Nawezaje kutumia forex kuingiza hela?
Jiunge MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Login MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Umesahau password yako?. Andika email yako hapo chini alafu bonyeza 'Reset'. Utapokea link katika email yako kwa ajili ya kutengeneza password mpya.
Tafadhali elezea kwa nini unahisi chapisho hili linapaswa kuripotiwa
Mugabe Abraham
FOREX ni ufupisho wa FOReign EXchange (ubadilishaji wa fedha za kigeni). Zimechukuliwa herufi tatu za mwanzo kwenye neno FOREIGN na herufi mbili za mwanzo kwenye neno EXCHANGE (FOREX).
Forex ni soko kubwa na ambalo linakua kwa kasi duniani. Mzunguko wake wa siku ni zaidi ya dola trillion tano ($5 Trillion) za kimarekani ambayo ni kiasi kikubwa kuliko soko lolote duniani,mfano wa masoko makubwa duniani ni NEW YORK STOCK MARKET(MAREKANI), TOKYO(JAPANI), FRANKFURT MARKET(UJERUMANI) , SYDNEY MARKET(AUSTRALIA) , LONDON MARKET(UINGEREZA) NA HONG KONG MARKET(CHINA). Wahusika kwenye soko hili ni benki kuu na mabenki ya kibiashara, Corporations, taasisi za uwekezaji, Hedge funds na watu wa kawaida kama wewe.
Soko ni sehemu ambalo bidhaa zinauzwa. Pia hata kwenye Forex kuna bidhaa kama vile sarafu za nchi mbalimbali na madini kama Dhahabu na silver pamoja na mafuta. Unaweza ukanunua au ukauza Euro(EUR) dhidi ya dolla(USD) ya marekani na ukapata faida. Yako mambo mengine mengi kwenye soko letu hili la FOREX yenye faida kama utaweza kuyafatilia na kuyajua kwa undani