Siasa ni nini?
Jiunge MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Login MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Umesahau password yako?. Andika email yako hapo chini alafu bonyeza 'Reset'. Utapokea link katika email yako kwa ajili ya kutengeneza password mpya.
Tafadhali elezea kwa nini unahisi chapisho hili linapaswa kuripotiwa
Hakuna maana moja ya siasa iliyokubaliwa na wasomi wote, kutokana na kutokubaliana huko, nadharia mbalimbali kuhusu maana ya siasa zimeibuka. nitazitaja chache tu.
(1) state centric view(mtizamo unaohusisha siasa na dola)
katika mtazamo huu siasa inaelezwa kua ni: kila kitu kinachofanywa na dola au serikali. wasomi kama Mao Tsetung na Otto Von Bismark wanashikilia msimamo huu.
udhaifu; mtizamo huu umeshindwa kuelezea taasisi nyingine kama vile vyama vya siasa vinaingia kwenye kundi gani kwakua hawavitaji wala kuvihusisha na siasa kwenye maana waliyoitoa.
(2)mtizamo unaohusisha siasa na nguvu za dola
miongoni mwa wasomi wanaofafanua mtizamo huu ni Okwudiba Nnoli na Harold Lasswell
OKWUDIBA NNOLI anaeleza kua siasa ni: mchakato unaohusisha uchukuaji wa madaraka(nguvu) ya dola, utumiaji(utekelezaji) wa madaraka(nguvu) ya dola na ulinzi wa hayo madaraka(nguvu) ya dola.
HAROLD LASSWELL anaeleza siasa kua ni: who gets what, when and how. maana yake inajikita katika mgawanyo wa rasilimali. Ili mgawanyo wa rasilimali utokee ni lazima mgawaji awe na madaraka(nguvu za dola)
(3)mtizamo wa siasa kama maisha ya jumla ya umma
mwanafalsafa Aristotle anaeleza siasa kama: shughuli ya kimaadili inayohusiana na ujengaji wa jamii yenye usawa.
anaendelea kudai kwamba binaadam ni mnyama wa kisiasa anayeishi kwenye jamii ya kisiasa hivyo kila kitu ni siasa.
mimi binafsi naunga mkono mtizamo huu wa Aristotle
hayo ni maoni ya mtumiaji mmoja wa Jamiiforums