Nawezaje kununua domain name kwa ajili ya blog yangu?
Jiunge MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Login MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Umesahau password yako?. Andika email yako hapo chini alafu bonyeza 'Reset'. Utapokea link katika email yako kwa ajili ya kutengeneza password mpya.
Tafadhali elezea kwa nini unahisi chapisho hili linapaswa kuripotiwa
ChuiTec
Kununua domain name ni rahisi tu. Kuna vitu unapaswa kuwa navyo kabla ya kununua.
Kitu cha kwanza ni pesa ya kulipia kwa mwaka wa kwanza (kwa makadirio ni Tsh 30,000). Kingine ni njia ya kulipia, hapa unaweza tumia Master au Visa card au Njia za malipo za mtandao kama TigoPesa na MPesa.
Kingine unachotakiwa kufahamu ni jina yani domain name unayotaka kama lipo au la. Mfano unaweza kuwa unataka mojasky.com na ukakuta kuwa jina hilo limeshachukuliwa hivyo inatakiwa kuchagua jina jipya ambalo bado halijatumika.
Ukiwa tayari katika hayo hapo juu. Unaweza kufanya yafuatayo. Ingia Kilihost alafu bonyeza kwenye Choose Another Category alafu chagua Register Domain. Hapo utaweka jina unalotaka kununua, utachagua kama unahitaji .com .net au .co.tz. Utamalizia kwa kufata hatua zilizobaki kulipia jina unalohitaji.
Kufahamu sehemu nyingine za kupata domain name tembelea ChuiTec