Unajua jinsi ya kupiga window PC?
Jiunge MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Login MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Umesahau password yako?. Andika email yako hapo chini alafu bonyeza 'Reset'. Utapokea link katika email yako kwa ajili ya kutengeneza password mpya.
Tafadhali elezea kwa nini unahisi chapisho hili linapaswa kuripotiwa
Hapana sijui, ila labda hii inaweza kukusaidia
MAMBO YA MUHIMU YA KUZINGATIA
Kabla ya kuinstall Windows 10 kwenye kompyuta yako yapo baadhi ya mambo ya kuzingatia, mambo haya yanatofautina kulingana na hali ya kompyuta yako hivyo ni vyema kama ukisoma mambo yote yaliyipo kwenye sehemu hii.
Jambo la kwanza, unatakiwa kuhakikisha unakuwa na programu ya Windows 10 kwaajili ya kuinstall kwenye kompyuta yako. Hapa ningependa kukushauri kuwa na Flash yenye programu hiyo kuliko kuwa na CD, kwani mara nyingi CD zinakuwa ni rahisi kupata michubuko na hivyo unaweza kukwama unapokuwa una install Windows kwenye kompyuta yako.
Jambo la pili, unatakiwa kujua kama kompyuta yako inayo Windows au Haina, hili ni muhimu kwani kuna watu unakuta tayari kompyuta zao zinayo programu ya Windows hivyo wanataka kuweka toleo jipya la Windows au kufuta lile la zamani na kuweka toleo jipya, kama unataka kufuta toleo la zamani ni vyema kufanya hivyo wakati una install windows kwani hii itakuwa ni rahisi zaidi.
Jambo la tatu, hakikisha kama unatumia laptop basi laptop yako ina chaji kwa kiwango fulani pia kama ni muhimu jaribu kuhakikisha laptop hiyo imechomekwa kwenye chaji. Kama unatumia desktop hakikisha unakuwa na uhakika kuhusu tatizo la umeme kwani kuna wakati kukitokea tatizo la umeme basi unaweza kuharibu hatua nzima na kujikuta una anza upya.
JINSI YA KUNSTALL WINDOWS
Kama tayari unavyo vitu vyote sasa twende hatua kwa hatua tukajifunze jinsi ya kunstall Windows kwenye kompyuta yako.
Chomeka USB au CD iliyokuwa na Windows hakikisha kompyuta yako imezimwa (kama unatumia CD weka kwanza CD kisha zima kompyuta yako au Restart), baada ya kuchomeka washa kompyuta yako kisha bofya kitufe chenye kusema boot on chagua CD kama unatumia CD na chagua USB kama unatumia USB.
Baada ya kompyuta kuwaka utaona Screen ya Blue ikitaka uchague lugha ambayo ungependelea kutumia, Chagua English kisha endelea kwenye hatua inayofuata.
Baada ya hapo utaona kitufe cha Install bofya hapo kuendendelea.
Baada ya hapo unachotakiwa kufanya ni kuweka KEY za programu ya Windows ambayo unataka kuweka kwenye kompyuta yako, kumbuka KEY hizi ni kama leseni hivyo ni muhimu kuwa nazo kabla ya kuamua kuanza process nzima.
Baada ya kuweka KEY na kubofya NEXT sasa ni wakati wa kukubali vigezo na masharti bofya ACCEPT iliyopo chini upande wa kulia.
Hatua inayofuata ni muhimu sana kwani hapa ndipo pale ambapo unaweza kuchagua kati ya kuweka Windows upya kwenye kompyuta yako au kupandisha toleo jipya la Windows. Kama unataka kuweka toleo jipya basi itakubidi kuchagua CUSTOM : na kama unataka tu kuweka toleo jipya basi chagua sehemu ya UPGRADE :
Unapo chagua sehemu ya CUSTOM utapelekwa kwenye ukurasa mpya ambapo unatakiwa ku-format partition unayotaka kuweka Windows, Chagua partition kisha bofya Format iliyopo chini.
Baada ya hapo utapelewa sasa kwenye ukurasa wa kuinstall Windows na utaona Windows imeanza kuinstall, Subiri kwa muda kisha endelea kwenye hatua zinazofuata.
Baada ya kukamilika utatakiwa kuseti kompyuta yako, bofya kitufe cha USE EXPERSS SETTINGS kuseti kompyuta yako kwa haraka.
Hadi hapo utakuwa umemaliza kuinstall Windows 10 kwenye kompyuta yako, Kama una swali au kuna mahali umekwama usiache kuuliza hapo chini.
Kujifunza kwa kina zaidi(Kuna picha zinazoelekeza vema zaidi)