Jiunge

Jiunge MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection

Unayo account ? Log In

Unayo account ? Log in

Log In

Login MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection

Jiunge Hapa

Umesahau Password?

Hauna Account, Jiunge Hapa

Umesahau Password

Umesahau password yako?. Andika email yako hapo chini alafu bonyeza 'Reset'. Utapokea link katika email yako kwa ajili ya kutengeneza password mpya.

Unayo account ? Log in

Tafadhali andika jina lako kamili.

Tafadhali andika E-Mail yako.

Please choose an appropriate title for the question so it can be answered easily.

Tafadhali elezea kwa nini unahisi chapisho hili linapaswa kuripotiwa

Sign InSign Up

1Sky

1Sky

1Sky Navigation

  • Blog
  • Wasiliana Nasi
  • Advanced Search
  • App

Mobile menu

Close
Uliza Swali
  • Home
  • Maswali
  • Points
  • Miongozo
  • Wasiliana Nasi
  • Advanced Search
  • App
Home» Maswali»Q 34544
In Process
Adv
Anonymous
Asked: January 11, 20202020-01-11T09:39:35+03:00 2020-01-11T09:39:35+03:00Wazazi

Nifanyeje ili mtoto wangu anisikilize na kuniamini?

Nifanyeje ili mtoto wangu anisikilize na kuniamini?
  • 1
  • 257
  • 0
  • Share
    • Share on WhatsApp
    • Share on Facebook
    • Share on Twitter
Jibu
  • Report
Adv

Jibu 1

  • Kura
  • Zamani
  • Mpya
  1. 1sky

    1sky

    • Dar es Salaam, Tanzania
    • 1 Question
    • 17 Answers
    • 0 Best Answers
    • 22 Points
    View Profile
    1sky New
    2020-01-11T09:47:19+03:00Jibu - January 11, 2020 saa 9:47 am
    Jibu hili limerekebishwa.

    TAFITI zinaonesha kwamba watoto wengi  ni ‘mayatima’ wenye wazazi tunaoishi lakini hatupo kwenye maisha yao. Wazazi tupo lakini hatuna muda wa kujua hisia zao, fadhaa zao, maoni yao, hofu zao na hata matumaini yao. Aidha, tafiti hizo hizo zinasema wazazi wengi tunatumia muda mwingi na watoto wetu ama kuwaonya, kuwakosoa ama kuwapa hotuba/maagizo ya ‘fanya hivi, acha hiki’ kuliko tunavyowasaidia kujenga mahusiano ya moja kwa moja kati yetu na watoto.

     

    ‘Elimu ya kujitegemea’ inavyowaathiri watoto

    Wazazi wengi tunasubiri watoto ‘wapate akili’ ili tuanze dozi rasmi ya mihadhara ya maagizo, maelekezo, makanyo, maonyo na kadhalika, tukiamini mtoto hujifunza kwa mafundisho rasmi. Wakati mwingine tunaamini fimbo ndilo jibu la tabia njema ya mtoto. Tunatumia na vifungu vya biblia, ‘Usimnyime mtoto mapigo/fimbo’. Na tunawachapa kweli tukitarajia heshima na adabu.

     

    Mtoto huyu anapofikia umri wa kuanza kufanya mambo yake kwa uhuru kwa kutumia elimu hiyo aliyoipata kwa mfumo wa kujitegemea tangu amezaliwa , tena bila ‘ukaguzi’ wa mzazi, ndipo mzazi hukumbuka ‘shuka asubuhi’. Huurejea wajibu wake na huanza jitihada za kutafuta/kulazimisha urafiki na mtoto wakati ambao mtoto hana haja na urafiki huo. Too late wanasema wazungu. Shughuli pekee inayoweza kufanyika kwa ufanisi katika kipindi hiki kizito ni kulalamika, kufoka na kuadhibu, mahusiano ambayo kwa hakika huongeza umbali wa mawasiliano baina ya mtoto na mzazi. Mzazi humwona mtoto ameasi, na mtoto humwona mzazi anajipendekeza na kumfuata fuata.

     

    Tuyape malezi uzito unaostahili

    Ili kukwepa fedheha ya kulazimisha urafiki na mtoto hapo baadae, tunashauriwa sisi kama wazazi tuyape malezi uzito unaostahili kuanzia pale tunapofikiria kupata mtoto. Na kwa kweli malezi ndiyo fursa pekee ya mtu kubadili maisha ya mtu mwingine vile apendavyo. Fursa hii huwezi kuipata hata kwa mwenzi/mpenzi wako maana katika mahusiano ya ukubwani kinachotokea zaidi ni kuchukuliana na sio kubadilishana tabia. Kwa hiyo kama kuna fursa pekee ya kubadili mtu katika dunia hii ni malezi. Tuitumie.

     

    Tupatikane kwa watoto, tuwasiliane na mioyo yao mapema

    Hatuwezi kuwasiliana na moyo wa mtoto pasipo kupatikana. Kuwa nao, kucheza nao, kutembelea nao, kuzungumza nao na mambo yanayofanana na hayo huhakikisha tunaweka alama njema ya kudumu katika maisha ya mtoto. Kupatikana na kuwasiliana na moyo wa mtoto ni muhimu kuanze tangu anapozaliwa au hata anapohesabu majuma tumboni mwa mama.

     

    Hivi kwa jinsi maisha yalivyobana namna hii, wazazi tunapata hata dakika hizo kumi kwa siku kukaa na wanetu na kuwasikiliza na kuwasiliana nao kirafiki ukiacha kuonya na kuadhibu? Wengine tunaishi Dar es Salaam kikazi, watoto wako kwa bibi yao! Si ajabu hatufanikiwi kuwa na influence yoyote kwa watoto. Wakianza kufanya vitu vyao, tunaishia kulalamika ‘watoto wa siku hizi wameharibika.’

     

    Tuwe vile tunavyotaka watoto wawe

    Mtoto hujifunza kwa kiasi kikubwa kupitia kile kinachofanywa na watu wake muhimu wanaomzunguka. Ni muhimu kufanya kile tunachotaka mtoto akifanye. Tuwe na tabia na imani tunazotaka kuzihamisha kwa mtoto. Mathalani, kama ninatamani mtoto awe msomaji wa vitabu, ni lazima nihakikishe ninajenga mazingira ya usomaji nyumbani kwa kuonesha mfano mimi mwenyewe. Mtoto anakua akijua maisha ni kusoma. Na sihitaji kumwandalia somo la ‘umuhimu wa kusoma vitabu’ ili ajenge tabia ya kusoma. Nafanya ninachotaka afanye. Aone nikifanya ibada kama ningependa awe mwombaji na yeye. Niwe na upendo kwake na mke wangu kama ninataka awe mtu wa upendo kwa watu.

     

    Tuwapende watoto, wajisikie kukubalika

    Ninapompenda mtoto vile alivyo bila kujali alichokifanya ninamfanya aelewe maana ya upendo na aniamini. Simpendi ili nimdai tabia njema. Hapana. Nampenda hata anapokosea. Nampenda kwa sababu ni mwanangu apatie au akosee. Na wala si kumdekeza. Wakati mwingine tunakosea kama wazazi. Tunawapenda watoto kama malipo ya tabia njema. Na wakati mwingine hatufichi, tunawaambia waziwazi kuwa tutawapenda kama watafanya tulichowaagiza kukifanya. Tutawapa zawadi wakifanya vizuri. Conditions.

     

    Tushughulike na msongo wa nafsi zetu kwanza

    Kazi ya kulea inahitaji nafsi iliyotulia. Nafsi isiyotafuta amani kwa kuumiza wengine. Ninapokuwa mzazi mwenye nafsi iliyosongwa na matatizo siwezi kutekeleza ipasavyo jukumu nyeti la malezi yatakayomjenga mtoto anayejitambua, anayejiamini na atakayekabiliana na changamoto za maisha ya ukubwani. Nitajikuta nikimtumia mtoto kama dodoki la kufyoza ugonjwa unaoisumbua nafsi yangu. Nitakuwa mwepesi, pasipo mimi kujua, kusema maneno magumu yasiyolingana na umri wa mtoto. Nitajisikia kuridhika kumfanya mtoto alie na kukosa amani. Nitaadhibu na kukemea kuliko ninavyowajibika kujenga imani, mitazamo na tabia njema.

     

    Kusoma chapisho hili kwa urefu zaidi tembelea HAPA

    • 0
    • Reply
    • Share
      Share
      • Share on WhatsApp
      • Share on Facebook
      • Share on Twitter
      • Report
Jibu swali hili

Jibu swali hili
Cancel reply

Chagua
Captcha Click on image to update the captcha.

Adv

Sidebar

Uliza Swali

Promo

  • Usihangaike tena, Tumekuwekea Kampuni zote za kubet katika app moja! Jaribu Sasa

  • Beti kwa mara ya kwanza, ukishindwa unarudishiwa hela yako

  • Tafuta Ajira kiurahisi. Jaribu Sasa

  • Jifunze jinsi ya kubet kibingwa

  • Maswali yanayoendana

    • Nifanyeje ili mtoto wangu asiwe anadanganya?

    Explore

    • Home
    • Maswali
    • Polls
    • Points
    • Watumiaji
    • Miongozo
    • App

    MojaSky | Designed by ChuiTec.

    Insert/edit link

    Enter the destination URL

    Or link to existing content

      No search term specified. Showing recent items. Search or use up and down arrow keys to select an item.