HAKIKISHA: Usifanye chochote kabla hujamaliza kusoma maelezo hayo hapo chini ili kutatua tatizo la audio driver.

HATUA YA KWANZA;
Bonyeza start na angalia sehemu ya power icon,shikilia batani ya shift kisha right kwenye power icon na bonyeza restart wakati bado umeshikilia batani ya shift. Angalia picha hapo chini.


HATUA YA PILI;

Windows yako lazima itafanya boot kwenye menu kama inavyoonekana hapo chini,kisha chagua troubleshoot”


HATUA YA TATU;

Kompyuta yako itafunguka hapo na chagua “advanced options” Tazama picha hapo chini.

HATUA YA NNE;

Sasa kwa urahisi kabisa unaweza kubonyeza sehemu iliyoandikwa “restart” Tazama picha hapo chini.

HATUA YA TANO;

Mwisho kabisa utapata muonekano kama huu kwenye screen yako,na utabonyeza namba 7 kwenye keyboard yako na windows itajianzisha.

MWISHO;

Angalia kama unayo sauti kwenye kompyuta yako.

KUMBUKA;

Kama umesahau hizi hatua na ukafanya restart ya kompyuta yako kawaida,unaweza kushikilia batani ya shift huku kompyuta yako ikiendelea kufanya restart ya windows na ukafata hatua kama kawaida.