Tofauti ya kibebeo na kifungashio ni ipi?
Jiunge MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Login MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Umesahau password yako?. Andika email yako hapo chini alafu bonyeza 'Reset'. Utapokea link katika email yako kwa ajili ya kutengeneza password mpya.
Tafadhali elezea kwa nini unahisi chapisho hili linapaswa kuripotiwa
Flora Jumanne
Apa lazima tuliangalie ili swala kiuzito kidogo ili tusije kumbwa na balaa la kupigwa faini kwa sababu faini haitaangalia aidha unajua au hujui.
Picha chini inaonesha vifungashio vya korosho. Inamaana vifungashio ni vile ambavyo vinakuja moja kwa moja na bidhaa unayonunua mfano korosho, mkate au maziwa ya pakiti.
Tukija kwenye upande wa vibebeo ndo vile vyote unavyopewa baada ya kununua bidhaa ili kuwezesha ubebaji au kusitiri vyema kile ulichonunua mwanzo mfano unaweza nunua mkate ulio ndani ya kifungashio na ukapewa mfuko wa plastiki kama kibebeo.
Pia kitu cha kukumbuka ni kwamba kifungashio hakiruhusiwi pia kutumiaka kama kibebeo. Mfano umemaliza kutumia mkate na ukautumia ule mfuko kubebea kitu kingine sasa unakuwa kibebeo na sio kifungashio tena.
KUWA MAKINI.