Nini maana ya mila na desturi?
Jiunge MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Login MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Umesahau password yako?. Andika email yako hapo chini alafu bonyeza 'Reset'. Utapokea link katika email yako kwa ajili ya kutengeneza password mpya.
Tafadhali elezea kwa nini unahisi chapisho hili linapaswa kuripotiwa
Flora Jumanne
Mila na desturi ni nini?
Tukianza na mila ni mambo yanayofanywa na jamii fulani ambayo yanalingana na asili, mazingira na nyendo za jamii hiyo. Desturi ni jambo la kawaida linalotendwa kila siku.
Hivyo tunaweza kusema mila na desturi ni sawa na utamaduni wa sehemu fulani. Wikipedia imeandika hivi kuhusu utamaduni. Utamaduni ni jinsi binadamu anavyokabili maisha katika mazingira yake. Hiyo inajumlisha ujuzi, imani, sanaa, maadili, sheria, desturi n.k. ambavyo mtu anajipatia kama mwanajamii.
Kama sifa maalumu ya binadamu, inayomtofautisha na wanyama, utamaduni ni suala la msingi katika anthropolojia, ukihusisha yale yote yanayopokezwa katika jamii fulani, kama vile lugha inayounganisha watu wanaohusika nao, fasihi, mafungamano, ndoa, michezo, ibada, sayansi na teknolojia.
Utamaduni ulioendelea unaitwa pia “ustaarabu”.
Kila utamaduni unabadilikabadilika mfululizo: ndani ya watu husika, baadhi wanachangia na kuunga mkono mabadiliko, wakati wengine wanayakataa. Ujuzi mpya na teknolojia, pamoja na mahitaji ya uchumi, ni kati ya mambo yanayosukuma zaidi kubadili kiasi fulani utamaduni.