Jiunge

Jiunge MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection

Unayo account ? Log In

Unayo account ? Log in

Log In

Login MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection

Jiunge Hapa

Umesahau Password?

Hauna Account, Jiunge Hapa

Umesahau Password

Umesahau password yako?. Andika email yako hapo chini alafu bonyeza 'Reset'. Utapokea link katika email yako kwa ajili ya kutengeneza password mpya.

Unayo account ? Log in

Tafadhali andika jina lako kamili.

Tafadhali andika E-Mail yako.

Please choose an appropriate title for the question so it can be answered easily.

Tafadhali elezea kwa nini unahisi chapisho hili linapaswa kuripotiwa

Sign InSign Up

1Sky

1Sky

1Sky Navigation

  • Blog
  • Wasiliana Nasi
  • Advanced Search
  • App

Mobile menu

Close
Uliza Swali
  • Home
  • Maswali
  • Points
  • Miongozo
  • Wasiliana Nasi
  • Advanced Search
  • App
Home» Maswali»Q 34579
In Process
Adv
Anonymous
Asked: January 12, 20202020-01-12T07:54:07+03:00 2020-01-12T07:54:07+03:00Mapenzi

Nawezaje kutokuwa na wivu kwa mpenzi wangu?

Nawezaje kutokuwa na wivu kwa mpenzi wangu?
  • 1
  • 435
  • 0
  • Share
    • Share on WhatsApp
    • Share on Facebook
    • Share on Twitter
Jibu
  • Report
Adv

Jibu 1

  • Kura
  • Zamani
  • Mpya
  1. Jose Mandingo

    Jose Mandingo

    • Dar es Salaam, Tanzania
    • 0 Questions
    • 33 Answers
    • 0 Best Answers
    • 175 Points
    View Profile
    Jose Mandingo Advanced
    2020-01-12T07:57:57+03:00Jibu - January 12, 2020 saa 7:57 am
    Jibu hili limerekebishwa.

    Unapopata hisia za wivu, jambo la kwanza la kufahamu ni kwamba bado hujaweza kujiamini ipasavyo. Hujaweza kujipenda mwenyewe. Tafuta msaada wa kitaalamu uweze kujiamini na kujipenda mwenyewe kwanza kabla ya kusubiri mtu mwingine akupende kwa kiasi unachotaka. Na kuna ukweli fulani kwamba ni mara chache unaweza kumbadilisha mwenzako. Kumbe kwa kutokujiamini na kujipenda, unajiwekea mazingira ya kuteseka unapoingia kwenye mahusiano.

     

    Kwa lugha rahisi kabisa, hisia za wivu maana yake ni kutokuamini watu. Una mashaka na tabia za watu. Unaamini uko sahihi, wengine wanakosea. Badilika. Tafuta msaada uweze kuwaamini watu. Itakusaidia kuepuka kuteseka kwa mambo yasiyokuwepo kwa sababu tu huwezi kuwaamini watu. Kutokuamini, ndiyo wivu wenyewe.

     

    Ni kweli kuwa wakati mwingine hisia za wivu huwa hisia za hali iliyopo. Kwamba ni kweli yupo mtu wa tatu katika mahusiano yenu. Kama mwanadamu unajisikia vibaya. Lakini dawa si wivu wa kiwango cha kupambana na mshindani wako. Katika mazingira hayo, wakati mwingine tatizo huwa ni wewe. Ndio. Huenda hujalipa gharama ya kumfanya mpenzi wako ajisikie kupendwa na kuthaminiwa.

     

    Huenda umemfanya ajisikie kutumika kama daraja la mtu kufikia malengo mengine ya kimaisha. Badilisha mtazamo wako. Tafuta msaada wa kukufanya ujisikie mwenye wajibu wa kuleta mabadiliko kwenye mahusiano yako. Wivu haukusaidii kutatua matatizo yako.

     

    Wivu usikufanye upambane na mtu asiyehusika. Hasira ni kiburi. Hasira, tunaambiwa haijawahi kutenda haki. Itakugharimu kukarabati mahusiano kwa kuongeza duara la mapambano na mtu wa tatu. Pambana na mwenzi wako kwa kumpa haki yake. Kama una hakika analo tatizo la kuvutwa na vya nje, kabiliana naye abadilike. Tafuteni msaada wa kitaalam kushughulikia mahusiano yenu. Hamna haja ya kupambana na mtu wa tatu ambaye kimsingi mmemkaribisha wenyewe.

     

    Wivu ni sumu mbaya katika mahusiano. Unapojisikia hatari ya kumpoteza mpenzi wako, unapojisikia unatumia nguvu nyingi kuliko anazotumia yeye, maana yake ni kwamba bado hujampenda. Ni hatari ya hisia zako, na za mwenzako. Unajeruhi hisia zao mara nyingi kwa jambo lisilokuwepo. Unajikuta unachukua hatua zinazoongeza majeraha hata baada ya kushughulikia tatizo lenu. Upendo wa kweli hauhesabu gharama. Upendo hauna masharti. Unapompenda mtu, hufikirii yeye anafanya nini. Na unapofanya hivyo, mara nyingi, unamsababisha kubadilika.

     

    Kabla hujafanya maamuzi ya kuhusiana na mtu, jitathimini. Jichunguze mwenyewe kwanza. Je, unajiamini? Unaamini wengine? Unafikiri nini kuhusu kupenda na kupendwa? Je, mahusiano ni kulipa gharama au kutarajia kutendewa? Kama huna hakika, tafuta msaada ndipo uweze kuingia kwenye mahusiano. Vinginevyo, utamjeruhi huyo unayetaka kuhusiana nae, utajijeruhi mwenyewe, na zaidi, utajeruhi wengine. Kwa sababu wivu, imethibitika, ni jaribio la kumtumia umpendaye kudhihirisha ulivyo na mtazamo hasi nafsi yako mwenyewe. Ishughulikie.

    Chanzo : Bwaya blog

    • 0
    • Reply
    • Share
      Share
      • Share on WhatsApp
      • Share on Facebook
      • Share on Twitter
      • Report
Jibu swali hili

Jibu swali hili
Cancel reply

Chagua
Captcha Click on image to update the captcha.

Adv

Sidebar

Uliza Swali

Promo

  • Usihangaike tena, Tumekuwekea Kampuni zote za kubet katika app moja! Jaribu Sasa

  • Beti kwa mara ya kwanza, ukishindwa unarudishiwa hela yako

  • Tafuta Ajira kiurahisi. Jaribu Sasa

  • Jifunze jinsi ya kubet kibingwa

  • Maswali yanayoendana

    • Nawezaje kuzipata sms za mke wangu katika simu yangu ambazo zinatumwa na watu wake?

    • Nimfanyie nini mwanamke ili anipende?

    • Wanaume wanahitaji nini katika mahusiano?

    • Aina gani za wanaume wa kuepuka katika mahusiano?

    • Sifa za mwanamke anayefaa kuolewa ni zipi?

    • Dalili zipi zinaonesha kuwa mwanamke anaweza kuwa msaliti?

    Explore

    • Home
    • Maswali
    • Polls
    • Points
    • Watumiaji
    • Miongozo
    • App

    MojaSky | Designed by ChuiTec.

    Insert/edit link

    Enter the destination URL

    Or link to existing content

      No search term specified. Showing recent items. Search or use up and down arrow keys to select an item.