Hekima ni nini?
Jiunge MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Login MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Umesahau password yako?. Andika email yako hapo chini alafu bonyeza 'Reset'. Utapokea link katika email yako kwa ajili ya kutengeneza password mpya.
Tafadhali elezea kwa nini unahisi chapisho hili linapaswa kuripotiwa
Emmanuel Magessa
Kila kitu duniani unachokiona ni matokeo ya hekima; inaweza kuwa ni hekima ya Mungu au hekima ya dunia hii. Lakini hakuna chochote duniani ambacho hufanyika nje ya hekima yo yote ile.
Hata ulimwengu huu unaouona uliumbwa na Mungu kwa hekima (Zaburi 104:24), na Mungu akajaza vitu vyote ndani yake na kuviweka katika mpangilio na utaratibu kwa hekima yake. Ubunifu, uvumbuzi, na kazi zote za ustadi unazoziona ni mazao ya hekima ambayo Mungu ameweka ndani ya watu. Kwa hiyo kila ukionacho ni hekima fulani iliyofunuliwa hata vitu kutokea.
Hakuna jinsi ambayo wewe unaweza kuwa bora zaidi katika maisha yako kama huna hekima ndani yako; na hapa nazungumzia zaidi hekima ya Mungu ambayo ndiyo msingi wangu wa kufundisha somo hili.
Kusudi la somo hili ni kukuwezesha wewe mwamini kuwa na maisha yenye matokeo yatokanayo na hekima uliyonayo ndani yako iwapo tu utajua kuwa una hekima na ukaitafuta na kisha kuitumia hekima hiyo kukabiliana na changamoto katika maisha yako.
Sasa, basi, hekima ni nini?
Hekima ni uwezo wa ndani (wa kufikiri na kutenda kwa kutumia ufahamu, uzoefu na maarifa) unaoambatana na roho (chanzo kisichoonekana) nyuma yake uletao matokeo hitajika au yaliyokusudiwa; roho hiyo inaweza kuwa ni Roho wa Mungu au ni roho ya Shetani. Ujuzi huu ni uwezo wa kutumia maarifa na ufahamu alionao mtu ili kuleta matokeo hitajika yaliyokusudiwa.
Jambo la kwanza hapa ambalo nataka wewe ulione ni uwezo wa ndani; hekima inaonekana katika utendaji pale unapokuwa na ujuzi wa jambo fulani na ujuzi huo ukiwa na nguvu nyuma yake inayopelekea kuwepo na matokeo, na nguvu hiyo ni roho; inaweza kuwa ya Mungu au ya Shetani.
Mwanzo 41:39
Farao akamwambia Yusufu, Kwa kuwa Mungu amekufahamisha hayo yote, hapana mwenye akili na hekima kama wewe.
Jambo la pili katika maana hii ya hekima ambayo nataka wewe ulielewe ni roho hii inayoambatana na huo ujuzi au uwezo; hapa ndipo kunakopelekea kuwepo na aina mbili za hekima; hekima ya Mungu na hekima ya dunia. Hekima ya Mungu inatokana na Roho wa Mungu, na hekima ya dunia inatokana na roho ya dunia hii. Kwa hiyo, unapoona unayo hekima ni muhimu sana ukaangalia ni roho ya namna gani iliyoko ndani yako.
Luka 9:53-56
[53] Lakini wenyeji hawakumkaribisha kwa vile alivyouelekeza uso wake kwenda Yerusalemu.
[53] Wanafunzi wake Yakobo na Yohana walipoona hayo, walisema, Bwana, wataka tuagize moto ushuke kutoka mbinguni, uwaangamize; [kama Eliya naye alivyofanya]?
[54] Akawageukia, akawakanya. [Akasema, Hamjui ni roho ya namna gani mliyonayo].
[55] Kwa maana Mwana wa Adamu hakuja kuziangamiza roho za watu, bali kuziokoa. Wakaondoka wakaenda mpaka kijiji kingine.
Kushusha moto kutoka mbinguni ni hekima ya hali ya juu, lazima uwe na ujuzi juu ya jambo fulani ndani yako na uwezo unaokuwezesha kuutumia ujuzi huo ili kuleta matokeo, na roho ndani yako itakayopelekea moto huo kushuka kutoka mbinguni (yaani juu).
Katika habari hii ya Yesu na wanafunzi wake, wanafunzi baada ya kuona Yesu amekataliwa na wanakijiji, waliingiwa na hasira, wakamwambia Yesu kuwa wanataka kushusha moto kutoka juu ili uwateketeze watu hao. Yesu moja kwa moja aliiona ile roho iliyokuwa nyuma yao ambayo ilishikamana na ujuzi waaliokuwa nao, akaona kuwa haikuwa ni Roho ya Mungu bali ni roho ya ulimwengu huu; kwa sababu Roho ya Mungu haipo ili kuangamiza bali kuokoa ila roho itawalayo ulimwengu huu yenyewe ipo kwa ajili ya kuangamiza. Na kwa sababu hiyo, hekima ya Mungu haipo ili kujijenga yenyewe kwa kuwaangamiza wengine, ipo kwa ajili ya kujijenga na kuwajenga wengine kwa kuwaokoa kutoka katika hatari. Kwa hiyo akawakanya; na kama asingeliwakanya, wangelishusha moto kweli.
Ayubu 38:35, 36
[35] Waweza kutuma umeme, nao ukaenda,
Ukakuambia, Sisi tupo hapa?
[36] Je! Ni nani aliyetia hekima moyoni?
Au ni nani aliyetia ufahamu rohoni?
Hekima yo yote ni matokeo ya ujuzi unaoambatana na roho nyuma yake; bila roho nyuma yake ni ngumu sana kuwepo na matokeo hitajika. Unaweza kwa hekima kuagiza cho chote au kufanya cho chote na kikakupa matokeo uyatakayo. Na ujuzi huo ni ufahamu, maarifa na busara.
Unaweza ukawa na ufahamu na maarifa lakini usiwe na hekima lakini haiwezekani kuwa na hekima bila ya kuwa na ufahamu na maarifa. Kwa sababu hekima inathibitika mahali ambapo kuna ufahamu na maarifa na busara, na vyote hivi ni sehemu ya hekima mahali penye hekima.
Kutoka 31:3
Nami nimemjaza roho ya Mungu, katika hekima, na maarifa, na ujuzi, na mambo ya kazi ya kila aina.
Kwa hiyo, hata Mungu ili ampe mtu hekima ni lazima amjaze Roho yake katika hekima kwa sababu hekima ina matunda pale tu inapoambatana na roho ndani yake au nyuma yake. Unapokuwa na ufahamu na maarifa, yanaweza kuwa na maana pale tu unapokuwa na hekima ambayo ni uwezo wa kutumia hivyo (ufahamu na maarifa) kuleta matokeo hitajika. Kwa hiyo hekima inahusisha ujuzi, maarifa,ufahamu na busara. Na kama inahusisha vitu hivi maana yake matumizi ya akili yako ni muhimu sana katika kujipatia hekima na kuitumia yakiwezeshwa na nguvu ya roho iliyopo ndani yako na nyuma ya hekima husika.