Ni namna gani ya kuwateketeza kunguni na chawa ndani ya nyumba bila kutumia dawa za kisasa?
RickyllobbeProffesional
Jiunge MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Login MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Umesahau password yako?. Andika email yako hapo chini alafu bonyeza 'Reset'. Utapokea link katika email yako kwa ajili ya kutengeneza password mpya.
Tafadhali elezea kwa nini unahisi chapisho hili linapaswa kuripotiwa
Fred Moshi
Kunguni wanaweza kumsumbua mtu yeyote. Ni rahisi kuwadhibiti ukitambua mapema kwamba wapo. Kwa hiyo, jifunze kutambua ishara za kwamba wapo nyumbani na unaposafiri. Chunguza fanicha zako na vitu vingine vya mbao pamoja na mizigo, uone ikiwa kuna mayai madogo yanayofanana na mbegu ndogo nyeusi au alama za damu. Tumia tochi unapowatafuta kunguni ili uweze kuwaona.
Usiruhusu kunguni wawe na sehemu nyingi za kujificha. Ziba nyufa zote ukutani na kwenye viunzi vya milango. Ingawa kunguni hawaletwi na uchafu, itakuwa rahisi zaidi kuwatambua na kuwadhibiti ikiwa unasafisha nyumba kwa ukawaida na kupunguza vitu vilivyorundamana. Ukiwa hotelini, unaweza kupunguza uwezekano wa kubeba kunguni kwa kuepuka kuweka masanduku yako sakafuni na kitandani
Inaelezwa hivyo katika tovuti ya dw
Unaweza kuangalia video pia jinsi ya kutengeneza sumu ya kuwauua ukiwa nyumbani