Nawezaje kutengeneza app?
RickyllobbeProffesional
Jiunge MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Login MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Umesahau password yako?. Andika email yako hapo chini alafu bonyeza 'Reset'. Utapokea link katika email yako kwa ajili ya kutengeneza password mpya.
Tafadhali elezea kwa nini unahisi chapisho hili linapaswa kuripotiwa
ChuiTec
Kama ungependa kujua jinsi ya kutengeneza app ya android bila kuwa na ujuzi yani programming endelea kusoma . Kama ungependa kujua namna ya kutengeneza app hizo kwa njia ya programming yani Android Studio na nyingine post hii haielezei kuhusu hilo japo unaweza kujifunza mambo kadhaa ambayo ni muhimu pia.
Hatua za kufuata kutengeneza app yako
1.Research (fanya uchunguzi)
Unatengeneza app kwa nini? Labda unataka kutatua tatizo fulani mfano app ya Thl ni utatuzi wa tatizo la notes kwa wanafunzi. Pia unaweza kuamua kutengeneza app kwa ajili ya burudani, app kwa ajili ya wewe kujifunza tu au hata app isiyokuwa na maana yoyote
Kama unatengeneza app kwa ajili ya biashara ni vizuri ukajua watumiaji watakuwa wa kina nani? watakuwa tayari kulipia? Unatoa huduma ambayo watu wataihitaji? na mengine yanayofanana na hayo
2.Tengeneza app yako
Ukishajua app unayohitaji kuitengeneza unakuja kwenye hatua muhimu kabisa ya kuitengeneza app yako. Njia rahisi ni kwa kutengeneza app online yaani katika website zinazotoa huduma hiyo. Unaweza kutumia njia hizi rahisi.
AppCreator 24
Kama unataka kutengeneza app hasa kwa ajili ya blog au website yako ili ni chaguo bora. Unachotakiwa kufanya ni kuingia katika website yao unajiunga au una log in alafu utaweza kutengeneza app yako ndani ya dakika chache tu.
Andromo
Unataka kutengeneza app kwa ajili ya Masomo, sauti, ramani, picha, ukurasa wa youtube, blog au website unaweza tumia hii. Unachotakiwa kufanya ni kuingia katika website yao ili kuanza kutengeneza app yako. TanzaniaTech wameeleza hatua jinsi ya kutengeneza app kwa kutumia Andromo hapa
Website nyingine zinazoweza kufanikisha lengo lako ni kama
3.Test app yako
Hii ndiyo hatua inayofurahisha zaidi. Hapa unajaribu app uliyoitengeneza kama inakidhi vigezo na matarajio uliyoyaweka kabla ya kuitengeneza app yenyewe. Kama unatumia kompyuta kutengeneza ni vyema ukawa na simu kwa ajili ya ku test.
4.Sambaza app yako
Kama umemaliza hatua zote sasa unaweza kuiweka app yako katika platforms mbalimbali na hata kufanya matangazo kwa ajili ya kupata watumiaji. Unaweza kuiweka Google Play Store (ni muhimu kwa sababu watumiaji wengi wapo hapa), Amazon App Store na nyingine.