Sifa za mwanamke anayefaa kuolewa ni zipi?
Jiunge MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Login MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Umesahau password yako?. Andika email yako hapo chini alafu bonyeza 'Reset'. Utapokea link katika email yako kwa ajili ya kutengeneza password mpya.
Tafadhali elezea kwa nini unahisi chapisho hili linapaswa kuripotiwa
Jose Mandingo
Katika siku hizi za kisasa za sayansi na teknolijia wanaume wengi wamejikuta katika mkanganyiko mkubwa hasa linapokuja suala la kutafuta mchumba au mwenza wa kumuoa na kuanzisha maisha na familia.
Hizi ni baadhi tu ya sifa za masingi ambazo mwanamke anatakiwa awe nazo kama unataka kuoa. Pia kama mwanakmke unataka kuolewa na kuishi na mume zisome hizi sifa naamini zitakusaidia sana:.
1: Tabia njema. Uzuri wa mwanamke ni tabia mimi naamini hivo ndio maana hata mwanaume atadate na wanawake wazuri ila akitaka kuoa lazima aangalie yupi ana adabu na tabia njema moyoni mwake.
2: Anyeshika dini, kuna wanawake wengi wazuri sana ila hawashiki dini. Tunaamini kuwa anayaeshika dini huwa na heshima kwa mumewe kwa kuwa hata dini inafundisha hivo. Japo si wote wanaoshika dini huwa na heshima ila aghalabu wale waliosalia katika dini huwa na hashima sana kwa waume zao.
3: Heshima na adabu. Hapa hekima inahitajika kujua yupi anaheshima, unakuta mwanamke ni mzuri ila hana hata chembe ya heshima, ni hata mavazi yake si ya heshima, sijui nguo zimechanika chaninka au nguo za kulalia anavaa mchana na za machana usiku.
4: Anaye vaa kwa staha na heshima. Mwanamke avae kwa staha sio anavaa kama mhuni au kahaba fulani hivi. Mwanamke usivae tu kisa fasheni au kwa kuwa fulani kavaa, au ili uoneshe kuwa una kiuno na vitu kama hivyo.
5: Anayependa na kuwaheshimu wazazi. Ni wajibu wa mwanamke kuwapenda wazazi wake na wa upande wa kiume.
6: Awe na mapenzi ya dhati na anayejua kupenda. Wengi wameumia sana kwa kupenda au kupenda kisa mtu ana kitu fulani aidha fedha au mali. Kumbuka furaha na upendo wa kweli hautokani na mali au pesa, mwamke asikupendea kwa kuwa una pesa au wewe ni meneja, ukifilisika lazima uone dunia kama kuzimu vile.
7: Kauli njema na za adabu. Chunguza kauli zake je za kutia moyo au kukatisha tamaa? Yaani awe mtu wa kukutia moyo wewe mwanaume.
8: Mwenye malengo na mtazamo wa kimaendeleo. Siku hizi wanawake wameamka sana na wanapenda kuendeleo, awe mtu mwenye mipango ya mbele ya namna ya kuendesha familia na kufanikiwa, awe anashirikiana nawe katika kutekeleza mipango ya maendeleo.
9: Asiwe mtu wa makundi sana na starehe. Katika vitu vinavyofanya mwanamke akakosa adabu ni makundi. hatukatai kila mtu anazungukwa na watu ila makundi mengine yanabomoa.
10: Asiyependa kuiga. Utasikia “beby nataka simu kama ya Mwajuma ile Iphone 7” au si jui gauni la Angel.
11. Asojivunia uzuri wake. Mwanaume unakutana binti kauli zake tu ni kukutishia eti mimi mzuri sana! Mimi nasemaga hata Cleopatra alikuwa mzuri ila alimtii mumewe, wewe nani hata ujidai na uzuri wako?
12: Anasikiliza na kukutii. Mwanamke bora huwa anakuwa msikilizaji, anahoji vizuri na kwa utulivu.
13: Usafi. Kiufupi wanawake wameumbwa na hulka ya usafi, awe mtu wa kupangilia vitu vizuri anavaa kwa unadhifu kiasi hata ukitembea nae njiani huogopi kumtambulisha.
14: Asiwe mtu wa ugomvi. Tuanaamini kuwa mwanamke aliumbwa mpole na mnyeynyekevu, awe angalau mtu wa kushuka hata ukimkosea, ili kwa kinywa chake asiharibu ndoa na uhusiano.
15: Mchapa kazi. Simaanishi awe ameajiriwa au awe na kazi ila namanisha anayewza kutimiza majukumu yake vizuri na kwa wakati.
16. Mdomo wa heshima. Mwanamke mpenda maneno mengi si vema ukawa nae makini.
Bonyeza hapa kusoma kwa urefu zaidi