPF/REG.4). Mwanachama ataelekeza kiasi ambacho yuko tayari kuchangia kwa mwezi, kwa wiki na hata kwa siku, iIi mradi jumla yake isiwe chini ya shilingi 20,000/= kwa mwezi

     

    Fomu za Kujiunga:

    Bofy hapa kupata fomu za kujiuunga.

    • 0
    • Reply
    • Share
      Share
      • Share on WhatsApp
      • Share on Facebook
      • Share on Twitter
      • Report
Jibu swali hili

Jibu swali hili
Cancel reply

Chagua

Sidebar

Promo

  • Smartphone mpya ya Samsung kwa Tsh 220,000 Tu

  • Nafasi zote mpya za kazi zipo hapa

  • Tafuta vitu mtandaoni kwa lugha ya Kiswahili

  • Tafuta Ajira kiurahisi. Jaribu Sasa

  • Explore

    • Home
    • Maswali
    • Polls
    • Points
    • Watumiaji
    • Miongozo
    • App

    MojaSky

    Insert/edit link

    Enter the destination URL

    Or link to existing content

      No search term specified. Showing recent items. Search or use up and down arrow keys to select an item.