Neema ni nini?
Jiunge MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Login MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Umesahau password yako?. Andika email yako hapo chini alafu bonyeza 'Reset'. Utapokea link katika email yako kwa ajili ya kutengeneza password mpya.
Tafadhali elezea kwa nini unahisi chapisho hili linapaswa kuripotiwa
Emmanuel Magessa
Katika Biblia Agano Jipya neno “Neema” limetokana na maneno mawili ya Kigiriki ambayo yametafsiriwa kama neema. Neno la kwanza ni “Charis” (khar’-ece) lenye maana ya upendeleo, wema, uwezesho; na neno hili limejitokeza katika Biblia katika Agano Jipya mara 157. Kutokana na neno hili la kwanza tunaweza kusema kuwa neema ni upendeleo na wema wa Mungu kwa mwanadamu ambao umekuja kwa njia ya Yesu Kristo.
Neno la pili la Kigiriki lililotafsiriwa kama neema katika Agano Jipya ni “Charisma” (khar’-is-mah) lenye maana ya karama au kipawa cha neema kinachotolewa bure, au upendeleo asiostahili mtu. Neno hili katika Agano Jipya limejitokeza mara 17. Na katika maana hii, karama na vipawa vyote vya Roho vinahesabiwa kuwa ni neema ya Mungu kwa mwanadamu.
Nini maana ya neema sasa?
Neema ni kipawa cha Mungu kwa mwanadamu kinachotolewa bure ambacho huachilia upendeleo na wema wa Mungu kwa mwanadamu. Ni upendeleo wa Mungu kwa mwanadamu asiostahili mtu ambao Mungu anauachilia kwa mwanadamu akionyesha wema wake kutoka katika pendo lake lisilokuwa na sababu wala masharti. Kwa kifupi tunaweza kusema kuwa, neema ni kustahilishwa wema wa Mungu pasipo kustahili kwa sababu ya pendo lake kwa mwanadamu.
Kustahilishwa pasipo kustahili nini maana yake:
Tangu mwanadamu alipomtenda Mungu dhambi hakustahili tena kupata wema wa Mungu maishani mwake isipokuwa hukumu kwa sababu ya dhambi zake. Lakini Mungu kwa njia ya Yesu Kristo amemstahilisha mwanadamu mema na wema wake wote si kwa sababu ya matendo yake bali kwa sababu ya Yesu Kristo kufa kwa ajili ya mwanadamu