Jiunge MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Login MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Umesahau password yako?. Andika email yako hapo chini alafu bonyeza 'Reset'. Utapokea link katika email yako kwa ajili ya kutengeneza password mpya.
Tafadhali elezea kwa nini unahisi chapisho hili linapaswa kuripotiwa
Unaweza kujua tabia ya mtu kwa kuangalia mwandiko wake?
Salim Jumbe
Katika blog ya bwaya aliwahi kuandika kuhusu aina ya miandiko na siri zilizofichwa nani yake, aliandika hivi 1. Mwandiko wa kukandamiza: Maana yake akiandika nundu nundu za herufi zinaonekana upande wa pili wa karatasi. Ni dalili ya fikira chanya, kujiamini (hata kunakozidi mipaka) jeuri saa nyinginSoma Zaidi
Katika blog ya bwaya aliwahi kuandika kuhusu aina ya miandiko na siri zilizofichwa nani yake, aliandika hivi
1. Mwandiko wa kukandamiza: Maana yake akiandika nundu nundu za herufi zinaonekana upande wa pili wa karatasi. Ni dalili ya fikira chanya, kujiamini (hata kunakozidi mipaka) jeuri saa nyingine, majigambo.
2. Kuandika juu juu kwa kuparua: Kutokujiamini, na tabia ya kufikiria mambo kinyume. Yaani kufikiria ubaya, udhaifu wa jambo zaidi.
3. Mwandiko unaolalia kulia: Mwandishi anafikiria anakoenda zaidi, anafikiria mbele. Mara nyingi hana muda wa kutafakari makosa yaliyowahi kumtokea kwenye maisha yake.
4. Mwandiko unaolalia kushoto: Hufikiria jana na yaliyopita. Hujilaumu kwa makosa aliyowahi kuyafanya.
5. Mwandiko unaoongozeka ukubwa kadiri unavyoandika
6. Mwandiko unaopungua ukubwa wa herufi kadiri unavyoandika
7. Mwandiko usiobadilika kadiri unavyoandika
8. Herufi kubwa kubwa zenye urefu na upana sawa
9. Herufi kubwa ndefu nyembamba
10. Herufi pana fupi (nene):
11. Mwandiko mdogo
12. Mwandiko mkubwa (Jiandiko)
13. Mwandiko unaogeuka geuka, mkubwa mara mdogo nk
14. Mwandiko unaopungua ukubwa kadiri unavyoandika
soma kwa urefu zaidi
See lessPromo – MeridianBet
Kubet kumerahisishwa
Jipatie Tsh 3,500 ya kuanzia kama zawadi ya kujiunga.
Jiunge SasaKwanini watu huwasema vibaya wenzao?
Salim Jumbe
Sababu ni kwamba binadamu tunapenda kuonekana wa thamani hata kama mara nyingine thamani hiyo tunayoidai hatunayo. Tunalo hitaji la kuona kuwa wengine wanatuheshimu, kututhamini na kuwa na maoni chanya kutuhusu. Kinachotofautiana, ni kiwango. Hebu fikiria. Mfanyakazi mwenzako anakujia na kuuponda utSoma Zaidi
Sababu ni kwamba binadamu tunapenda kuonekana wa thamani hata kama mara nyingine thamani hiyo tunayoidai hatunayo. Tunalo hitaji la kuona kuwa wengine wanatuheshimu, kututhamini na kuwa na maoni chanya kutuhusu. Kinachotofautiana, ni kiwango.
Hebu fikiria. Mfanyakazi mwenzako anakujia na kuuponda utendaji wako wa kazi uso bin uso. Bila adabu. Bila staha. Ama mwenzi wako anakukosoa mbele za watu kuhusu mambo ambayo yanawahusu ninyi wawili. Ama mkuu wako wa kazi anapokuhamakia kikaoni. Ama rafiki yako anakusemea mbovu mtaani. Kwa wengi wetu, japo katika viwango tofauti, itauma…. endelea kusoma
See lessPromo – MeridianBet
Kubet kumerahisishwa
Jipatie Tsh 3,500 ya kuanzia kama zawadi ya kujiunga.
Jiunge SasaHaiba ni nini?
Emmanuel Magessa
Haiba ni nini? Watu wengine watafikiria tunazungumzia mwonekano wa mtu kimavazi. Lakini haiba ni neno pana zaidi ya mwonekano wa mtu kwa nje. Haiba ni jumla ya tabia za mtu zinazotokana na kile anachofikiri, anachopenda, anavyojichukulia yeye mwenyewe, anavyowachukulia watu wengine na kadhalika. HaySoma Zaidi
Haiba ni nini? Watu wengine watafikiria tunazungumzia mwonekano wa mtu kimavazi. Lakini haiba ni neno pana zaidi ya mwonekano wa mtu kwa nje. Haiba ni jumla ya tabia za mtu zinazotokana na kile anachofikiri, anachopenda, anavyojichukulia yeye mwenyewe, anavyowachukulia watu wengine na kadhalika. Haya yote hujenga mwonekano wa mtu unaopimika (tabia) kama vile anavyoongea na watu, anavyodhibiti hasira zake, anavyofanya maamuzi, anavyoweza kuwa mwaminifu, anavyoweza kutunza siri moyoni, anavyoweza kukabiliana na changamoto, anavyovaa na mambo kama hayo mengi mengi mengi.
Haiba hii tunayoizungumzia hujengwa na mambo mengi. Tunaweza kutaja kurithi kama sehemu muhimu ya utengenezaji wa haiba. Hapa tunazungumzia kemikali zinazoongoza mienendo ya mwili ama homoni (kwa kutohoa). Ujue wingi ama uchache wa homoni fulani huchangia kujengeka kwa tabia fulani. Pia mazingira alimokulia mtu, kwa maana ya watu na malezi aliyopata na kadhalika.
Vile vile ni vyema kujua kuwa haiba ya mtu hubadilika kuendana na umri. Kila umri unazo changamoto zake zinazoathiri haiba ya mtu husika. Haiba yangu nilipokuwa na umri wa miaka mitano siyo niliyokuwa nayo nikiwa na umri wa miaka kumi na mitano na siyo niliyo nayo hivi sasa. Kwa sababu haiba yangu inabadilika kwa umri. Nikioa haiba yangu pia itabadilika…. endelea kusoma hapa Bwaya blog
See lessPromo – MeridianBet
Kubet kumerahisishwa
Jipatie Tsh 3,500 ya kuanzia kama zawadi ya kujiunga.
Jiunge SasaJe, kuna ulazima wa kuwa na dini?
Emmanuel Magessa
Kuna umuhimu mkubwa sana wa kuwa na dini na sio ulazima. Dini sio kitu kinachoweza kukufikisha mbinguni. Dini ni kitu kinachotumiaka kuwaweka watu pamoja ili watu waweze kuwa na nia inayofanana na kushirikiana kuweza kufikia malengo ya kiroho au malengo ya kuishi maisha mema. Je kuna ulazima wa kuwaSoma Zaidi
Kuna umuhimu mkubwa sana wa kuwa na dini na sio ulazima. Dini sio kitu kinachoweza kukufikisha mbinguni. Dini ni kitu kinachotumiaka kuwaweka watu pamoja ili watu waweze kuwa na nia inayofanana na kushirikiana kuweza kufikia malengo ya kiroho au malengo ya kuishi maisha mema.
Je kuna ulazima wa kuwa na dini?. Hakuna ulazima ila kuna umuhimu.
See lessPromo – MeridianBet
Kubet kumerahisishwa
Jipatie Tsh 3,500 ya kuanzia kama zawadi ya kujiunga.
Jiunge SasaUnawezaje kutengeneza sarafu bandia?
Kwa nn unataka kutengeneza sarafu na sio noti, sarafu si utaishia tu kupata hasara. Lakini inabidi ujue kwanza si halali kisheria na ukikamatwa utapata adhabu kali sana. Kutengeneza pesa bandia nadhani inaanzia na ubunifu wa mtu alioamua kuutumia vibaya au isivyo halali. angalia video inapoanza hapoSoma Zaidi
Kwa nn unataka kutengeneza sarafu na sio noti, sarafu si utaishia tu kupata hasara.
Lakini inabidi ujue kwanza si halali kisheria na ukikamatwa utapata adhabu kali sana.
Kutengeneza pesa bandia nadhani inaanzia na ubunifu wa mtu alioamua kuutumia vibaya au isivyo halali. angalia video inapoanza hapo katumia tu vifaa vingi vya kawaida kutengeneza izo pesa.
See lessPromo – MeridianBet
Kubet kumerahisishwa
Jipatie Tsh 3,500 ya kuanzia kama zawadi ya kujiunga.
Jiunge SasaUlishawahi kujutia kuwa na watoto?
Glory Joseph
Kupitia bbc Rachel anasema hivi kuhusu topic hii “Kama ningeweza kurudisha muda nyuma nisingekuwa na watoto” anasema Rachel ambaye sasa ana umri wa miaka 50. Ana watoto watatu – mdogo zaidi ana miaka 17 – na kwa muda mwingi yeye amekuwa mama mjane. “Kuna nyakati ambapo sikujisikia kukomaa kwa kutoshSoma Zaidi
Kupitia bbc Rachel anasema hivi kuhusu topic hii
“Kama ningeweza kurudisha muda nyuma nisingekuwa na watoto” anasema Rachel ambaye sasa ana umri wa miaka 50.
Ana watoto watatu – mdogo zaidi ana miaka 17 – na kwa muda mwingi yeye amekuwa mama mjane.
“Kuna nyakati ambapo sikujisikia kukomaa kwa kutosha kuwa na jukumu kwa mtu fulani, mtu huyu mdogo aliyehitaji mimi kuwapo,” anasema.
“Ilionekana tu kama mzunguko usio na mwisho wa kuweka chupa au chakula katika kinywa chao ili itatoke kwenye mwisho mwingine – na kwa wakati gani jambo lolote litakuwa la kufurahisha?
“Nilihisi tu kama kupiga kelele kwamba kwa kweli sio yote yamevunjika. Kama wewe ni kweli wa uzazi basi hiyo ni nzuri una kila kitu ulichotaka, lakini wakati usio mama wote uliyofanya ni mtego wewe mwenyewe. ”
Rachel anakubali kwamba hakufikiria kwa bidii juu ya jinsi kuwa na watoto bila kuathiri maisha yake – alikuwa amegundua, hakutaka kuwa na.
“Lakini ninahisi kuwa na hatia kwa kusema hivyo, kwa sababu ninawapenda watoto wangu sana,” anasema.
“Unajisikia kama hukuwa mama mzuri na ni hatia unayobeba kila wakati, haujawahi kamwe na unajiuliza kama wanajua.
“Lakini maisha haipaswi kuwa juu ya kuacha maisha yako, uhuru wako, ili waweze kuwa na maisha.”
Hii ni ngumu kwa yeye kukubali, kwa sababu “watu wanadhani kuwa wewe si mtu mzuri”.
Rachel ana hamu kwa wanawake wanaojisikia njia ile ile ya kutopigwa vibaya.
“Nilisikia peke yangu .. Nilihisi kama kuna kitu kibaya na mimi. Ikiwa ningeweza kuzungumza juu yake na mtu fulani alielewa, ningeona ni rahisi sana kukabiliana na mama.”
habari hii imetafsriwa kutoka bbc
See lessPromo – MeridianBet
Kubet kumerahisishwa
Jipatie Tsh 3,500 ya kuanzia kama zawadi ya kujiunga.
Jiunge SasaUhai ulianzia wapi?
Emmanuel Magessa
Wanasayansi wengi wanaoamini mageuzi watakuambia kwamba uhai ulianza mabilioni ya miaka iliyopita kwenye ukingo wa kidimbwi cha kale kilichojaa maji wakati wa kupwa au katika sehemu za chini ya bahari. Wao huhisi kwamba katika maeneo yasiyojulikana kama hayo, kemikali zilijikusanya na kuwa vitu vinaSoma Zaidi
Wanasayansi wengi wanaoamini mageuzi watakuambia kwamba uhai ulianza mabilioni ya miaka iliyopita kwenye ukingo wa kidimbwi cha kale kilichojaa maji wakati wa kupwa au katika sehemu za chini ya bahari. Wao huhisi kwamba katika maeneo yasiyojulikana kama hayo, kemikali zilijikusanya na kuwa vitu vinavyofanana na mapovu,vikafanyiza molekuli tata, na kuanza kujigawanya-gawanya. Wanaamini kwamba uhai wote duniani ulijitokeza wenyewe tu kutokana na chembe “sahili,” moja au zaidi.
Wanasayansi wengine wanaoheshimika ambao pia wanaunga mkono mageuzi hawakubaliani na wazo hilo. Wanakisia kwamba chembe za kwanza au angalau sehemu zake kuu zilikuja duniani kutoka anga la nje.
Licha ya jitihada zao nyingi, wanasayansi hawajaweza kuthibitisha kwamba uhai unaweza kutokea ghafla kutokana na molekuli zinazodhaniwa zilitokeza uhai. Katika mwaka wa 2008, Alexandre Meinesz, Profesa wa Biolijia, alizungumzia utata huo. Alisema kwamba kwa zaidi ya miaka 50 iliyopita, “hakuna uthibitisho wowote uliopatikana kupitia majaribio yaliyofanywa unaounga mkono nadharia ya kwamba uhai ulitokea ghafla Duniani kutokana na molekuli fulani, wala hakuna maendeleo ya kisayansi yanayoweza kuthibitisha hilo.”
Siku zote uhai hutokana na uhai ambao tayari upo. Watafiti wamegundua kwamba ili chembe iendelee kuwa hai, angalau aina tatu tofauti za molekuli tata lazima zifanye kazi pamoja – DNA au deoksiribonyuklia asidi, RNA( ribonucleic acid), na protini. Leo, ni wanasayansi wachache wanaoweza kudai kwamba chembe kamili iliyo hai iliyojitokeza yenyewe kutokana na mchanganyiko wa kemikali zisizo hai.
Wanasayansi wengi huhisi kwamba huenda uhai ulijitokeza wenyewe kwa sababu ya jaribio fulani lililofanywa kwa mara ya kwanza mwaka 1953. Mwaka huo Stanley L. Miller aliweza kutengeneza asidi – amino, kemikali za msingi zinazofanyiza protini,kwa kupitisha nguvu za umeme ndani ya mchanganyiko wa gesi zilizodhaniwa kuwa zingewakilisha anga la Dunia. Toka wakati huo, asidi – amino zimepatikana pia katika vimondo. Ugunduzi huu haumaanishi kwamba kemikali za msingi za uhai zinaweza kujitokeza zenyewe.
Robert Shapiro, aliyekuwa profesa wa kemia katika Chuo Kikuu cha New York, anasema, “ Baadhi ya waandishi wameamini kwamba kemikali za msingi za uhai zinaweza kutengenezwa kwa urahisi kwa kutumia majaribio kama yale ya Miller na kwamba zinapatikana katika vimondo. Hata hivyo sivyo ilivyo.” * 1
Fikiria molekuli ya RNA. Imefanyizwa na molekuli ndogo zinazoitwa nukliotidi. Nukliotidi ni aina tofauti ya molekuli na ni tata zaidi kidogo kuliko asidi – amino. Shapiro anasema kwamba “ hakuna nukliotidi za aina yoyote zinazoripotiwa kuwa zilitokana na majaribio yanayohusu umeme wala katika uchunguzi wa vimondo. Pia anasema kwamba uwezekano wa molekuli kujifanyiza bila mpangilio maalum na kujikusanya toka kemikali nyingi za msingi “ ni mdogo sana hivi kwamba hata kama ungetokea mahali popote katika ulimwengu unaonekana ungeonwa bahati.
Mtafiti Hubert P. Yockey, anayeunga mkono fundisho la mageuzi ana maelezo zaidi. Anasema: “Haiwezekani kwamba chanzo cha uhai ni ‘protini tu.’”* 2 RNA inahitajika kutengeneza protini, hata hivyo, protini zinahusika katika utengenezaji wa RNA.
Je, kuna uwezekano wowote kwamba protini na molekuli ya RNA kutokea mahali pamoja kwa wakati uleule na kufanyiza uhai unaoweza kutokeza chembe ambazo zinaweza kuzaa na kuendeleza uhai?
Yaelekea uwezekano wa jambo hilo kujitokeza lenyewe, kukiwa na mchanganyiko usio na mpangilio maalumu wa protini na RNA, ni mdogo sana, anasema Dkt. Carol Creland ; mshiriki wa NASA ( National Aeronautics and Space Administration’s Astrobilogy Institute).
1* Profesa Shapiro haamini kwamba uhai ulitokana na Muumba. Anaamini kuwa uhai ulijitokeza wenyewe kwa njia fulani ambayo bado haijaeleweka. Mwaka wa 2009 wanasayansi katika Chuo Kikuu cha Manchester, Uingereza,waliripoti kwamba wametengeneza nukliotidi katika maabara yao. Hata hivyo, Shapiro anasema kwamba viambatano vyao “bila shaka havifikii viwango vyangu vinavyokubalika vya kutengeneza RNA.”
2* Dkt. Cleland haamini masimulizi kuhusu uumbaji wa Mungu . Anaamini kwamba uhai ulijitokeza wenyewe katika njia fulani ambayo bado haijaeleweka vizuri.
UKWELI KUHUSU UCHUNGUZI WA KISAYANSI NA UHAI (UUMBAJI)
Ukweli wa mambo: Utafiti wote wa kisayansi umeonyesha kwamba uhai hauwezi kujitokeza wenyewe kutokana na kitu kisicho hai.
Swali : Kuna msingi gani wa kisayansi unaowafanya watu waseme kwamba chembe ya kwanza ilitokana na kemikali zisizo hai?
Ukweli wa mambo: Wanasayansi wamebuni katika maabara, hali za kimazingira ambazo wanaamini zilikuwako mapema katika historia ya dunia.Katika majaribio hayo, wanasayansi fulani wametengeneza baadhi ya molekuli zinazopatikana katika viumbe hai.
Swali: Ikiwa kemikali katika jaribio hilo zinawakilisha mazingira ya awali ya dunia na molekuli inayotokezwa inawakilisha chembe za msingi za uhai, mwanasayansi aliyefanya jaribio hilo anawakilisha nani au nini? Je, anawakilisha matukio yaliyojitokeza kiholela au mtu fulani mwenye akili?
Ukweli wa mambo: Ili chembe iendelee kuwa hai, lazima protini na molekuli ya RNA zishirikiane.Wanasayansi wamekiri kwamba haiwezekani kuwa molekuli ya RNA ilijitokeza yenyewe. Uwezekano
wa hata protini moja kujitokeza yenyewe ni mdogo sana. Haiwezekani kamwe kwamba molekuli ya RNA na protini zingeweza kujitokeza zenyewe mahali palepale, wakati uleule na ziweze kushirikiana.
Swali: Ni nini kinachohitaji imani zaidi—kuamini kwamba chembe pamoja na mamilioni ya sehemu zake zinazoshirikiana kwa ustadi wa hali ya juu zilijitokeza zenyewe au kwamba chembe zilibuniwa
na Muumba mwenye akili?
chanzo: Jamiiforums
See lessPromo – MeridianBet
Kubet kumerahisishwa
Jipatie Tsh 3,500 ya kuanzia kama zawadi ya kujiunga.
Jiunge SasaUnawashauri nini vijana wa siku hizi?
Salim Jumbe
Tumia muda wako vizuri, fanya unachopenda hautakuwa kijana milele
Tumia muda wako vizuri, fanya unachopenda hautakuwa kijana milele

See lessPromo – MeridianBet
Kubet kumerahisishwa
Jipatie Tsh 3,500 ya kuanzia kama zawadi ya kujiunga.
Jiunge SasaDalili gani zinaweza kunionesha kuwa nimekua mtu mzima tayari?
Lameck Alen
Unaona kulala ni bora kuliko mitoko ya usiku Unasamehe zaidi Unaheshimu vitu viliyo tofauti Haulazimishi mapenzi Hauwasemi wengine Saa nyingine unaamua kuwa kimya kuliko kujiingiza kwenye ugomvi Furaha yako haitegemei watu wengine bali wewe mwenyewe
Unaona kulala ni bora kuliko mitoko ya usiku
Unasamehe zaidi
Unaheshimu vitu viliyo tofauti
Haulazimishi mapenzi
Hauwasemi wengine
Saa nyingine unaamua kuwa kimya kuliko kujiingiza kwenye ugomvi
Furaha yako haitegemei watu wengine bali wewe mwenyewe
See lessPromo – MeridianBet
Kubet kumerahisishwa
Jipatie Tsh 3,500 ya kuanzia kama zawadi ya kujiunga.
Jiunge SasaMambo gani ambayo yanaweza kunisaidia siku moja?
Lameck Alen
Msikilize vizuri jinsi mtu anavyowaongelea watu wengine ukiwa nae. Hiyo inaweza kuonesha jinsi anavyokuongelea kwa watu wengine. Kwa kawaida mtu huwa anachezesha sana mikono wakati anelezea stori ya kweli. Akiwa anasema uongo mikono inakua imetulia. Wanawake huwa wanapenda wanaume wanaowafanya wacheSoma Zaidi
Msikilize vizuri jinsi mtu anavyowaongelea watu wengine ukiwa nae. Hiyo inaweza kuonesha jinsi anavyokuongelea kwa watu wengine.
Kwa kawaida mtu huwa anachezesha sana mikono wakati anelezea stori ya kweli. Akiwa anasema uongo mikono inakua imetulia.
Wanawake huwa wanapenda wanaume wanaowafanya wacheke, hii tabia inamfanya mtu kuwa na mvuto zaidi.
Kama unakohoa sana, nyanyua mikono yako juu ya kichwa chako tatizo hilo litakwisha.
Njia rahisi ya kumfanya mtu aseme ukweli wote. Endelea kunyamaza, atajielezea mwenyewe.
Kujua kama betri ziko vizuri, zidondoshe kwenye sakafu. Kama zikidunda ziko vizuri, kama zikidunda zaidi ya mara moja basi zimeisha.
Waza kama upo na mtu unayempenda wakati wa kupiga picha. Itakupa tabasamu halisi.
Ukiweka yai kwenye maji, likielea ujue sio zima. Kama likizama basi liko vizuri.
See less