Uhai ulianzia wapi?
Jiunge MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Login MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Umesahau password yako?. Andika email yako hapo chini alafu bonyeza 'Reset'. Utapokea link katika email yako kwa ajili ya kutengeneza password mpya.
Tafadhali elezea kwa nini unahisi chapisho hili linapaswa kuripotiwa
Emmanuel Magessa
Wanasayansi wengi wanaoamini mageuzi watakuambia kwamba uhai ulianza mabilioni ya miaka iliyopita kwenye ukingo wa kidimbwi cha kale kilichojaa maji wakati wa kupwa au katika sehemu za chini ya bahari. Wao huhisi kwamba katika maeneo yasiyojulikana kama hayo, kemikali zilijikusanya na kuwa vitu vinavyofanana na mapovu,vikafanyiza molekuli tata, na kuanza kujigawanya-gawanya. Wanaamini kwamba uhai wote duniani ulijitokeza wenyewe tu kutokana na chembe “sahili,” moja au zaidi.
Wanasayansi wengine wanaoheshimika ambao pia wanaunga mkono mageuzi hawakubaliani na wazo hilo. Wanakisia kwamba chembe za kwanza au angalau sehemu zake kuu zilikuja duniani kutoka anga la nje.
Licha ya jitihada zao nyingi, wanasayansi hawajaweza kuthibitisha kwamba uhai unaweza kutokea ghafla kutokana na molekuli zinazodhaniwa zilitokeza uhai. Katika mwaka wa 2008, Alexandre Meinesz, Profesa wa Biolijia, alizungumzia utata huo. Alisema kwamba kwa zaidi ya miaka 50 iliyopita, “hakuna uthibitisho wowote uliopatikana kupitia majaribio yaliyofanywa unaounga mkono nadharia ya kwamba uhai ulitokea ghafla Duniani kutokana na molekuli fulani, wala hakuna maendeleo ya kisayansi yanayoweza kuthibitisha hilo.”
Siku zote uhai hutokana na uhai ambao tayari upo. Watafiti wamegundua kwamba ili chembe iendelee kuwa hai, angalau aina tatu tofauti za molekuli tata lazima zifanye kazi pamoja – DNA au deoksiribonyuklia asidi, RNA( ribonucleic acid), na protini. Leo, ni wanasayansi wachache wanaoweza kudai kwamba chembe kamili iliyo hai iliyojitokeza yenyewe kutokana na mchanganyiko wa kemikali zisizo hai.
Wanasayansi wengi huhisi kwamba huenda uhai ulijitokeza wenyewe kwa sababu ya jaribio fulani lililofanywa kwa mara ya kwanza mwaka 1953. Mwaka huo Stanley L. Miller aliweza kutengeneza asidi – amino, kemikali za msingi zinazofanyiza protini,kwa kupitisha nguvu za umeme ndani ya mchanganyiko wa gesi zilizodhaniwa kuwa zingewakilisha anga la Dunia. Toka wakati huo, asidi – amino zimepatikana pia katika vimondo. Ugunduzi huu haumaanishi kwamba kemikali za msingi za uhai zinaweza kujitokeza zenyewe.
Robert Shapiro, aliyekuwa profesa wa kemia katika Chuo Kikuu cha New York, anasema, “ Baadhi ya waandishi wameamini kwamba kemikali za msingi za uhai zinaweza kutengenezwa kwa urahisi kwa kutumia majaribio kama yale ya Miller na kwamba zinapatikana katika vimondo. Hata hivyo sivyo ilivyo.” * 1
Fikiria molekuli ya RNA. Imefanyizwa na molekuli ndogo zinazoitwa nukliotidi. Nukliotidi ni aina tofauti ya molekuli na ni tata zaidi kidogo kuliko asidi – amino. Shapiro anasema kwamba “ hakuna nukliotidi za aina yoyote zinazoripotiwa kuwa zilitokana na majaribio yanayohusu umeme wala katika uchunguzi wa vimondo. Pia anasema kwamba uwezekano wa molekuli kujifanyiza bila mpangilio maalum na kujikusanya toka kemikali nyingi za msingi “ ni mdogo sana hivi kwamba hata kama ungetokea mahali popote katika ulimwengu unaonekana ungeonwa bahati.
Mtafiti Hubert P. Yockey, anayeunga mkono fundisho la mageuzi ana maelezo zaidi. Anasema: “Haiwezekani kwamba chanzo cha uhai ni ‘protini tu.’”* 2 RNA inahitajika kutengeneza protini, hata hivyo, protini zinahusika katika utengenezaji wa RNA.
Je, kuna uwezekano wowote kwamba protini na molekuli ya RNA kutokea mahali pamoja kwa wakati uleule na kufanyiza uhai unaoweza kutokeza chembe ambazo zinaweza kuzaa na kuendeleza uhai?
Yaelekea uwezekano wa jambo hilo kujitokeza lenyewe, kukiwa na mchanganyiko usio na mpangilio maalumu wa protini na RNA, ni mdogo sana, anasema Dkt. Carol Creland ; mshiriki wa NASA ( National Aeronautics and Space Administration’s Astrobilogy Institute).
1* Profesa Shapiro haamini kwamba uhai ulitokana na Muumba. Anaamini kuwa uhai ulijitokeza wenyewe kwa njia fulani ambayo bado haijaeleweka. Mwaka wa 2009 wanasayansi katika Chuo Kikuu cha Manchester, Uingereza,waliripoti kwamba wametengeneza nukliotidi katika maabara yao. Hata hivyo, Shapiro anasema kwamba viambatano vyao “bila shaka havifikii viwango vyangu vinavyokubalika vya kutengeneza RNA.”
2* Dkt. Cleland haamini masimulizi kuhusu uumbaji wa Mungu . Anaamini kwamba uhai ulijitokeza wenyewe katika njia fulani ambayo bado haijaeleweka vizuri.
UKWELI KUHUSU UCHUNGUZI WA KISAYANSI NA UHAI (UUMBAJI)
Ukweli wa mambo: Utafiti wote wa kisayansi umeonyesha kwamba uhai hauwezi kujitokeza wenyewe kutokana na kitu kisicho hai.
Swali : Kuna msingi gani wa kisayansi unaowafanya watu waseme kwamba chembe ya kwanza ilitokana na kemikali zisizo hai?
Ukweli wa mambo: Wanasayansi wamebuni katika maabara, hali za kimazingira ambazo wanaamini zilikuwako mapema katika historia ya dunia.Katika majaribio hayo, wanasayansi fulani wametengeneza baadhi ya molekuli zinazopatikana katika viumbe hai.
Swali: Ikiwa kemikali katika jaribio hilo zinawakilisha mazingira ya awali ya dunia na molekuli inayotokezwa inawakilisha chembe za msingi za uhai, mwanasayansi aliyefanya jaribio hilo anawakilisha nani au nini? Je, anawakilisha matukio yaliyojitokeza kiholela au mtu fulani mwenye akili?
Ukweli wa mambo: Ili chembe iendelee kuwa hai, lazima protini na molekuli ya RNA zishirikiane.Wanasayansi wamekiri kwamba haiwezekani kuwa molekuli ya RNA ilijitokeza yenyewe. Uwezekano
wa hata protini moja kujitokeza yenyewe ni mdogo sana. Haiwezekani kamwe kwamba molekuli ya RNA na protini zingeweza kujitokeza zenyewe mahali palepale, wakati uleule na ziweze kushirikiana.
Swali: Ni nini kinachohitaji imani zaidi—kuamini kwamba chembe pamoja na mamilioni ya sehemu zake zinazoshirikiana kwa ustadi wa hali ya juu zilijitokeza zenyewe au kwamba chembe zilibuniwa
na Muumba mwenye akili?
chanzo: Jamiiforums