Jiunge

Jiunge MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection

Unayo account ? Log In

Unayo account ? Log in

Log In

Login MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection

Jiunge Hapa

Umesahau Password?

Hauna Account, Jiunge Hapa

Umesahau Password

Umesahau password yako?. Andika email yako hapo chini alafu bonyeza 'Reset'. Utapokea link katika email yako kwa ajili ya kutengeneza password mpya.

Unayo account ? Log in

Tafadhali andika jina lako kamili.

Tafadhali andika E-Mail yako.

Please choose an appropriate title for the question so it can be answered easily.

Tafadhali elezea kwa nini unahisi chapisho hili linapaswa kuripotiwa

Sign InSign Up

1Sky

1Sky

1Sky Navigation

  • Blog
  • Wasiliana Nasi
  • Advanced Search
  • App

Mobile menu

Close
Uliza Swali
  • Home
  • Maswali
  • Points
  • Miongozo
  • Wasiliana Nasi
  • Advanced Search
  • App
Home» Maswali»Q 29992
In Process
Adv
Poll
Anonymous
Asked: February 18, 20192019-02-18T12:56:18+03:00 2019-02-18T12:56:18+03:00Muziki, Watu Maarufu

Nani mkali kati ya Diamond na Alikiba?

Poll Results

75%Diamond ( 6 )
25%Alikiba ( 2 )
Based On 8 Votes

Nani mkali

Nani mkali kati ya Diamond na Alikiba?
  • 2
  • 2,309
  • 0
  • Share
    • Share on WhatsApp
    • Share on Facebook
    • Share on Twitter
Jibu
  • Report
Adv

Majibu 2

  • Kura
  • Zamani
  • Mpya
  1. Abdallah Hassan
    2020-04-24T18:36:19+03:00Jibu - April 24, 2020 saa 6:36 pm

    KUNA vita ya maneno kati ya makundi mawili ya mashabiki wa muziki wa Bongo Fleva, wanaowashabikia wasanii Alikiba na Nasibu Abdul ‘Diamond’, kila upande ukidai mtu wao ndiyo anajua zaidi kuliko mwingine.

    Ni mjadala mpana katika mitandao ya kijamii, mitaani na hata miongoni mwa wasanii wenyewe ambao kwa kificho au waziwazi, wamewahi kuzungumzia nani mkali katika wawili hao ambao wote ni vijana wenye asili ya Kigoma.

    Alikiba ama King Kiba, ndiye wa kwanza kuingia na kupata jina katika Muziki wa Bongo Fleva, katikati ya miaka ya 2000 akiwa na singo yake ya kwanza, Cinderella ndiyo ilimfungulia milango, kwani alichomoza hadi juu ambako alidumu kwa muda mrefu.

    Huenda Diamond amewahi kuimba kwa kuiga baadhi ya nyimbo za Ali Kiba, kwa sababu yeye alianza kupata jina mwaka 2009, mwaka ambao mwenzake tayari alishakuwa na albamu mtaani.

    Unapotaka kufanya ulinganisho wa wawili hawa, ni lazima uchague unataka kuwalinganisha nini, vinginevyo unaweza kujikuta umewekeza katika chuki au ushabiki, kitu ambacho hakitakiwi. Kwa mfano, ni vigumu kupata idadi kamili ya mashabiki wa wasanii hao, ingawa mapokeo ya kazi zao yanaweza kumuongoza mtu kuelewa.

    Kitu kimoja cha msingi ambacho wengi wanakubaliana ni kwamba Alikiba ana uwezo mkubwa wa kuimba na mwenye sauti nzuri kuliko Diamond. Msanii mmoja chipukizi, Ibrahim Kidugu ‘Wizzy Rapper’ katika kibao chake cha Kote Nisikike, kwenye mojawapo ya vesi anasema “Ali ni mwanamuziki, Nasibu Mfanyabiashara.”

    Maana ya Wizzy Rapper ni kuwa Diamond anafanya biashara ya muziki, ndiyo maana anaonekana kuwa juu ya Alikiba ambaye anafanya muziki kwa mazoea.

    Katika ubora wake, Alikiba aliwahi kukutana na mkali wa R&B duniani, R Kelly, katika projekti iliyoitwa One8, ambapo wakali nane wa Afrika walifanya ngoma moja iliyoitwa Hands Across Africa ambao walikuwa ni yeye, Fally Ipupa, 2Face, Amani, Movaizhaleine, 4X4, Navio na JK.

    Licha ya Kiba kufika nyumbani kwa R Kelly, studio kwake, alishindwa kutumia ushawishi wa msanii huyo mkubwa ili aweze kumsaidia kuingia katika soko la Marekani. Mbaya zaidi, alishindwa pia kujitangaza kimataifa kupitia Fally Ipupa na 2Face ambao ni maarufu kuliko yeye.

    Ambwene Yessaya alimkutanisha Diamond na Davido wa Nigeria na akafanya naye Ngoma ya Number One Remix. Hapa kijana yule wa Tandale hakutaka kuishia kwa msanii huyo pekee, akaingia nchini humo na kufanya kazi na wasanii karibu wote wakubwa, wakiwemo waliofanikiwa zaidi, P Square.

    Hiyo imempa Diamond kujulikana zaidi na kumfanya kuwa mmoja wa wasanii wakubwa Afrika, kiasi cha wengi kuhitaji kolabo naye kutoka Afrika Kusini, Zimbabwe, Ivory Coast na kwingineko Afrika.

    Alikiba haonekani kuwekeza akili yake yote katika muziki anaoufanya. Ni kama mtu ambaye anafanya muziki kwa kujifurahisha na siyo kufikia malengo ambayo mashabiki wake wangependa aende. Ana uwezo mkubwa nyuma ya Mic, lakini ameshindwa kuutumia ili kuliteka soko.

    Kiba anaridhika au labda niseme, mvivu. Katika uhalisia, ni makosa kumshindanisha na Diamond kwa sababu haonyeshi kama ni mshindani wake. Alipokuwa katika ziara yake Ulaya, akaitumia nafasi adimu aliyoipata kukutana na marehemu Papa Wemba na kufanya naye wimbo.

    Baada ya kuliweza soko la Afrika, Diamond anaonekana wazi kulitamani la Ulaya na Marekani na hii ndiyo sababu ya yeye kuwa msanii anayelipwa zaidi kuliko wote kwa sasa hapa Bongo.

    Kiba hatafuti kolabo na watu wa nje kwa vile anadhani ataonekana anamuiga mwenzake, wakati katika maisha, kuiga vitu vizuri na vya maendeleo ni jambo la kupongezwa. Hata hivyo, Kiba anayo nafasi ya kubadilika ili aweze kuwa mshindani wa kweli wa Diamond, vinginevyo asahau!

    imetoka Jamiiforums

    • 1
    • Reply
    • Share
      Share
      • Share on WhatsApp
      • Share on Facebook
      • Share on Twitter
      • Report
  2. Promo – MeridianBet

    Kubet kumerahisishwa

    Jipatie Tsh 3,500 ya kuanzia kama zawadi ya kujiunga.

    Jiunge Sasa
  3. Faustine John

    Faustine John

    • Dar es Salaam, Tanzania
    • 16 Questions
    • 75 Answers
    • 0 Best Answers
    • 248 Points
    View Profile
    Faustine John Advanced
    2019-04-27T08:02:33+03:00Jibu - April 27, 2019 saa 8:02 am

    Mkali zaidi ni Diamond. Ndicho mwandishi wa Swahilihub alichojaribu kutuambia katika andiko lake, aliandika hivi.

    HAPA suala sio Diamond kumpa mkona Ali Kiba tena pale msibani kwa Agnes Gerald, kisha Ali Kiba akaupokea kwa staili ya aina yake.

    Suala hapa ni ushindani wa nani mkali kati ya Diamond Platnumz na Ali Kiba ambao umekuwepo nchini Tanzania kwa muda mrefu.

    Mtandao wa Googletrends unaamua ubishi katika suala la ufuatiliwaji kwenye mitandao.

    Mtandao huo unaonyesha katika kipindi cha mwaka mmoja, Diamond amempiku Alikiba kwa ufuatiliwaji na watu kwa kila tukio analolifanya.

    Hata hivyo, kwa mara ya kwanza ndani ya kipindi cha miaka mitano Ali Kiba alimpiku Diamond Aprili 19, kwa ufuatiliwaji nchini ambayo ilikuwa siku ya harusi yake. Katika siku hiyo Ali Kiba alifikia ufuatiliwaji kwa asilimia 90 huku mpinzani wake Diamond akiwa katika asilimia 75.

    Siku iliyofuata ambayo ni Aprili 20, Alikiba alishuka mpaka asilimia 34 na Diamond alipanda kufikia asilimia 57. Aprili 17, 2018 Diamond alikuwa na asilimia 57 na kilichosababisha akafuatiliwa ilikuwa ni tukio la kukamatwa na polisi kwa kosa la kusambaza picha za chumbani, alifuatiliwa na idadi kubwa ya watu waliotaka kujua undani tukio hilo.

    Tukio la kukamatwa kwa Diamond Platnumz, lilifuatiliwa zaidi na nchi za Canada, Uswidi, Ufaransa, India, Uingereza, Australia na Afrika Kusini. Kwa upande wa Ali Kiba alifuatiliwa kwa asilimia 19 na mashabiki wake baada ya kutuma video fupi katika Mtandao wa Instagram, akionekana akizungumza lafudhi ya Kijaluo na wengi kujiuliza je, ataoa upande wa Kenya kutokana na tetesi ambazo zilikuwepo kwa wakati huo. Ali Kiba alifuatiliwa zaidi Oman pamoja na Saudi Arabia.

    • 0
    • Reply
    • Share
      Share
      • Share on WhatsApp
      • Share on Facebook
      • Share on Twitter
      • Report
Jibu swali hili

Jibu swali hili
Cancel reply

Chagua
Captcha Click on image to update the captcha.

Adv

Sidebar

Uliza Swali

Promo

  • Usihangaike tena, Tumekuwekea Kampuni zote za kubet katika app moja! Jaribu Sasa

  • Beti kwa mara ya kwanza, ukishindwa unarudishiwa hela yako

  • Tafuta Ajira kiurahisi. Jaribu Sasa

  • Jifunze jinsi ya kubet kibingwa

  • Maswali yanayoendana

    • DJ Mwanga ndio nani?

    • BekaBoy ni nani?

    • Messi anacheza timu gani?

    • Samatta analipwa kiasi gani Aston Villa?

    • Samatta anavaa jezi namba ngapi Aston Villa?

    • AY anatokea mkoa gani?

    Explore

    • Home
    • Maswali
    • Polls
    • Points
    • Watumiaji
    • Miongozo
    • App

    MojaSky | Designed by ChuiTec.

    Insert/edit link

    Enter the destination URL

    Or link to existing content

      No search term specified. Showing recent items. Search or use up and down arrow keys to select an item.