SMS zipi nzuri za vichekesho?
Faustine JohnAdvanced
Jiunge MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Login MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Umesahau password yako?. Andika email yako hapo chini alafu bonyeza 'Reset'. Utapokea link katika email yako kwa ajili ya kutengeneza password mpya.
Tafadhali elezea kwa nini unahisi chapisho hili linapaswa kuripotiwa
Chukua hii.
Askari wameitwa kwenye nyumba ambayo kuna ugomvi. Wakafika halafu ikabidi waripoti kwa simu yale waliyokuta
Askari: mkuu tumekuja hapa tumekuta mama mwenye nyumba amempiga mumewe chuma cha kichwa na kumuumiza sana
Afande: kisa na mkasa hata akafanya hivyo?
Askari: mama alikua anapiga deki, mumewe akaingia na viatu kabla sakafu haijakauka.
Afande: Mmeshamkamata huyo mama??
Askari: hapana bado mkuu
Afande: mnangoja nini sasa??
Askari: tunangoja sakafu ikauke afande
Na hii nyingine
HAYA NDIO MADHARA YA KULALA KANISANI
Tukiwa kanisani mdada alikuwa amelala , akaamka akasikia Pastor anasema
” SIMAMA”
Yule dada akasimama akashangaaa kanisa zima linamtizima kwa mshangao akiwemo mumewe, akaangalia kanisa zima akashtuka kujiona yeye peke yake ndiye aliesimama
Pastor akaendelea vizur endelea kusimama, tumepata mmoja hadi sasa aliyesimama narudia kwa mara ya mwisho kama hujasikia vizuri
” kama wew umewahi kumsaliti au bado unasaliti ndoa yako SIMAMA”
Binti akazimia
😂😂 😂 😂😂