Nawezaje kujua kua nina uwezo wa kuzalisha?
Jiunge MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Login MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Umesahau password yako?. Andika email yako hapo chini alafu bonyeza 'Reset'. Utapokea link katika email yako kwa ajili ya kutengeneza password mpya.
Tafadhali elezea kwa nini unahisi chapisho hili linapaswa kuripotiwa
Fred Moshi
Jamii yetu imekua ikiamini kuwa wanawake ndio huwa na matatizo, kwa hiyo ni hatua nzuri kwa mawanaume kujiuliza swali kama hili na kutafuta majibu yake.
Tutaliangalia swala hili kwa upande tofauti, namaanisha tutazitazama dalili zinazoweza kumpa mtu taarifa kwamba uwezo wake wa kuweza kusababisha ujauzito ni mdogo au anaweza asiwe nao kabisa. Maana yake ni kwamba kinyume chake kama hauna dalili hizi ni kwamba kuna uwezekano ukawa na uwezo wa kusababisha ujauzito.
Kutokuzalisha manii au kushindwa kufika kileleni. Hii huenda ikasababishwa na tatizo la uume kutokusimama kabisa. Kwa hiyo kama mwanaume anashindwa kabisa kuzalisha majimaji haya ambayo ndio yanakuwa na mbegu zinazoweza kumfanya mwanamke apate ujauzito, inamaana inaweza kuwa dalili ya kutokuweza kuzalisha
Mambo mengine ya kuangalia ni kama Maumivu, uvimbe au vidonda katika uume. Kuwa na korodani ndogo. Kukua kwa matiti kusiko kwa kawaida.
Pia kuna mambo ambayo yanaonekana kama hayana uhusiano wa moja kwa moja. Mambo yenyewe ni kama kutokuwa na uwezo wa kunusa, kuwa na matatizo ya mfumo wa upumuaji yanayojirudia mara kwa mara na kupungua kwa nywele katika mwili.
Kama unaona dalili au wasiwasi basi ni bora kufika hospitali mapema ili kugundua tatizo kabla halijawa kubwa zaidi
Kwa hiyo hizo ndo dalili. Ila ni vyema kujihakikishia afya bora ya uzazi kwa kubadilisha ‘lifestyle’ zetu, kula vyakula bora, kuondokana na msongo wa mawazo na kufanya mazoezi.