Ni halali mwanamke kuhubiri au kuwa mchungaji?
Ni halali mwanamke kuhubiri au kuwa mchungaji?
Jiunge MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Login MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Umesahau password yako?. Andika email yako hapo chini alafu bonyeza 'Reset'. Utapokea link katika email yako kwa ajili ya kutengeneza password mpya.
Tafadhali elezea kwa nini unahisi chapisho hili linapaswa kuripotiwa
Emmanuel Magessa
Mistari muhimu ya kukumbuka:-
1 WAKORINTHO 14:34-36:-
34 Wanawake na wanyamaze katika kanisa, maana hawana ruhusa kunena bali watii, kama vile inenavyo torati nayo.
35 Nao wakitaka kujifunza neno lo lote, na wawaulize waume zao wenyewe nyumbani mwao; maana ni aibu wanawake kunena katika kanisa.
36 Au je! Neno la Mungu lilitoka kwenu? Au kuwafikia ninyi peke yenu?
1 TIMOTHEO 2:11-12:-
11 Mwanamke na ajifunze katika utulivu, akitii kwa kila namna.
12 Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha, wala kumtawala mwanamume, bali awe katika utulivu.
HII NI MADA YENYE UBISHI MKUBWA miongoni mwa vichwa vya watu wengi . Na maandiko hayo kwa kueleweka isivyo sahihi hutumiwa na baadhi ya watu wengi kujaribu kujenga hoja zao za kupinga kwamba mwanamke hana haki yoyote ya kuwa Mchungaji wala kusimama madhabahuni kuwahubiria watu kanisani.
Jambo hili limeleta mzozano mkubwa na mpasuko ndani ya makanisa mengi ya Mungu, kuhusu uhalali wa mwanamke kuhubiri madhabahuni na kuwa Mchungaji. Kuna mawazo ya positive na Negative, kuna wengine wanaona ni sahihi na kuna wengine kwao siyo sahihi kabisa .
Sasa basi ukweli na usahihi wa maandiko hayo ni upi basi? Je, ni sahihi kwamba mwanamke hatakiwi kuhubiri madhabahuni kanisani au kuwa Mchungaji ? Tatizo ni kwamba Maandiko hayo hayaeleweki vizuri kwa kwa wakristo wengi na hata baadhi ya wachungaji na Maaskofu, wanalifafanua hilo Andiko kwa maana potofu kabisa .
NB:-
Kuitwa Mtume, Nabii Askofu au Mchungaji n.k. Siyo kigezo kikubwa cha kwamba wewe unaielewa sana Biblia kwa usahihi wake. La asha ! Ndiomaana wako hata wachungaji wengine tena wengi tu ambao huyatafsiri maandiko isivyo na kuyapotosha kwa tamaa zao wenyewe.
MWALIMU MKUU WA BIBLIA NI ROHO MTAKATIFU; yeye ndiye aliyeyaleta maandiko hayo kwetu. Na hatuwezi sisi kuamua kuyatafsiri maandiko hayo vyovyote tu kama apendavyo mtu fulani kutafsiri. La Asha
[ 2 PETRO 1:19-20 ] .
Bali katika kanuni za kuyatafsiri maandiko, tunahitaji sana maongozi ya msaada wa Roho Mtakatifu mwenyewe katika kuyasoma na kuyaelewa maandiko vizuri na kuyatafsiri kwa usahihi wake. Neno la Biblia. Tunaweza kulifaham kwa kufunuliwa na Roho Mtakatifu pekee yake. Ndiomaana Yesu alisema uliwaficha wenye hekima na Akili (Wasomi), ukawafunulia watoto wachanga (Watu wasio na elimu) . Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyokupendeza mbele zako [ MATHAYO 11:25-26]. “Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho Mtakatifu . Maana Roho huchunguza yote hata mafumbo ya Mungu. Lakini sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu makusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu ” .
[1 WAKORINTHO 2:10-15].
Si hilo tu. Nikodemo alikuwa ni mwalimu mkuu wa chuo cha Torati. Na watu walimwamini sana katika Taifa la Israeli. Lakini Nikodemo alipoambiwa na Yesu maneno mepesi tu ya Mungu , na usomi wake wote, alishindwa kuyaelewa maana yake nini !! Sasa Yesu ambaye hakupita chuo chochote cha Theolojia, ikambidi amfundishe Nikodemo, mwalimu mkuu wa chuo cha Theolojia ya Torati.
[ YOHANA 3:1- 10 ]
Sisemi wala kupinga kwamba kusoma chuo cha Biblia ni kosa au ni vibaya, au ni dhambi. Hapana. Ni nini maana ya kuanza kukwambia hayo. Maana yangu ni hii kwamba :- Ondoa dhana potofu ukafikili kila mtu anayeitwa Mchungaji, Askofu au Mwanatheolojia fulani msomi anaielewa sana Biblia ki-maana. Ukiwa na mawazo hayo tu, utapotezwa na kudanganyika sana Mpendwa . Na Mungu huwa hatendi kazi kwa misingi hiyo. Mchungaji /Ev/ Mwanatheolojia huyo Anaweza kuielewa Biblia kwa namna fulani tu ya akili hivi , lakini asiweze kabisa kuielewa Biblia kwa jinsi ya rohoni zaidi kwa ufunuo wa Roho Mtakatifu . Na maana ya kweli ya maneno ya Biblia hutumbalikana kwa jinsi ya rohoni zaidi na sio kwa jinsi ya mwilini.
[ WAGALATIA 1:11-12 ; WAEFESO 1:17-19].
Hivyo ni vema zaidi tusiweke vipimo vyetu vya usomi kama kigezo cha kuitafsiri Biblia; bali tumuhitaji sana Roho wa Mungu ndio atuongoze katika kulitafsiri Neno lake Mungu.