Saikolojia ni nini?
Jiunge MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Login MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Umesahau password yako?. Andika email yako hapo chini alafu bonyeza 'Reset'. Utapokea link katika email yako kwa ajili ya kutengeneza password mpya.
Tafadhali elezea kwa nini unahisi chapisho hili linapaswa kuripotiwa
1sky
SAIKOLOJIA ni neno lililotoholewa kutoka neno la kiingereza psychology, si elimu inayoeleweka sana katika jamii yetu. Asili ya ‘psychology’ ni neno ‘psyche’ lenye maana ya nafsi.
Neno kuu linalobeba dhana ya saikolojia ni tabia. Tunapozungumzia tabia, tuna maana ya matendo, miitikio au mienendo inayoweza kuonekana wazi, kupimwa na hata kuchunguzika kwa kufuata misingi ya kisayansi. Kwa maana hiyo, saikolojia ni sayansi ya kuchunguza tabia, mitazamo, imani walizonazo watu na namna inavyoathiri wayatendayo.
Kwa hiyo, tunapozungumzia saikolojia, kimsingi tunazungumzia msingi wa tabia zetu na jinsi tabia hizo zinavyojiumba kwa maana ya namna zinavyoanzia mbali kwenye ufahamu kisha kuhamia kwenye mitazamo ambayo ndiyo huzaa matendo yanayoonekana na ambayo tunayaita tabia.Tabia hii, kama tulivyoona, huchunguzwa kwa kutumia majaribio ya kisayansi na wala sio hisia, maoni au bashiri za kimazoea.
chanzo – Bwaya blog