Utaratibu wa kuomba mafao NSSF uko vipi?
Jiunge MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Login MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Umesahau password yako?. Andika email yako hapo chini alafu bonyeza 'Reset'. Utapokea link katika email yako kwa ajili ya kutengeneza password mpya.
Tafadhali elezea kwa nini unahisi chapisho hili linapaswa kuripotiwa
Salim Jumbe
Utaratibu wa kuomba mafao ya NSSF ni kama ufuatavyo;
Mafao ya Uzee
Fika ofisi ya NSSF ukiwa na Barua ya kustaafu kutoka kwa mwajiri, kadi yako ya uanachama ya NSSF na kopi yake, picha tatu za paspot saiz na kopi ya kadi ya benki.
Utapatiwa fomu NSSF/R.6 NA NSSF/B.1 ujaze kisha utafunguliwa madai
Mafao ya Ulemavu
Fika ofisi ya NSSF ukiwa na ripoti kuhusu ulemavu kutoka kwa jopo la madaktari,kadi ya uanachama ya NSSF na kopi yake pamoja na picha tatu za paspot saiz.
Utapatiwa fomu NSSF/B.1 ujaze kisha utafunguliwa madai
Mafao ya Urithi
Fika ofisi ya NSSF ukiwa na viambatanisho vifuatavyo;
.Cheti cha kifo, kopi yake iwe imethibitishwa na mahakama
.Muhtasari wa kikao cha wanandugu, kopi yake iwe imethibitishwa na mahakama
.Cheti cha ndoa ikiwa mafao yatafunguliwa na mwenza wa marehemu, kopi yake iwe imethibitishwa na mahakama
.Cheti cha kuzaliwa ikiwa madai yatafunguliwa na mtoto wa marehemu, kopi yake iwe imethibitishwa na mahakama
.Fomu namba 4 ya usimamizi wa mirathi ambayo hutolewa na mahakama
.Kadi ya uanachama ya NSSF kama ipo na kopi yake
Utapatiwa fomu NSSF/B.2 na NSSF/ B.18 ujaze kisha utafunguliwa madai
Mafao ya Uzazi
Mwanachama anatakiwa kufungua madai akiwa wiki ya 24 ya ujauzito au ndani ya siku 90 baada ya kujifungua
Fika ofisi ya NSSF ukiwa na picha tatu za paspot saiz, kadi ya uanachama ya NSSF na kopi yake pamoja na kopi ya kadi ya benki.
Utapatiwa fomu MB1,MB2 na MB3 kisha kufunguliwa madai
Msaada wa mazishi
Fika ofisi ya NSSF ukiwa na Kibali cha mazishi/cheti cha kiufo,risiti halisi ya gharama za mazishi zinazomuhusu marehemu moja kwa moja, muhtasari wa kikao cha wanandugu kumteua anayekuja kufungua madai haya pamoja na kadi ya marehemu ya uanachama wa NSSF kama ipo.
Utapatiwa fomu NSSF/B.3 ujaze kisha utafunguliwa madai.
Mafao ya Matibabu (SHIB)
Fika ofisi ya NSSF ukiwa na vyeti vya kuzaliwa vya watoto (nakala halisi na kopi mbili kwa kila cheti) kwa mwanachama mwenye mtoto, Cheti cha ndoa kwa mwanachama mwenye mwenza (nakala halisi na kopi mbili), picha tatu za paspot saiz kwa mwanachama na tatu kwa kila mtegemezi.
Utapatiwa fomu SHIB 3A ujaze na Kuandikishwa kwaajili ya mafao ya matibabu.
Kurudishiwa michango ya Uanachama/Kujitoa
Fika ofisi ya NSSF ukiwa na nakala halisi na kopi ya barua ya kuacha kazi kutoka kwa mwajiri, Kadi ya uanachama ya NSSF na kopi yake, picha tatu paspoy saix na kopi ya kadi ya benki.
Utapatiwa fomu NSSF B.17 ujaze na NSSF/R.6 upeleke kwa mwajiri kisha utafunguliwa madai
chanzo ; Tovuti ya serikali