Jiunge MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Login MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Umesahau password yako?. Andika email yako hapo chini alafu bonyeza 'Reset'. Utapokea link katika email yako kwa ajili ya kutengeneza password mpya.
Tafadhali elezea kwa nini unahisi chapisho hili linapaswa kuripotiwa
Nini mawazo yako kuhusu uwepo wa mungu?
Emmanuel Magessa
” Kwa vyovyote kuna nguvu inayoendesha haya mambo, kuna nguvu ambayo ni ya ajabu katika hufanyaji kazi wake. nguvu hii wakristo huuita Mungu na waislamu huiita Allah, kila mtu hujiona yuko sahihi lakini wanasayansi ndio basi kwani wao huiita Nguvu tu kama ilivyo. siku zote wanasayansi hukataa kuwepoSoma Zaidi
” Kwa vyovyote kuna nguvu inayoendesha haya mambo, kuna nguvu ambayo ni ya ajabu katika hufanyaji kazi wake.
nguvu hii wakristo huuita Mungu na waislamu huiita Allah, kila mtu hujiona yuko sahihi lakini wanasayansi ndio basi kwani wao huiita Nguvu tu kama ilivyo. siku zote wanasayansi hukataa kuwepo kwa mtu anayeitwa Mungu lakini hukubali kuwepo kwa nguvu na wanasema kuwa nguvu haiwezi kubadirishwa wala kuharibiwa na wala kupindishwa!
uwepo wa nguvu unaonekana tu wenyewe, biblia inasema tumeumbwa kwa mfano wa Mungu kwa hiyo basi na sisi ni nguvu au Roho kama ilivyo hiyo Mungu.
sisi kama binadamu mawazo yetu, maneno (kauli) yetu, yananguvu kuliko tunavyofikiri na hubadirisha na kutupangia maisha yetu. kwamfano, Tanzania sio nchi masikini na wala watanzania sio masikini bali ni nguvu ya Hoja ya watu fulani na sisi kuipokea na kukubali ndivyovinatufanya kuonekana masikini – Nguvu hizo!
Dini nyingi huamini kwamba nguvu hiyo (Mungu) inahasira na ….. endelea kusoma
See lessPromo – MeridianBet
Kubet kumerahisishwa
Jipatie Tsh 3,500 ya kuanzia kama zawadi ya kujiunga.
Jiunge SasaJe kuna Mungu?
Emmanuel Magessa
Zamani kabla hawajaja wakoloni(wazungu na waarabu) hakukuwa na kitu kinachoitwa Mungu,wao waliamini ktk Nguvu kuu.Ndiyo maana utakuta wengine waliamini ktk miti wengine katika majabali,na kikubwa ndugu zangu ieleweke wengi wa watu wa zamani waliamini zaidi katika kanuni za kimaumbile ndiyo ilikuwa mSoma Zaidi
Zamani kabla hawajaja wakoloni(wazungu na waarabu) hakukuwa na kitu kinachoitwa Mungu,wao waliamini ktk Nguvu kuu.Ndiyo maana utakuta wengine waliamini ktk miti wengine katika majabali,na kikubwa ndugu zangu ieleweke wengi wa watu wa zamani waliamini zaidi katika kanuni za kimaumbile ndiyo ilikuwa msingi wao.
Kwa mtazamo wangu wengi hatumwelewi mungu sana tunachofanya ni kujenga hofu kwa Mungu,linapokuja suala la kutaka kumjua huyo mungu kwa undani utaambiwa unakufuru,sasa mi huwa ninajiuliza iweje utake kujua asili za aliyetuumba uambiwe unakufuru? Haingii akilini umuulize mzazi wako asili yake wapi akuambie unakufuru.
ninaweza kukubaliana na wanasayansi … endelea kusoma
See lessPromo – MeridianBet
Kubet kumerahisishwa
Jipatie Tsh 3,500 ya kuanzia kama zawadi ya kujiunga.
Jiunge SasaUbatizo ni nini?
Emmanuel Magessa
Ubatizo ni nini? A. -Ni ishara ya nje inayoonyesha kuwa mtu ameacha njia zake za zamani na ameanza kumfuata Yesu Kristo. -Ni ishara ya kufa kuzikwa na kufufuka na Kristo. Warumi 6:4 Wakolosai 2:12 B. Maana ya neno “BATIZA”. Neno batiza limetokana na neno la Kiyunani,”BAPTIDZO” lenye maana zamisha auSoma Zaidi
Ubatizo ni nini?
See lessA. -Ni ishara ya nje inayoonyesha kuwa mtu ameacha njia zake za zamani na ameanza kumfuata Yesu Kristo.
-Ni ishara ya kufa kuzikwa na kufufuka na Kristo.
Warumi 6:4
Wakolosai 2:12
B. Maana ya neno “BATIZA”. Neno batiza limetokana na neno la Kiyunani,”BAPTIDZO” lenye maana zamisha au zika kabisa. Hivyo neno batiza maana yake ni zamisha, auzika kabisa.
Promo – MeridianBet
Kubet kumerahisishwa
Jipatie Tsh 3,500 ya kuanzia kama zawadi ya kujiunga.
Jiunge SasaKucheza kamari ni dhambi?
Emmanuel Magessa
Katika Ulimwengu wa Sasa,Kumekuwepo na Wimbi la Michezo Mingi inayojulikana kama MICHEZO YA KAMARI(LOTTERING,BETTING,GAMBLING)iliyofanikiwa Kuchukua Ulimwengu mzima au Inaweza ikawa Taifa zima zima Kuvutiwa Kushiriki Katika Michezo hiyo wakiwa na Shauku ya Kujishindia Mamilioni ya Pesa na Matajiri kSoma Zaidi
Katika Ulimwengu wa Sasa,Kumekuwepo na Wimbi la Michezo Mingi inayojulikana kama MICHEZO YA KAMARI(LOTTERING,BETTING,GAMBLING)iliyofanikiwa Kuchukua Ulimwengu mzima au Inaweza ikawa Taifa zima zima Kuvutiwa Kushiriki Katika Michezo hiyo wakiwa na Shauku ya Kujishindia Mamilioni ya Pesa na Matajiri kwa Ghafla au kwa siku Moja
Jambo hili limepelekea Kupendwa Sana Na watu wa aina zote hata na watu wanaojiita ni watu wa Mungu au Wakristo wengine ni Maaskofu,Wachungaji au Waumini mbalimbali wa dini zinazojiita za kikristo au zinazomuamini Mungu.Na hasa mijadala hii ipo karibu ulimwenguni pote ikijadiliwa bila kufikia maamuzi
Katika Nchi Yetu ya Tanzania,Kumekuwepo na Hii Michezo ya Bahati nasibu Kama TATU MZUKA Au BIKO AU MKEKA ambapo mtu atatoa pesa yake kama ni 500 au 1000 n.k kushiriki katika droo mbalimbali za kutafuta mshindi wa kujishindia Kitita cha Pesa Mil 60 mpaka mil 100.Na wakati mwingine hata kushinda pesa hizi ndogo ndogo.Na Matangazo ya biashara ya hii michezo yanatawala kwenye luninga channel zote na redio.Matangazo haya yanashindana na mashirika ya simu!Hii ni ishara kuna PESA nyingi sana zinazalishwa kwenye hii michezo Sasa Je,Tunajiuliza Ushiriki wa Mkristo katika Michezo hii ni halali kibiblia? Kabla Sijaanza Kueleza Ni halali au Si halali.Labda Nianze na Hoja zao kuu wanayokuja nayo hawa wakristo wanaoshiriki Michezo hii (Ni Hoja ya Kibiblia)
HOJA YA KWANZA HAKUNA ANDIKO LINALOKATAZA KUCHEZA BAHATI NASIBU(LOTTERY) AU KAMARI(GAMBLING) AU KUBETI KWENYE BIBLIA
Ni kweli hakuna Andiko la moja kwa Moja kama tunavyotaka kuona Kamari au Betting au Bahati nasibu lakini Ipo mifano ya wazi kabisa kwenye biblia inayonyesha Michezo ya Kamari Kufanyika.Nitaeleza mbeleni wakati natoa sababu za sisi kutoshiriki michezo kama hii
Pia Ni Muhimu Kufahamu,Si kweli Kwamba Kwa kuwa Neno Lottery au Gambling halipo direct kama neno lilivyo kwenye biblia basi tuseme hicho kitu hakipo au hatuwezi Kukiamini kama Maana yake inaelekea na Makatazo yaliyopo kwenye Biblia
See lessPromo – MeridianBet
Kubet kumerahisishwa
Jipatie Tsh 3,500 ya kuanzia kama zawadi ya kujiunga.
Jiunge SasaAina za maombi ya kufunga ni zipi?
Emmanuel Magessa
1. Mfungo kamili Katika mfungo huu hakuna kula kabisa chakula kigumu bali waweza kunywa maji au kimiminika chochote cha kukusupport. Siku ngapi waweza kufunga mfungo wa aina hii unategemea na neema na malengo yako katika mfungo huo. Wengine huenda siku moja, mbili, tatu, wiki, n.k n.k 2. Mfungo nusuSoma Zaidi
1. Mfungo kamili
Katika mfungo huu hakuna kula kabisa chakula kigumu bali waweza kunywa maji au kimiminika chochote cha kukusupport.
Siku ngapi waweza kufunga mfungo wa aina hii unategemea na neema na malengo yako katika mfungo huo. Wengine huenda siku moja, mbili, tatu, wiki, n.k n.k
2. Mfungo nusu
Mfungo nusu huanzia saa 12 asbh hadi saa 9 mchana au kuanzia jua linapoibuka hadi linapozama. Mfungo ambao madhehebu mengine wamewazoeza waumini wao kuufanya. Wengine wameweza kuufanya kila ijumaa. Madhehebu ambayo yamewazoesha watu wao kufunga angalau kila wiki mara moja wameweza kuwa na mafanikio makubwa sana katika kuzifungua nira na vifungo mbali mbali
3. Mfungo wa Daniel
Daniel alifunga mifungo miwili ya aina yake;• Katika Sura ya I Daniel alifunga alikula mboga mboga tu (Yaweza kuwa alikula mboga mboga na juisi Fulani Fulani)
• Katika sura ya 10 Daniel alifunga kwa siku 21 kwa kutokula chakula kitamu, wala nyama wala divai haikuingia kinywani mwake”
See lessPromo – MeridianBet
Kubet kumerahisishwa
Jipatie Tsh 3,500 ya kuanzia kama zawadi ya kujiunga.
Jiunge SasaNeema ni nini?
Emmanuel Magessa
Katika Biblia Agano Jipya neno “Neema” limetokana na maneno mawili ya Kigiriki ambayo yametafsiriwa kama neema. Neno la kwanza ni “Charis” (khar’-ece) lenye maana ya upendeleo, wema, uwezesho; na neno hili limejitokeza katika Biblia katika Agano Jipya mara 157. Kutokana na neno hili la kwanza tunaweSoma Zaidi
Katika Biblia Agano Jipya neno “Neema” limetokana na maneno mawili ya Kigiriki ambayo yametafsiriwa kama neema. Neno la kwanza ni “Charis” (khar’-ece) lenye maana ya upendeleo, wema, uwezesho; na neno hili limejitokeza katika Biblia katika Agano Jipya mara 157. Kutokana na neno hili la kwanza tunaweza kusema kuwa neema ni upendeleo na wema wa Mungu kwa mwanadamu ambao umekuja kwa njia ya Yesu Kristo.
Neno la pili la Kigiriki lililotafsiriwa kama neema katika Agano Jipya ni “Charisma” (khar’-is-mah) lenye maana ya karama au kipawa cha neema kinachotolewa bure, au upendeleo asiostahili mtu. Neno hili katika Agano Jipya limejitokeza mara 17. Na katika maana hii, karama na vipawa vyote vya Roho vinahesabiwa kuwa ni neema ya Mungu kwa mwanadamu.
Nini maana ya neema sasa?
Neema ni kipawa cha Mungu kwa mwanadamu kinachotolewa bure ambacho huachilia upendeleo na wema wa Mungu kwa mwanadamu. Ni upendeleo wa Mungu kwa mwanadamu asiostahili mtu ambao Mungu anauachilia kwa mwanadamu akionyesha wema wake kutoka katika pendo lake lisilokuwa na sababu wala masharti. Kwa kifupi tunaweza kusema kuwa, neema ni kustahilishwa wema wa Mungu pasipo kustahili kwa sababu ya pendo lake kwa mwanadamu.
Kustahilishwa pasipo kustahili nini maana yake:
See lessTangu mwanadamu alipomtenda Mungu dhambi hakustahili tena kupata wema wa Mungu maishani mwake isipokuwa hukumu kwa sababu ya dhambi zake. Lakini Mungu kwa njia ya Yesu Kristo amemstahilisha mwanadamu mema na wema wake wote si kwa sababu ya matendo yake bali kwa sababu ya Yesu Kristo kufa kwa ajili ya mwanadamu
Promo – MeridianBet
Kubet kumerahisishwa
Jipatie Tsh 3,500 ya kuanzia kama zawadi ya kujiunga.
Jiunge SasaYesu ni Mungu?
Emmanuel Magessa
Haya ni maoni ya mdau asiyependa jina lake lijulikane. Nimeyatundika hapa kwa sababu ya uzito wa anachokisema. Tafadhali soma na kama unaweza changia maoni yako tuelimike. Nimshukuru sana kwa kutumia muda wake kuandika maoni yake na hapa namnukuu: MAKANISA ya Kikristo yanafunza ya kuwa Yesu Kristo sSoma Zaidi
Haya ni maoni ya mdau asiyependa jina lake lijulikane. Nimeyatundika hapa kwa sababu ya uzito wa anachokisema. Tafadhali soma na kama unaweza changia maoni yako tuelimike.
Nimshukuru sana kwa kutumia muda wake kuandika maoni yake na hapa namnukuu:
MAKANISA ya Kikristo yanafunza ya kuwa Yesu Kristo si kama kuwa ni Mwana wa Mungu tu, bali hakika ni Mungu khasa. Baba, Mwana na Roho Mtakatifu ni mmoja. Watatu katika mmoja, na mmoja katika watatu. Wote ni wa milele, wote ni sawa. Yesu ni Mungu, na Mungu ni Yesu. Hiyo ni imani ya Kikristo, ambayo inaaminiwa na karibu Wakristo wote. Hebu tuifunue Biblia tutazame inasema nini katika jambo hili?
Mt Paulo katika barua yake ya kwanza kuwapelekea Wakorintho aliandika:
Naam, na sisi tumeonekana kuwa mashahidi wa uongo wa Mungu; kwa maana tulimshuhudia Mungu ya kuwa alimfufua Kristo, ambaye hakumfufua, ikiwa wafu hawafufuliwi.
1 Wakorintho 15.15
Juu ya kuwa Paulo anaambiwa ya kuwa akiamini kuwa Masihi (yaani Kristo) na Mwenyezi Mungu ni kitu kimoja hapa anasema: “Tulimshuhudia Mungu ya kuwa alimfufua Kristo.” Ikiwa Mungu kamfufua Kristo, hawawezi kuwa wote wawili hao ni mtu mmoja. Mmoja alikuwa ni mtenda, mfufuaji, na wa pili alikuwa ni mtendwa, mfufuliwa. Kama Kristo ni Mungu mwenye uwezo wa kufufua basi maelekeo ni kusema: “Kristo kajifufua”, sio kafufuliwa. Mwenye kufufuliwa ni mfu asiyejiweza kitu.
Katika kitabu cha Matendo ya Mitume inasimuliwa kuwa Mt Stefano alisema aliyoyaona yaliyo mbinguni. Alisema:
Tazama! naona mbingu zimefunguka, na Mwana wa Adamu amesimama mkono wa kuume wa Mungu.
Matendo 7.56
Mwana wa Adamu ndiye Yesu, na kwa jina hilo ndio mwenyewe akipenda kujiita, sio Mwana wa Mungu. Hapo basi huko mbinguni Stefano anasema anamwona Yesu kakaa mkono wa kulia wa Mungu. Mwenye kukaa mkono wa kulia wa fulani hawezi kuwa ndiye yule yule fulani. Hayo ni maelezo ya mbinguni. Ni wazi basi kwa ushahidi wa Biblia kuwa Yesu hakuwa Mungu mbinguni kama alivyokuwa si Mungu duniani.
Yesu alipokimbilia kwenye Mlima wa Zaituni na huku akisakwa na Mayahudi alijitenga na wanafunzi wake. Huko faraghani aliomba hivi:
Ee Baba, ikiwa ni mapenzi yako, uniondolee kikombe hiki; walakini si mapenzi yangu, bali yako yatendeke. Malaika kutoka mbinguni akamtokea akamtia nguvu.
Luka 22.42-43
Hapa tunaona mambo matatu muhimu:
Yesu anamwomba Mungu. Yesu anamwabudu Mungu. Wawili hao ni mbali mbali, na vyeo vyao ni mbali mbali. Yesu ni mtumwa mnyonge mwenye kuomba na kuabudu. Na Mungu ni Mwenyezi Mungu mwenye uwezo wote na mwenye kustahiki kuabudiwa pekee, hata na Yesu, mwenye kutakiwa msaada pekee, hata na Yesu.
Mapenzi ya Mungu ni mbali na yale ya Yesu. Yesu hataki kuuliwa, ananyenyekea na kuomba kwa Bwana wake: “uniondolee kikombe hiki” cha mauti. Yesu hana azma hata chembe ya kufa msalabani, kifo cha mhalifu, kifo cha laana kama maadui zake Mayahudi walivyoazimia kumpatilisha nacho. Lakini anakiri kuwa ni mapenzi ya Mungu sio yake yeye yatendeke. Yeye hana hila wala nguvu za kuzuia kudra ya Mwenyezi Mungu.
Yesu, Mwana wa Adamu, anakata tamaa. Imani inampunguka. Kavunjika moyo. Ikabidi “Malaika kutoka mbinguni akamtokea akamtia nguvu.”
Jee, yaelekea kuwa Yesu ndiye Mungu? Yaelekea kuwa yeye na Mungu kuwa ni sawa? Kama upo wasiwasi wo wote wa kujibu hayo, mwenyewe Yesu anajibu kama anavyo hadithiwa na Yohana kuwa kasema:
Baba ni mkuu kuliko mimi.
Yohana 14.28
Na mwishoni naye yupo msalabani:
Na kama saa tisa, Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu akisema, Eloi, Eloi, lama sabakthani? yaani, Mungu wangu, Mungu wangu, Mbona umeniacha?
Mathayo 27.46
Yafaa hapa tujiulize: Yesu akimlilia Mungu gani hapo msalabani ikiwa naye mwenyewe ni Mungu? Au nini alikusudia aliposema: “Mungu wangu naye ni Mungu wenu”? Maneno hayo kama yanaonyesha cho chote basi yanaonyesha unyenyekevu wa Yesu mbele ya Mungu wake. La kustaajabisha ni kule kukata tamaa kwake na kuvunjika moyo. Huwaje mtu wa imani, licha ya nabii na mwana pekee wa Mungu, akate tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu. Ama kuwa Mungu akate tamaa na Mungu, na kumyayatikia: “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha”, ni jambo ambalo halimkiniki kuwa.
Kwa uthibitisho ulio wazi Biblia inatwambia kuwa Yesu si Mungu, wala Mungu si Yesu.”
Mwisho kunukuu.
Kusoma original na kuendelea na hii discussion nenda 👉Bwaya blog
See lessPromo – MeridianBet
Kubet kumerahisishwa
Jipatie Tsh 3,500 ya kuanzia kama zawadi ya kujiunga.
Jiunge SasaNi halali mwanamke kuhubiri au kuwa mchungaji?
Emmanuel Magessa
Mistari muhimu ya kukumbuka:- 1 WAKORINTHO 14:34-36:- 34 Wanawake na wanyamaze katika kanisa, maana hawana ruhusa kunena bali watii, kama vile inenavyo torati nayo. 35 Nao wakitaka kujifunza neno lo lote, na wawaulize waume zao wenyewe nyumbani mwao; maana ni aibu wanawake kunena katika kanisa. 36 ASoma Zaidi
Mistari muhimu ya kukumbuka:-
1 WAKORINTHO 14:34-36:-
34 Wanawake na wanyamaze katika kanisa, maana hawana ruhusa kunena bali watii, kama vile inenavyo torati nayo.
35 Nao wakitaka kujifunza neno lo lote, na wawaulize waume zao wenyewe nyumbani mwao; maana ni aibu wanawake kunena katika kanisa.
36 Au je! Neno la Mungu lilitoka kwenu? Au kuwafikia ninyi peke yenu?
1 TIMOTHEO 2:11-12:-
11 Mwanamke na ajifunze katika utulivu, akitii kwa kila namna.
12 Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha, wala kumtawala mwanamume, bali awe katika utulivu.
HII NI MADA YENYE UBISHI MKUBWA miongoni mwa vichwa vya watu wengi . Na maandiko hayo kwa kueleweka isivyo sahihi hutumiwa na baadhi ya watu wengi kujaribu kujenga hoja zao za kupinga kwamba mwanamke hana haki yoyote ya kuwa Mchungaji wala kusimama madhabahuni kuwahubiria watu kanisani.
Jambo hili limeleta mzozano mkubwa na mpasuko ndani ya makanisa mengi ya Mungu, kuhusu uhalali wa mwanamke kuhubiri madhabahuni na kuwa Mchungaji. Kuna mawazo ya positive na Negative, kuna wengine wanaona ni sahihi na kuna wengine kwao siyo sahihi kabisa .
Sasa basi ukweli na usahihi wa maandiko hayo ni upi basi? Je, ni sahihi kwamba mwanamke hatakiwi kuhubiri madhabahuni kanisani au kuwa Mchungaji ? Tatizo ni kwamba Maandiko hayo hayaeleweki vizuri kwa kwa wakristo wengi na hata baadhi ya wachungaji na Maaskofu, wanalifafanua hilo Andiko kwa maana potofu kabisa .
NB:-
Kuitwa Mtume, Nabii Askofu au Mchungaji n.k. Siyo kigezo kikubwa cha kwamba wewe unaielewa sana Biblia kwa usahihi wake. La asha ! Ndiomaana wako hata wachungaji wengine tena wengi tu ambao huyatafsiri maandiko isivyo na kuyapotosha kwa tamaa zao wenyewe.
MWALIMU MKUU WA BIBLIA NI ROHO MTAKATIFU; yeye ndiye aliyeyaleta maandiko hayo kwetu. Na hatuwezi sisi kuamua kuyatafsiri maandiko hayo vyovyote tu kama apendavyo mtu fulani kutafsiri. La Asha
[ 2 PETRO 1:19-20 ] .
Bali katika kanuni za kuyatafsiri maandiko, tunahitaji sana maongozi ya msaada wa Roho Mtakatifu mwenyewe katika kuyasoma na kuyaelewa maandiko vizuri na kuyatafsiri kwa usahihi wake. Neno la Biblia. Tunaweza kulifaham kwa kufunuliwa na Roho Mtakatifu pekee yake. Ndiomaana Yesu alisema uliwaficha wenye hekima na Akili (Wasomi), ukawafunulia watoto wachanga (Watu wasio na elimu) . Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyokupendeza mbele zako [ MATHAYO 11:25-26]. “Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho Mtakatifu . Maana Roho huchunguza yote hata mafumbo ya Mungu. Lakini sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu makusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu ” .
[1 WAKORINTHO 2:10-15].
Si hilo tu. Nikodemo alikuwa ni mwalimu mkuu wa chuo cha Torati. Na watu walimwamini sana katika Taifa la Israeli. Lakini Nikodemo alipoambiwa na Yesu maneno mepesi tu ya Mungu , na usomi wake wote, alishindwa kuyaelewa maana yake nini !! Sasa Yesu ambaye hakupita chuo chochote cha Theolojia, ikambidi amfundishe Nikodemo, mwalimu mkuu wa chuo cha Theolojia ya Torati.
[ YOHANA 3:1- 10 ]
Sisemi wala kupinga kwamba kusoma chuo cha Biblia ni kosa au ni vibaya, au ni dhambi. Hapana. Ni nini maana ya kuanza kukwambia hayo. Maana yangu ni hii kwamba :- Ondoa dhana potofu ukafikili kila mtu anayeitwa Mchungaji, Askofu au Mwanatheolojia fulani msomi anaielewa sana Biblia ki-maana. Ukiwa na mawazo hayo tu, utapotezwa na kudanganyika sana Mpendwa . Na Mungu huwa hatendi kazi kwa misingi hiyo. Mchungaji /Ev/ Mwanatheolojia huyo Anaweza kuielewa Biblia kwa namna fulani tu ya akili hivi , lakini asiweze kabisa kuielewa Biblia kwa jinsi ya rohoni zaidi kwa ufunuo wa Roho Mtakatifu . Na maana ya kweli ya maneno ya Biblia hutumbalikana kwa jinsi ya rohoni zaidi na sio kwa jinsi ya mwilini.
[ WAGALATIA 1:11-12 ; WAEFESO 1:17-19].
Hivyo ni vema zaidi tusiweke vipimo vyetu vya usomi kama kigezo cha kuitafsiri Biblia; bali tumuhitaji sana Roho wa Mungu ndio atuongoze katika kulitafsiri Neno lake Mungu.
See lessPromo – MeridianBet
Kubet kumerahisishwa
Jipatie Tsh 3,500 ya kuanzia kama zawadi ya kujiunga.
Jiunge SasaKunywa pombe na kulewa ni dhambi?
Emmanuel Magessa
KUNYWA TU POMBE NA KULEWA POMBE VYOTE NI DHAMBI MBELE ZA MUNGU. Kama ni wanafunzi wazuri wa Biblia. Tutafaham kwamba NENO LA MUNGU katika maandiko limetupiga marufuku sio kwamba tusilewe pombe bali hata tusiiguse kabisa pombe vinywani mwetu. Yaani TUSIINYWE KABISA. Biblia inasema katika maandiko yaSoma Zaidi
KUNYWA TU POMBE NA KULEWA POMBE VYOTE NI DHAMBI MBELE ZA MUNGU.
Kama ni wanafunzi wazuri wa Biblia. Tutafaham kwamba NENO LA MUNGU katika maandiko limetupiga marufuku sio kwamba tusilewe pombe bali hata tusiiguse kabisa pombe vinywani mwetu. Yaani TUSIINYWE KABISA.
Biblia inasema katika maandiko ya fuatayo:-
MITHALI 23:19-20:-” Sikia mwanangu, uwe na hekima, Nakuongoza moyo wako katika njia njema. USIWE MIONGONI MWAO WANYAO MVINYO (pombe); miongoni mwao walao nyama kwa pupa”.
KUMBUKUMBU 29:5-6:” Nami miaka arobaini nimewaongoza jangwani asema BWANA; nguo zenu hazikuchakaa juu yenu, wala kiatu chako hakikuchakaa katika mguu wako. Hamkula mkate, WALA HAMKUNYWA DIVAI, WALA KILEO (pombe); ili mpate kujua kwamba, Mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.”
ISAYA 5:11-12, 22, 24:- ” OLE WAO wamkao asubuhi na mapema wapate kufuata kileo: wakishinda sana hata usiku wa manene mpaka Mvinyo imewaka kama moto ndani yao! Na kinubi, na zeze, na matari, na filimbi na mvinyo, zote zi katika karamu zao; lakini hawaingalii Nazi ya BWANA wala kuyafikiri matendo ya mikono yake. OLE WAO walio hodari KUNYWA KILEO CHENYE NGUVU, watu waume wenye nguvu kuchanga vileo (pombe). Ole wao. Kwahiyo kama vile mwali wa moto uteketazao mabua makavu, na manyasi makavu yaangukavyo KATIKA MWALI WA MOTO ; kadhalika shina lao ( hao wanywao pombe) litakuwa kama ubovu, na ua lao litapeperushwa juu kama mavumbi; kwa sababu wameikataa sheria ya BWANA wa majeshi, na kulidharau neno lake yeye aliye Mtakatifu wa Israeli”.
Mstari huo unaeleza waziwazi kabisa kwamba watu wale wote wanaokunywa pombe (vileo) . Kwa kufanya hivyo wamemdharau Mungu aliye Mtakatifu. Na pia mwisho wao hao walevi wanaokunywa pombe ni kutupwa jehanamu ya moto.
MATHAYO 24:48-51:-” Lakini mtumwa yule mbaya akisema moyoni mwake, Bwana wangu anakawia; akaanza kuwapiga wajoli wake, na kula NA KUNYWA PAMOJA NA WALEVI; bwana wake mtumwa Huyo atakuja Siku asiyodhani, na saa asiyoijua, ATAMKATA VIPANDE VIWILI (Huyo mnywa pombe), na kumweka fungu lake pamoja na wanafiki; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno”.
ISAYA 24:9:-” Hawatakunywa divai pamoja na nyimbo; KILEO KITAKUWA UCHUNGU KWAO WAKINYWAO, asema Bwana”.
HESABU 6:1-3:-” Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia, Nena na watu wa Israel, uwaambie, mtume mume au mtu mke atakapoweka Nadhiri kubwa, nadhiri ya mnadhari, ili ajiweke wakfu kwa BWANA; ATAJITENGA NA DIVAI NA VILEO ; HATAKUNYWA SIKI YA DIVAI, WALA SIKI YA KILEO(Pombe)……”
WAAMUZI 13:4, 13-14:-“Basi sasa, Jihadhari nakuomba, USINYWE DIVAI WALA KILEO (POMBE), wala usile kitu kilicho najisi. Malaika wa Mungu akamwambia Manoa, katika hayo yote niliyomwambia huyo mwanamke na ajihadhari……….WALA ASINYWE DIVAI , WALA MVINYO, wala asile kitu chochote kilicho najisi; hayo niliyomwamuru na ayatunze.”
LUKA 1:13, 15:-” Lakini yule malaika akamwambia usiogope, Zakaria, maana dual yako imesikiwa, na mkeo Elizabeth atakuzalia mtoto mwanamume, na jina lake utamwita Yohana. Kwa sababu atakuwa mkuu mbele za Bwana; HATAKUNYWA DIVAI WALA KILEO (POMBE); naye atajwa Roho Mtakatifu hata tangu tumboni mwa mamaye.”
WAEFESO 5:18:-” Tena MSILEWE KWA MVINYO, ambamo mna ufisadi; Bali mjazwe Roho”.
Unaweza kuona mpaka hapo. Neno la Mungu Biblia imetuonya kabisa na kutupiga marufuku sio kulewa tu kwa kutumia pombe kupita kiasi ndio dhambi. Hapana. Bali hata kunywa tu mdomoni ni dhambi vilevlile iwe kwa mantiki ya kulewa au pasipo kulewa kabisa. Bado ni dhambi na machukizo mbele za Mungu. Utakwenda jehanamu ya moto.
See lessPromo – MeridianBet
Kubet kumerahisishwa
Jipatie Tsh 3,500 ya kuanzia kama zawadi ya kujiunga.
Jiunge SasaDivai/mvinyo ni nini?
Emmanuel Magessa
UFAFANUZI KUHUSU NENO MVINYO, DIVAI NA KILEO KATIKA BIBLIA. Neno Divai, Mvinyo au kileo ( WINE) limetajwa katika Biblia nzima zaidi ya mara 234. Katika Biblia yetu ya kiswahili hatuwezi kukuta neno hili “Pombe“. Lakini badala yake maneno yanayotumika kuizungumzia pombe katika Biblia yanasimama kamaSoma Zaidi
UFAFANUZI KUHUSU NENO MVINYO, DIVAI NA KILEO KATIKA BIBLIA.
Neno Divai, Mvinyo au kileo ( WINE) limetajwa katika Biblia nzima zaidi ya mara 234.
Katika Biblia yetu ya kiswahili hatuwezi kukuta neno hili “Pombe“. Lakini badala yake maneno yanayotumika kuizungumzia pombe katika Biblia yanasimama kama Mvinyo, Divai au kileo kwa eneo la upande mmoja.
NB:-
Ijapokuwa kwa upande wa pili vile vile. SIO KILA NENO MVINYO au DIVAI linapotumika katika mistari ya Biblia linamainisha pombe kama pombe. Hapana.
Kuna mahali pengine katika maandiko ya Biblia limetafsiriwa neno MVINYO/DIVAI lakini haina maana ya pombe kama pombe kwa namna ile inavyofahamika kwa wengi . Lakini ukirudi katika LUGHA YA ASILI YA BIBLIA ya kiebrania na kiyunani, neno lilotumika hapo halimainisha pombe kama pombe hasa ( Alcoholic drink). Ingawa kwa kiswahili wametafsiri mvinjo au Divai.
Kuna maneno zaidi ya 11 tofauti ya kiebrania yanayotumika kuelezea kinywaji kinachotokana na zabibu. Sasa ingawa katika Biblia ya kiswahili au kingereza limetumika neno moja tu MVINYO au WINE.
Nimesema sio kila neno mvinjo au Divai linapotumika katika Biblia linamainisha pombe moja kwa moja . La hasha!
NENO MVINYO/ DIVAI au WINE linapotafsiriwa katika Biblia. Limetokana na neno la kiebrania “YAYIN” na kiyunani “OINOS“. Ambapo haya ni maneno ya jumla yanayotumika kuilezea ile divai iliyochachuka tayari ( Pombe) na ile Divai ambayo bado kabisa haijachachuka (fesh grabe juice).
Kwa hiyo SIO KILA NENO mvinyo/Divai linapotumika katika mistari ya Biblia inamainisha pombe. Mahali pengine inaweza ikamainisha mvinjo pombe na mahali pengine mvinyo isiwe na maana ya pombe.
KWA MFANO.
Katika MWANZO 27:28, 37, Biblia inasema :- ” Mungu na akupe umande wa mbinguni, Na ya manono ya nchi, na wingi wanafaka na MVINYO. Isaka akajibu, akamwambia Esau, Tazama, nimemfanya awe bwana wako, na ndugu zake wote nimempa kuwa watumishi wake ; kwa nafaka na MVINYO nimemtegemeza……”
Sasa kwa haraka haraka unaweza kufikiri mvinyo uliotamkwa hapo ni Pombe. Jambo ambalo siyo kweli.
Neno mvinyo lilotafsiriwa hapo limetokana na neno la kiebrania ambalo ni ” TYROSH”. Na neno hilo maana yake ni “FRESH GRAPE JUICE”. Ni juice fresh tu ya zabibu iliyotumika hapo na siyo pombe.
Sijui unaweza kunielewa mpaka hapo!!
Mfano mwingine.
MITHALI 3:10:-” Ndipo ghala zako zitakapojazwa kwa wingi; na mashinikizo yako yatafurika DIVAI MPYA”.
MIKA 6::15:-” Utapanda lakini hutavuna; utazikanyaga zeituni, lakini hutajipaka Mafuta; na hizo zabibu, lakini HUTAKUNYWA DIVAI“.
ISAYA 65:8:-” BWANA asema hivi, kama vile DIVAI MPYA ipatikanayo katika kichala, na mtu mmoja husema, usikiharibu kwa maana mna baraka ndani yake; ndivyo nitakavyotenda kwa ajili ya watumishi wangu, ili nisiwaharibu wote”.
Neno DIVAI iliyotajwa hapo kiebrania ni “TYROSH”. Ambalo maana yake ni kinywaji cha juice fresh ya zabibu.
Ambapo Mungu mwenyewe amesema hapo kinywaji cha namna hiyo, kinakuwa kina baraka ndani yake. Mungu anakikubali tukitumie .
Hata katika ushirika wa meza ya BWANA, ni makosa kutumia pombe (wine). Bali inapaswa itumike tu juice fresh ya zabibu ambayo haina Alcoholic. Na ndiyo Divai ya namna hii iliyotumika katika MATHAYO 26:26-29.
MFANO MWINGINE
Biblia inasema MWANZO 9:20-24:-” Nuhu akaanza kuwa mkulima , akapanda mizabibu: AKANYWA DIVAI , akalewa , akawa uchi katika hema yake. Hamu baba wa kanaani, akauona uchi wa baba yake, akawaeleza ndugu zake wawili waliokuwa nje”.
MITHALI 23:30-32:” Ni wale wakaao sana kwenye MVINYO: waendao kutafuta DIVAI Iliyochanganyika. USIITAZAME MVINYO iwapo ni nyekundu; Itiapo bilauri rangi yake, ishukapo taratibu; mwisho wake huuma kama nyoka: huchoma kama fira”
Sasa neno DIVAI au MVIYO uliotumika katika mistari hiyo . Linatokana na neno la kiebrania ” YAYIN” iliyokwisha kuchachuka na kufikia hatua ya kuwa nyekundu. Ambapo kiufupi imekuwa ni Pombe tayari. Sasa
Na ikishakuwa Pombe , Biblia imepiga marufuku hapo ikisema USIITAZAME . Maana yake usijaribu kuigusa wala kuinywa huo mvinyo/Divai.
Unaweza kuona mpaka hapo.
Nilichotaka uelewe hapo mpendwa msomaji wangu ni kwamba neno hili DIVAI/ MVINYO (WINE) linapotumika katika Biblia, siyo kila eneo katika maandiko linapotumika linamainisha kuwa ni Pombe moja kwa moja . La hasha!!
Kwa ufupi Divai ambayo ni Pombe inaitwa pia ni DIVAI YA JEURI ambayo inatajwa wanaoitumia sio watu wa Mungu bali ni waovu ( MITHALI 4:14-17).
Lakini watakatifu wa Mungu tuliokolewa tunainywa tu ile DIVAI ILIYO NJEMA ambayo inakuwa tu ni juice fresh na siyo pombe. Unaweza kuona mpaka hapo
( YOHANA 2:10-11; ISAYA 65:8 ).
See less