Jiunge MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Login MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Umesahau password yako?. Andika email yako hapo chini alafu bonyeza 'Reset'. Utapokea link katika email yako kwa ajili ya kutengeneza password mpya.
Tafadhali elezea kwa nini unahisi chapisho hili linapaswa kuripotiwa
Nawezaje kuwasiliana na TRA?
Salim Jumbe
Wasiliana na TRA kwa njia hizi Msimbo wa Posta : 28 Edward Sokoine Drive, 11105 Mchafukoge, Ilala CBD, S.L.P 11491, Dar es salaam, Tanzania Simu:+255 22 2119591-4 Kituo cha huduma kwa Wateja Tafadhali piga simu kwa maswali, malalamiko na maoni. Wateja wote wa TRA wanahamasishwa kutumia huduma hiziSoma Zaidi
Wasiliana na TRA kwa njia hizi
Msimbo wa Posta : 28 Edward Sokoine Drive, 11105 Mchafukoge, Ilala CBD, S.L.P 11491, Dar es salaam, Tanzania
Simu:+255 22 2119591-4
Kituo cha huduma kwa Wateja
Tafadhali piga simu kwa maswali, malalamiko na maoni. Wateja wote wa TRA wanahamasishwa kutumia huduma hizi popote pale walipo.
Simu za Tanzania zitakuwa bure:
0800 750 075
0800 780 078
Muda wa kazi Kituoni utakuwa kuanzia Saa 02:00 Asubuhi mpaka 01:00 Usiku kwa saa za Afrika Mashariki Jumatatu hadi Ijumaa isipokuwa siku za sikukuu.
Ofisi za TRA za Mkoa
Tafuta taarifa zote za mawasiliano kwa ofisi za mikoani hapa.
Dar es salaam, Tanzania
Phone: 0800 750075 (Vodacom )
Arusha, Tanzania
Phone: +255 27 2502946
Kibaha
Phone: +255 23 240 2905
Dar es salaam
Phone: +255 22 2771846
Dar es salaam
Phone: +255 22 2185545
Dar es salaam
Phone: +255 22 2861122
Mwanza
Phone: +255 28 2500906
Phone: +255 27 2642200
Moshi
Phone: +255 27 2753268
Tabora
Phone: +255 26 2604609
Sumbawanga
Phone: +255 25 2801089
Songea
Phone: +255 25 2602140
Shinyanga
Phone: +255 28 2762385
Singida
Phone: +255 26 2502320
Mtwara
Phone: +255 23 2333662
Mbeya
Phone: +255 25 2502165
Musoma
Phone: +255 28 2622551
Babati
Phone: +255 27 2531006
Lindi
Phone: +255 23 2202662
Kigoma
Phone: +255 28 2802054
Bukoba
Phone: +255 28 2220390
Iringa
Phone: +255 26 270144
Morogoro
Phone: +255 23 261 4192
Dodoma
Phone: +255 26 232 2912
Promo – MeridianBet
Kubet kumerahisishwa
Jipatie Tsh 3,500 ya kuanzia kama zawadi ya kujiunga.
Jiunge SasaVAT Tanzania ni asilimia ngapi?
Salim Jumbe
Kiwango cha VAT kinachotumika Tanzania ni 18%
Kiwango cha VAT kinachotumika Tanzania ni 18%
See lessPromo – MeridianBet
Kubet kumerahisishwa
Jipatie Tsh 3,500 ya kuanzia kama zawadi ya kujiunga.
Jiunge SasaMasharti ya TRA yakoje katika kuanzisha biashara?
Salim Jumbe
Kupitia tovuti yao wameandika hivi Mtu Binafsi Mtu binafsi awe mkazi au si mkazi anatakiwa kutembelea ofisi ya TRA ya mkoa au wilaya na kujaza fomu ya maombi ya Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN). Maombi yanaweza kufanywa pia kwa njia ya mtandao, hata hivyo mwombaji lazima afike ofisi za TRA kwSoma Zaidi
Kupitia tovuti yao wameandika hivi
Mtu Binafsi
Mtu binafsi awe mkazi au si mkazi anatakiwa kutembelea ofisi ya TRA ya mkoa au wilaya na kujaza fomu ya maombi ya Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN). Maombi yanaweza kufanywa pia kwa njia ya mtandao, hata hivyo mwombaji lazima afike ofisi za TRA kwa ajili ya kuchukuliwa alama za vidole pamoja na kupiga picha na kuweka saini.
Baada ya kupata cheti cha namba ya utambulisho wa mlipakodi mwombaji atatakiwa kuomba leseni ya biashara kutoka ofisi za Biashara katika Wilaya, Manispaa, Jiji na Wizara ya Biashara na Viwanda kwa kutegemea aina ya biashara anayotaka kuanzisha.
Hati ya Usajili:
Mtu binafsi anaweza kuamua kusajili jina la biashara kwa wakala aliyepewa kazi hiyo na Wizara ya Biashara na Viwanda anayejulikana kama Mamlaka ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA). Jina lililosajiliwa linaweza kupatikana kabla au baada ya kutoa maombi ya TIN. Jina la biashara lililosajiliwa litaonyeshwa kwenye hati ya TIN pamoja na jina la mtu huyo ikionyesha jina la mmiliki wa biashara kama (T/A).
Shirika (kampuni yenye dhima ya ukomo)
Kuanzisha shirika kunahitaji mtu aombe kupatiwa Hati ya shirika kutoka Mamlaka ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA). Wahamasishaji wa kampuni wanatakiwa kuandaa na kuwasilisha hati na Mkataba na kanuni za kampuni.
Hati ya usajili wa shirika iambatishwe kwenye maombi ya TIN pamoja na Mkataba na Kanuni za Kampuni wakati mtu anapopeleka maombi TRA.
Kampuni yenye dhima ya ukomo itaomba kupatiwa hati ya TIN kwa kujaza fomu za maombi kama ifuatavyo:
Ubia
Wabia wanatakiwa kusajili kampuni katika ofisi za BRELA na kupata hati ya usajili ambayo inaonyesha namba na majina ya wabia pamoja na mgawanyo wa hisa zao.
Udhamini
Udhamini ni mpango ambapo wadhamini wanamiliki mali lakini haihusishi ubia na kampuni.
Amana inapaswa kusajiliwa kama kampuni katika ofisi za BRELA na kupata hati ya usajili ambayo inaonesha majina na anwani za wadhamini. Kila mdhamini anapaswa kuomba kupatiwa hati ya TIN, iwapo mdhamini yeyote kati yao akiwa ameshapatiwa hati ya TIN kwa madhumuni mengine hawezi kutuma maombi mengine. Namba ya TIN aliyo nayo itatumika.
Shirika la msaada:
Shirika hili litatambulika kama shirika la msaada kwa madhumuni ya masuala ya kodi baada ya kupatiwa kibali na Kamishna Mkuu. Mwombaji anatakiwa kupata nyaraka zote muhimu kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani.
Tamko la Makadirio ya Mapato
Utatakiwa kutoa tamko la makadirio ya mapato kwa ajili ya kufanyiwa makadirio ya awali ya kodi kwa mwaka husika. Afisa wa kodi anaweza kukuhoji na kurekodi taarifa za biashara yako na taarifa zako binafsi katika ofisi ya TRA.
See lessPromo – MeridianBet
Kubet kumerahisishwa
Jipatie Tsh 3,500 ya kuanzia kama zawadi ya kujiunga.
Jiunge SasaNawezaje kupata TIN kwa ajili ya biashara yangu?
Salim Jumbe
Masharti: Picha ya pasipoti Kadi ya kitambulisho/ kitambulisho cha kazi Taratibu: Wasilisha ombi la namba ya utambulisho wa ulipa kodi Kamilisha Fomu ya Maombi ya TIN (Nakala halisi) Chukua taarifa ya makadirio (chombo kinachoomba TIN) (Nakala halisi) Jaza fomu ya udhibitisho wa mlipa kodi (nSoma Zaidi
Masharti:
Taratibu:
Promo – MeridianBet
Kubet kumerahisishwa
Jipatie Tsh 3,500 ya kuanzia kama zawadi ya kujiunga.
Jiunge SasaTIN namba ni nini?
Salim Jumbe
Namba ya utambulisho wa mlipa kodi (TIN) ni namba ya tarakimu tisa inayotumika kufuatilia namba na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa madhumuni ya kodi.
Namba ya utambulisho wa mlipa kodi (TIN) ni namba ya tarakimu tisa inayotumika kufuatilia namba na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa madhumuni ya kodi.
See lessPromo – MeridianBet
Kubet kumerahisishwa
Jipatie Tsh 3,500 ya kuanzia kama zawadi ya kujiunga.
Jiunge SasaViwango vya kodi ya VAT vikoje?
Salim Jumbe
Kodi ya Ongezeko la Thamani(VAT) hutozwa katika bidhaa na huduma stahiki kwa viwango vifuatavyo :- Na. Viwango vya VAT Aina ya bidhaa na au huduma zinazohusika Kiwango cha VAT 1 Bidhaa na huduma zinazotozwa kodi - Tanzania bara 18% 2 Uagizaji na uingizaji wa bidhaa na huduma toka nje kuingiaSoma Zaidi
Kodi ya Ongezeko la Thamani(VAT) hutozwa katika bidhaa na huduma stahiki kwa viwango vifuatavyo :-
Na.
Viwango vya VAT Aina ya bidhaa na au huduma zinazohusika
Kiwango cha VAT
0%
Promo – MeridianBet
Kubet kumerahisishwa
Jipatie Tsh 3,500 ya kuanzia kama zawadi ya kujiunga.
Jiunge SasaKodi ya ongezeko la thamani(VAT) inatozwaje?
Salim Jumbe
Kila mtu aliyesajiliwa kwenye Kodi ya Ongezeko la Thamani katika mlolongo kati ya msambazaji wa kwanza na mnunuzi au mtumiaji wa mwisho, anatozwa kodi kwenye bidhaa alizouziwa (kodi kwenye manunuzi) na atatoza kodi kwa bidhaa atakazo uza (kodi kwenye mauzo). Analipa Mamlaka ya Mapato ziada ya kodi kSoma Zaidi
Kila mtu aliyesajiliwa kwenye Kodi ya Ongezeko la Thamani katika mlolongo kati ya msambazaji wa kwanza na mnunuzi au mtumiaji wa mwisho, anatozwa kodi kwenye bidhaa alizouziwa (kodi kwenye manunuzi) na atatoza kodi kwa bidhaa atakazo uza (kodi kwenye mauzo). Analipa Mamlaka ya Mapato ziada ya kodi kwenye mauzo juu ya kodi kwenye manunuzi, au anarudishiwa ziada ya kodi kwenye manunuzi juu ya kodi kwenye mauzo. Katika mfumo huu biashara huwa haziathiriki isipokuwa mfanyabiashara anatakiwa kukusanya kodi hiyo kutoka kwa mnunuzi na kuiwasilisha TRA.
See lessPromo – MeridianBet
Kubet kumerahisishwa
Jipatie Tsh 3,500 ya kuanzia kama zawadi ya kujiunga.
Jiunge SasaVAT ni nini?
Salim Jumbe
VAT ni kifupi cha Value Added Tax, kwa kiswahili ni Kodi ya Ongezeko la thamani. Kodi ya Ongezeko la Thamani ni nini? Kodi ya Ongezeko la Thamani ni kodi ya mlaji inayotozwa katika bidhaa zinazostahili kutozwa kodi, ikiwa ni pamoja na huduma, mali zisizohamishika na shughuli yoyote ya kiuchumi wakaSoma Zaidi
VAT ni kifupi cha Value Added Tax, kwa kiswahili ni Kodi ya Ongezeko la thamani.
Kodi ya Ongezeko la Thamani ni nini?
Kodi ya Ongezeko la Thamani ni kodi ya mlaji inayotozwa katika bidhaa zinazostahili kutozwa kodi, ikiwa ni pamoja na huduma, mali zisizohamishika na shughuli yoyote ya kiuchumi wakati wowote thamani inapoongezeka katika kila hatua ya uzalishaji na katika hatua ya mwisho ya mauzo. Kodi ya Ongezeko la Thamani inatozwa kwa bidhaa zote zinazozalishwa ndani na huduma na kwenye maduhuli. Kodi ya Ongezeko la Thamani anatozwa mtu aliyesajiliwa kulipa Kodi ya Ongezeko la Thamani tu.
Mawanda ya Kodi ya Ongezeko la Thamani ni yapi?
Kodi ya Ongezeko la Thamani itatozwa katika usambazaji wowote wa bidhaa, huduma na bidhaa zisizohamishika za shughuli yoyote ya kiuchumi Tanzania Bara ambapo ni usambazaji unaotozwa kodi unaofanywa na mlipa kodi katika shughuli ya kiuchumi anayofanya. Uingizaji wa bidhaa zinazokatwa kodi kutoka sehemu yoyote nje ya Tanzania Bara zitatozwa Kodi ya Ongezeko la Thamani na Sheria za Kawaida za Forodha na taratibu zitatumika. Bidhaa zote zitakazotumika nje ya Tanzania Bara hazitatozwa Kodi ya Ongezeko la Thamani baada ya kupata uthibitisho. Kodi ya Ongezeko la Thamani itatozwa kwa bidhaa na huduma zinazotozwa kodi. Viwango sanifu vya Kodi ya Ongezeko la Thamani ni 18% na 0% kwa bidhaa zinazosafirishwa nje ya nchi.
See less