Umewahi kufanya kitu gani cha ajabu?
Jiunge MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Login MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Umesahau password yako?. Andika email yako hapo chini alafu bonyeza 'Reset'. Utapokea link katika email yako kwa ajili ya kutengeneza password mpya.
Tafadhali elezea kwa nini unahisi chapisho hili linapaswa kuripotiwa
Faustine John
mimi ndio nilikuwa refa wa ngumi,yaani muda wa kutoka shule wanafunzi wenzangu walikuwa wanakuja kuniuliza kama kuna pambano.Yaani walikuwa wakitibuana tu,wanakuja kwangu kutoa taarifa nami nawaingiza kwenye ratiba.Wakati mwingine nilikuwa naratibu mapambano mpaka matatu kwa siku.Sheria ilikuwa ukitoka damu basi pambano limeisha na wewe uliyetoka damu ndio umeshapigwa.Kimbembe ni siku siri ilipovuja kwa walimu baada ya mtoto mmoja kula kichapo mpaka jino likatoka na mzazi akaja kesho yake shule.Yaani nilipomuona tu kijana yuko na mzazi wake wanaenda ofisi ya mwalimu mkuu,nilikula kona na sikutokea shule wiki nzima.Nilikua nikitoka nyumbani naaga naenda shule kumbe naishi porini.Bahati mbaya kuna siku dogo mmoja aliniona nimebana miembeni,daaah akaenda kumtonya ticha.Asikuambie mtu,darasa zima lilitumwa kunikamata,kuna watu wana mbio sio mchezo.Nilichezea fimbo sana siku hiyo na ndio nikastaafu rasmi urefa na kuratibu ndondi.
nimeikopi tu mahali nimecheka sana