Nawezaje kuunda blog?
Jiunge MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Login MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Umesahau password yako?. Andika email yako hapo chini alafu bonyeza 'Reset'. Utapokea link katika email yako kwa ajili ya kutengeneza password mpya.
Tafadhali elezea kwa nini unahisi chapisho hili linapaswa kuripotiwa
ChuiTec
Kutengeneza blog ni rahisi sana. Kitu cha kwanza inatakiwa uwe unajua unahitaji blog ya aina gani na ni kwa ajili ya nini. Kama ni kwa ajili ya kuchapisha maswala binafsi tu au kwa ajili ya kujifurahisha unaweza tumia Blogger.
Blogger ni njia rahisi ya kutengeneza blog bila hata kuwa na ujuzi wowote. Ila kama una ujuzi kidogo (html&css) itakua faida kwako. Kuunda blog kwa kutumia blogger nenda blogger.com au unaweza kupata ushauri wa bure HAPA.
Kama ni kwa ajili ya biashara au unahitaji kuwa siriazi na kutengeneza pesa kupitia blog, nakushauri utumie WordPress. Hii ni njia nyingine rahisi ya kutengeneza blog au website yoyote hata kama hauna ujuzi mkubwa. Ila tofauti ya njia hii na hiyo hapo juu ni kuwa hii unapaswa kulipia hosting na domain name. Malipo yake yanaweza kuanzia Tsh 100,000 kwa mwaka.
Sababu za kwa nini utumie njia hii ni kuwa utatengeneza blog inayoonekana professional na itakuwa rahisi kupata watumiaji wengi kwa sababu wordpress ina mfumo mzuri wa kupata watumiaji kutokea search engine kama Google
Unaweza kupata ushauri bure kabisa HAPA