Nimfanyie nini mwanamke ili anipende?
Jiunge MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Login MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Umesahau password yako?. Andika email yako hapo chini alafu bonyeza 'Reset'. Utapokea link katika email yako kwa ajili ya kutengeneza password mpya.
Tafadhali elezea kwa nini unahisi chapisho hili linapaswa kuripotiwa
Jose Mandingo
WANAUME wengi wanaamini wanawake, kwa kawaida, ‘wanapenda hela.’ Kwamba ukiweza kumhakikishia mwanamke ‘uhakika wa kiuchumi’ unakuwa umemaliza. Ingawa hatuwezi kupuuza ukweli kuwa uhakika wa ‘kiuchumi’ ni moja wapo ya mahitaji ya mwanamke, lakini si sahihi kuamini kuwa moyo wa mwanamke unaweza kuthamanishwa kwa fedha.
Hebu na tutazame mahitaji makubwa ya kihisia aliyonayo mwanamke mwenye upendo wa dhati kwa mwenzi wake.
Kupendwa kwa vitendo
Upendo kwa mwanamke unaeleweka anapoambiwa bila kuchoka na kuthibitishiwa kwa kutendewa vitendo kuwa anapendwa. Katika lugha ya kiingereza, hapa tungetumia neno affection, yaani matendo yanayoonesha mapenzi kwake.
Mfano, kumwambia mwanamke unampenda mara nyingi iwezekanavyo, ni hitaji la msingi. Kwa mwanamume, kuambiwa anapendwa inaweza isiwe jambo la maana, lakini si kwa mwanamke. Mwanamke anatamani kusikia mara nyingi kadri inavyowezekana kuwa anapendwa.
Pia kuna vitu kama kupewa zawadi asizotarajia, kutumia muda wa mapumziko pamoja nae, kutoka naye kwenda mbali na nyumbani na mambo kama hayo yanayoonesha kuwa kweli unampenda.
Anataka kuwa kipaumbele chako
Mwanamke hapendi kujikuta katika mazingira ya kushindania nafasi ya kwanza na kitu kingine chochote iwe ni kazi, mtu au chochote kile unachokipenda wewe mwanamume.
Mwanamke hatamani kuwa kwenye nafasi ya ‘mengineyo’, ‘ziada’, ‘baadae’ ‘nikipata muda’. Unapomweka ‘akiba’ mwanamke hawezi kufurahia kwa sababu anatamani awe kipaumbele chako.
Kueleweka kwa hisia zake
Kwa kawaida, wanaume hutamani kutoa majibu kwa matatizo. Uwezo wa kuwa na majibu ni sehemu muhimu ya heshima ya mwanamume. Ndio maana mwanamke anapomfuata mume wake pengine ili kusikilizwa na kueleweka, mara moja akili ya mwanamume hufanya kazi ya kuchakata majibu haraka na kuyakabidhi kwa mwanamke. Uharaka wa majibu humjengea mwanaume hali ya kujiamini.
Mwanamke anapokutana na changamoto kazini, kwa mfano, anapoudhiwa na watu wengine, anapohitafiana na majirani, anatamani mwenzi wake awe mtu wa kwanza kusimama upande wake na kuonesha kumwelewa. Ukiweza kuwa msikivu wa hisia za mwanamke unamfanya akuamini kwa alama nyingi kwa sababu umemwongezea hali ya kujiamini kuwa anaye mtu wa karibu anayemwelewa.
Uwazi wa mambo na kuambiwa ukweli
Katika macho ya mwanamke, usiri na faragha ni dalili ya kutokuwa mwaminifu. Sababu ni kuwa mwanamke anatamani zisiwepo siri zozote asizozijua katika kila kila kona ya maisha ya mume wake. Kujua mambo ya muhimu anayoyafanya mume wake kunamhakikisha kuwa ni kweli mume wake amempa nafasi ya kwanza.
Ikiwa unataka kuugusa moyo wa mke wako, jitahidi kuaminika kwa kufanya mambo yako kwa uwazi kadri unavyoweza. Mwambie unakokwenda, mwambie uliko, mshirikishe mipango yako, mshirikishe siri zako uzizoweza kumwambia mtu mwingine. Ukifanya hivyo, atakuamini na hatakuwa na sababu ya kukupeleleza.
Kusifiwa kwa ‘uanamke’ wake
Jitahidi kugundua mabadiliko anayoyafanya katika mwonekano wake na msifie kwa dhati. Unapofanya hivyo, unaongeza hali ya kujiamini kwake na anapojiamini atakuwa na nguvu ya kukupa heshima unayoihitaji kutoka kwake.
Wakati mwingine, ni kweli umbile la wanawake hubadilika kwa sababu nyingi ikiwemo uzazi. Mwanaume asiyefikiri vizuri huweza kuonesha kutokuvutiwa na mwonekano wake. Hali hiyo inamwuumiza mwanamke hata asiposema. Sababu ni kwamba anatamani awe na mvuto kwa mumewe.
Uhakika wa kiuchumi
Hili linaweza kuwa na sura ya kiutamaduni zaidi kuliko kimaumbile. Lakini katika mazingira yetu ya ki-Afrika, tafiti zinaonesha kuwa mwanamke [wa ki-Afrika] anatarajia kuwa majukumu mazito ya kifamilia hubebwa na mwanamume. Huo ndio ukweli. Mume wa ki-Afrika ndiye anayetarajiwa kujua wapi fedha zinakopatikana ili kukidhi mahitaji muhimu ya kifamilia.
Ukitaka kusoma kwa urefu zaidi bonyeza HAPA