Nitaanza vipi kama sina mtaji wowote?
Jiunge MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Login MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Umesahau password yako?. Andika email yako hapo chini alafu bonyeza 'Reset'. Utapokea link katika email yako kwa ajili ya kutengeneza password mpya.
Tafadhali elezea kwa nini unahisi chapisho hili linapaswa kuripotiwa
Salim Jumbe
Kupitia Bwaya blog mwandishi anasema hivi
“Ni vizuri kuanza na kile ulichonacho, na si kile usichonacho.
Fursa mara zote, huwa pale ulipo na katu si kule ulipokuwaga.
Suala la msingi ambalo kila mmoja anapaswa kuliweka sawa, si kile ambacho angeweza kukifanya kama angekuwa na muda, elimu na namna ya kufanya, lakini kile ambacho angepaswa kukifanya kwa kutumia vile alivyonavyo.”
Kuweka sawa zaidi ni kwamba inabidi uanze kwa kuangalia ulichonacho(hauwezi kukosa) mfano elimu, sio lazima iwe elimu ya darasani. Unaweza anza na ujuzi ulionao labda kama ujuzi wa kufundisha, kuongea na watu vizuri ama chochote kile.
Pia unaweza kuangalia vitu ulivyowahi kununua, watu unaojuana nao au vitu vinavyopatikana kwa urahisi au vilivyo karibu nawe.
Anza sasa na ulichonacho, fikiria ‘version’ ndogo ya ile ndoto kubwa uliyonayo mfano anza kutengenezea keki nyumbani kama una ndoto ya kuanzisha bakery.