Utaratibu wa kupata cheti cha kuzaliwa kwa watoto uko vipi?
Jiunge MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Login MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Umesahau password yako?. Andika email yako hapo chini alafu bonyeza 'Reset'. Utapokea link katika email yako kwa ajili ya kutengeneza password mpya.
Tafadhali elezea kwa nini unahisi chapisho hili linapaswa kuripotiwa
Salim Jumbe
Kwa mujibu wa sheria, vizazi ni lazima viandikishwe ndani ya siku 90 za kutokea kwake. Hata hivyo sheria inaruhusu usajili wa baadaye.
Muhimu:
Iwapo mtoto amezaliwa hospitali, vituo vya afya na zahanati, hakikisha kuwa unapata tangazo la kizazi.
Iwapo mtoto amezaliwa nyumbani, toa taarifa kwa ofisa mtendaji wa kijiji au msajili wa wilaya wa vizazi na vifo ili upate tangazo la kizazi. Hii ni lazima ifanyike ndani ya siku 90.
Taratibu za kufuata kupata cheti:
Wasilisha tangazo la kizazi kwa msajili wa vizazi na vifo wa wilaya ambako kizazi kimetokea.
Lipa ada inayotakiwa kwa ajili ya cheti (kwa sasa ada ni Tsh. 3500/=).