Nawezaje kutekeleza malengo niliyojiwekea?
Jiunge MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Login MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Umesahau password yako?. Andika email yako hapo chini alafu bonyeza 'Reset'. Utapokea link katika email yako kwa ajili ya kutengeneza password mpya.
Please briefly explain why you feel this question should be reported.
Tafadhali elezea kwa nini unahisi chapisho hili linapaswa kuripotiwa
Please briefly explain why you feel this user should be reported.
Tabia saba muhimu unazohitaji kuzibadili ili uweze kufanikiwa
Kuyatazama maisha kwa malengo ya muda mfupi
Malengo yanayoweza kubadili uelekeo wa maisha yako, mara nyingi, yanahitaji uwezo wa kuyatazama mambo kwa jicho la muda mrefu. Huwezi kufanikiwa kwa kuendeleza mtazamo mfupi. Huwezi kufanikiwa kwa kutazama kile unachohitaji leo.
Kuacha visingizio
Huwezi kufanikiwa kwa kuwategemea watu wengine watekeleze wajibu wako. Unahitaji kufikiria nafasi uliyonayo wewe katika kufikia malengo yao mwenyewe. Usitegee malengo yako mwenyewe kwa kusubiri watu wengine wafanye.
Usifanye mambo mengi kwa wakati mmoja
Huwezi kukimbiza sungura wawili kwa wakati mmoja na ukawapa. Utawakosa wote. Ndivyo ilivyo mara nyingi tunavyotekeleza mipango yetu. Tunataka kufanya mambo yote kwa wakati ule ule. Hasara yake ni kujikuta tukiyafanya mambo yote nusu nusu.
Jifunze kusema hapana
Usiwe mwepesi kusema kusema ‘sawa’ kwa mambo yasiyo ya lazima. Mara nyingi ‘sawa’ unazozitoa kwa lengo la kuwaridhisha watu wengine zinaweza kukwamisha malengo yako kwa kiasi kikubwa. Jifunze kusema hapana kwa maombi yanayoingiliana na malengo uliyonayo.
Jitenge na watu wasiokujenga
Chagua watu wanaofanana na malengo yako. Tafuta watu wanaoyaishi malengo uliyonayo. Kama unataka kuwa na familia imara mwaka huu, jenga urafiki na watu wenye familia imara. Utajifunza kwao. Kama unataka kufanya biashara fulani, jenga urafiki na watu wanaofanya biashara hiyo.
Usitumikishwe na mitandao ya kijamii
Katika mazingira haya, ni rahisi kupoteza muda mwingi kwenye mitandao ya kijamii. Tafiti zinazonesha kuwa watu wengi wanapoteza muda mwingi kwenye mitandao hii. Mrejesho wa papo kwa hapo unaowezeshwa na mitandao hii, unajenga utegemezi. Ni aina fulani ya ulevi.
Usikate tamaa unaposhindwa
Wakati mwingine tunashindwa kutekeleza malengo yetu kwa sababu tunakuwa wepesi kukataa tamaa mambo yanapokwenda vile tusivyotarajia. Tabia hii ya kughairi mambo kirahisi haiwezi kukusaidia kutekeleza mipango yako. Jifunze kuwa imara hata pale mambo yanapoharibika.
Ukitaka kusoma makala haya kwa urefu zaidi Soma hapa