Ni apps gani unahisi kila mtu inabidi awenazo katika simu yake?
Pinned
Jiunge MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Login MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Umesahau password yako?. Andika email yako hapo chini alafu bonyeza 'Reset'. Utapokea link katika email yako kwa ajili ya kutengeneza password mpya.
Tafadhali elezea kwa nini unahisi chapisho hili linapaswa kuripotiwa
Calvin Mlay
Kuna apps nyingi siku hizi lakini kuna apps ni muhimu zaidi ya nyingine. Sitaongelea apps ambazo unazikuta kwenye simu na hauwezi ata kuzi uninstall mfano Google Playstore, message app, camera, notebook, file manager nk. zaidi ni kwa watumiaji wa simu za Android.
Whatsapp
watu wengi wanajua umuhimu wa app hii. Inakupa uwezo wa kutuma ujumbe kwa kutumia internet kupiga simu kwa internet kutuma aina mbalimbali za mafaili na mengine mengi.
Gmail
app ya email ni muhimu sana katika simu yako, Ila gmail ni muhimu zaidi katika simu ya android kwa sababu apps nyingine nyingi zitahitaji kuwa na accout ya gmail kuweza kuzitumia, na pia unaweza kutumia email kutoka yahoo au outlook katika app hii.
Wps office
ukitaka kusoma documents katika simu yako vizuri ni vema ukatumia wps office, inasoma aina zote za documents ikiwemo pdf,powerpoint na exel. Pia unaweza kuitumia kuedit document hizo.
Google Chrome
browser yenye uwezo mkubwa wa kufanya mambo makubwa katika simu yako. Ukitumia utapata uwezo a kuingia website yoyote, inasave password mojakwamoja katika email yako ya gmail nk.
Google drive
Umewahi kupoteza picha na vitu vingine wakati ulipopoteza simu yako? ukiwa na app hii inakupa uhakiaka wa kupata tena vitu vyako ikiwemo picha, video, majina na message za whatsapp.
Swiftkey
App hii nadhani ndio bora katika apps za keybord. ina uwezo wa kusave maneno yako unayoandika kila siku ili mara nyingine ikusaidie katika kumalizia(autocorrect) na pia ina maneno ya kiswahili.
Xender
kushare ni kitu muhimu katika ulimwengu wa sasa. kwa kutumia Xender unaweza kutuma na kupokea vitu kutoka katika simu kwenda kwenye simu nyingine au kompyuta na kinyume chake.
Google Maps
Watu wengi wamezoea kwenda sehemu na kuuliza kuwas sehemu fulani ni wapi mwisho kuishia kupotezwa na mtu aidha kwa kukusudia au bila kukusudia, ukitumia app hii unaweza kutafuta eneo unaloenda njia utakayotumia na kwa usafiri unaotaka. pia kuna vitu vingine vingi. anza kutumia uone mengi zaidi.
Shazam
je umeusikia mziki unaopenda na ukashindwa kujua jina lake? Shazam ndio jibu lako.
Nova Laucher
Hii ni app inayobadilisha mwonekano wa simu yako kuanzia kwenye desktop hadi kwenye menu.