Nifanyeje ili nisikate tamaa?
Jiunge MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Login MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Umesahau password yako?. Andika email yako hapo chini alafu bonyeza 'Reset'. Utapokea link katika email yako kwa ajili ya kutengeneza password mpya.
Tafadhali elezea kwa nini unahisi chapisho hili linapaswa kuripotiwa
Salim Jumbe
Maji ya Mto hukabiliana na vikwazo mbalimbali lakini huwa haviuzuii maji kutiririka. Mto unapokutana na Miamba, hata siku moja hauwezi kujadiliana na miamba eti upiteje, bali hutengeneza njia yake juu ya mwamba huo.
Mto unazo nguvu kiasi ya kwamba binadamu hujenga madaraja juu yake ili waweze kuuvuka, na pale unapojaa huweza kubomoa hata daraja.
Jitihada huwa hazizidi kudra, hebu kuwa kama mto. Usijadiliane na vikwazo unavyokubaliana navyo. Iwe ni kazi, mahusiano, ama umasikini.
Kwa imani ya kiwango cha juu, tengeneza njia yako na pita kwa kujiamini. Mungu atakuinua kama alivyowalinda Shadraki, Meshaki na Abedinego. Maana siku zote Ulipendalo hupati, hupata ujaaliwalo.
Furaha ya maisha yako inategemeana na quality ya mawazo yako. Mawazo yako ni kama sumaku, endapo utawazia baraka, utazivuta baraka na endapo utawaza matatizo, matatizo yatakuwa ni kimbilio kwako..
Siku zote palilia na kukuza mawazo mazuri, jiwazie mawazo mazuri maana aliwazalo mtu nafsini mwake ndivyo alivyo.
Natamani sana niwe na maneno sahihi ya kukwambia, natamani niwe na mistari iliyojaa matumaini itakayokufanya ujisikie amani ila fahamu kwamba, Kilimia kikizama kwa jua, huzuka kwa mvua, na kikizama kwa mvua, huzuka kwa jua.
Nikueleze jambo moja tu kwamba, weka tumaini lako lote kwa MUNGU na sio kwa Wanadamu. Kila jambo huwa na majira na msimu wake, Hamadi ni ilio kibindoni, na silaha ni iliyo mkononi.
There is victory at the end of your suffering. Don’t give up.
Source: JamiiForums
Promo – AjiraSearch
Ajira ya Ndoto Yako
Sasa kutafuta ajira ni rahisi zaidi kwa kutumia app hii.
Tazama AppRickyllobbe
Kitu ambacho unatakiwa kufanya ili usikate tamaa ni inabidi ujaribu kufanya kitu kile unacho kipenda muda wote