Nawezaje kupenda na kufurahia kazi yangu?
Jiunge MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Login MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Umesahau password yako?. Andika email yako hapo chini alafu bonyeza 'Reset'. Utapokea link katika email yako kwa ajili ya kutengeneza password mpya.
Tafadhali elezea kwa nini unahisi chapisho hili linapaswa kuripotiwa
Salim Jumbe
Tafiti za ajira na kazi zinaonyesha kuwa mtazamo binafsi wa mfanyakazi una nafasi kubwa ya kumwongezea furaha ya kazi anayoifanya. Makala haya yanaangazia kanuni nne unazoweza kuzitumia kufurahia kazi unayofanya na hivyo kuongeza tija yako kazini.
Fahamu kinachokuridhisha
Hata hivyo, unapotambua kiwango chako cha kuridhika na kazi, unaweza kuchukua hatua stahiki. Si mara zote unapokosa msisimko wa kazi maana yake uache kazi. Wakati mwingine kubadili namna unavyoitazama kazi yako kunaweza kukusaidia. Kazi unayoona haina maana leo, wapo watu maelfu ambao pengine wanaota siku moja wangeipata. Labda huipendi kwa sababu ya namna unavyoitazama.
Jitambulishe na kazi yako
Ujasiri wa kujitambulisha na kazi yako ya sasa unakusaidia kuipenda zaidi kazi yako. Kufurahia kazi yako ya sasa haimaanishi usiwe na ndoto za kufanya kazi nyingine. Si watu wengi wanafanya kazi walizotamani kuzifanya.
Kuwa na bidii na ushirikiano
Heshima inayotokana na kazi ya mtu, kwa kawaida, inaongeza furaha ya kazi. Kule kujisikia kuwa mchango wako unatambuliwa, uwepo wako unahitajika, inakupa heshima. Lakini ili uweze kuheshimiwa kazini, unahitaji kujituma. Fanya kazi kwa bidii. Ione kazi yako kama njia halali ya kukusaidia kupata heshima unayohitaji kuwa nayo.
Rekebisha namna unavyoyachukulia maisha
Mtu asiye na furaha na maisha yake ya kawaida, anakuwa na uwezekano mdogo wa kufurahia kazi yake. Unapokuwa na utulivu na mtazamo chanya na maisha, inakuwa rahisi kwako kuipenda kazi yako. Kinyume chake pia ni kweli. Usipokuwa na furaha na maisha, hutafurahia kazi yoyote utakayopewa.
Soma kwa urefu HAPA