Jiunge

Jiunge MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection

Unayo account ? Log In

Unayo account ? Log in

Log In

Login MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection

Jiunge Hapa

Umesahau Password?

Hauna Account, Jiunge Hapa

Umesahau Password

Umesahau password yako?. Andika email yako hapo chini alafu bonyeza 'Reset'. Utapokea link katika email yako kwa ajili ya kutengeneza password mpya.

Unayo account ? Log in

Tafadhali andika jina lako kamili.

Tafadhali andika E-Mail yako.

Please choose an appropriate title for the question so it can be answered easily.

Tafadhali elezea kwa nini unahisi chapisho hili linapaswa kuripotiwa

Sign InSign Up

1Sky

1Sky

1Sky Navigation

  • Blog
  • Wasiliana Nasi
  • Advanced Search
  • App

Mobile menu

Close
Uliza Swali
  • Home
  • Maswali
  • Points
  • Miongozo
  • Wasiliana Nasi
  • Advanced Search
  • App
Home» Maswali»Q 31102
In Process
Adv
Anonymous
Asked: May 1, 20192019-05-01T09:33:08+03:00 2019-05-01T09:33:08+03:00Kilimo/Ufugaji

Nawezaje kujenga banda bora la kuku wa kienyeji?

Nawezaje kujenga banda bora la kuku wa kienyeji?
  • 1
  • 587
  • 0
  • Share
    • Share on WhatsApp
    • Share on Facebook
    • Share on Twitter
Jibu
  • Report
Adv

Jibu 1

  • Kura
  • Zamani
  • Mpya
  1. Anold Abu
    2020-05-12T10:55:26+03:00Jibu - May 12, 2020 saa 10:55 am

    Banda bora ni muhimu ili ufugaji wa kuku wa kienyeji uweze kuleta manufaa kwa mfugaji. Kuku huhitaji banda bora ili wasiathirike na madhara mbalimbali kama wezi, wanyama wakali, jua kali au mvua.

    1.SIFA ZA BANDA BORA LA KUKU

    Liwe na kuta, paa na sakafu imara. kuta na sakafu zisiwe na nyufa Liwe na sehemu ya kuku kutagia, kuatamia na sehemu ya kulea vifaranga. Liwe na vichanja kwa ajili ya kuku kupumzika na kulala. Liwe na nafasi ya kutosha kulingana na idadi ya kuku Liwe na uwezo wa kuingiza mwanga na hewa ya kutosha. Liwe na nafasi inayoruhusu mtu kuingia na kufanya usafi.

    2.SEHEMU INAYOFAA KUJENGA BANDA LA KUKU.
    Isiyokuwa na mteremko mkali. Isiyoruhusu maji kutuama. Iwe sehemu inayoruhusu hewa na mwanga wa kutosha. Ikiwezekana iwe sehemu yenye kivuli.

    3.AINA ZA MABANDA YA KUKU.
    Uchaguzi wa aina ya banda la kuku hutegemea mazingira. Kuku wanaofugwa kwenye mazingira ya joto wanahitaji banda lenye ukuta mfupi na sehemu kubwa ya uwazi wenye wavu hadi kufikia kwenye paa kulinganisha na sehemu zenye baridi ambapo,banda linahitaji kuwa na ukuta mrefu unaokaribia paa na sehemu ndogo tu,iliyo na uwazi wenye wavu ili kupitisha hewa na mwanga.vilevile eneo lenye matatizo kama ya majimaji au wanyama wanaoshambulia kuku inabidi kujenga aina ya banda lenye sakafu iliyonyanyuliwa juu.

    4.VIFAA VINAVYOTAKIWA KATIKA UJENZI WA BANDA.
    Vifaa vya kujengea banda vizingatie gharama na upatikanaji wake katika eneo husika.Vifaa hivyo vimepangwa katika makundi yafuatayo:

    1. Vifaa vya kujengea sakafu Sakafu la banda la kuku linaweza kujengwa kwa kutumia,saruji,udongo,mbao,mianzi au fito.

    2. Vifaa vya kujengea kuta kuta zinaweza kujengwa kwa kutumia , fito,udongo,matofali,mawe,mabati,mianzi,wavu,mabanzi au mbao.

    3. Vifaa vya kujengea paa. Paa la banda la kuku linaweza kuezekwa kwa kutumia nyasi, makuti, bati, migomba na vigae kulingana na uwezo wako.

    4. Vifaa vya kujengea wigo Wigo unaweza kujengwa kwa kutumia mbao,mianzi,matete,wavu,matofali,miti, au fito,mabanzi au mabati.

    UKUBWA WA BANDA LA KUKU KULINGANA NA IDADI YA KUKU
    Ukubwa wa banda la kuku unategemea na idadi ya kuku na aina ya kundi la kuku.Kuku wanaweza kugawanywa katika makundi mbalimbali kutegemea umri wao na madhumuni ya uzalishaji.

    •BANDA LA VIFARANGA WADOGO WA KUKU NA UKUBWA WAKE 

    (UKUBWA WA BANDA LA VIFARANGA WADOGO)
    Vifaranga wa siku moja hadi wiki nane Kundi hili la kuku wadogo hivyo wanahitaji eneo dogo la mita mraba 0.075 kkwa kuku mmoja,hivyo vifaranga 100 wanahitaji eneo la mita mraba saba na nusu (urefu wa mita 2.5 X na upana wa mita 3).

    •BANDA LA VIFARANGA WAKUBWA
    banda la vifaranga wa kuku wa wiki tisa hadi 20. Kuku mmoja wa umri huu anahitaji mita za mraba 0.15,hivyo kuku 100 wanahitaji mita za mraba 15 (urefu wa mita 5 X na upana wa mita

    •BANDA LA KUKU WAKUBWA
    Ili linajumlisha kuku wa wiki 21 na zaidi.Mara nyingi kundi hili ni la kuku waliopevuka (majogoo na majike wanaotaga) ambalo kuku mmoja huitaji mita mraba 0.2  hivyo kuku 100 huitaji mita za mraba 20 (urefu wa mita 5 X upana wa mita 4).

    •UKUBWA WA WIGO
    Mabanda yanayozungushiwa wigo kama ilivyo katika mfumo wa nusu huria ,kuku mmoja huhitaji eneo lenye ukubwa wa mita mraba 10 hivyo kuku 100 huhitaji eneo la mita za maraba 1000 (urefu wa mita 50 X upana wa mita 20). Kumbuka unaweza kupunguza vipimo lakini uwe mwangalifu na mahitaji ya kuku kwani kadri watakavyosongamana katika eneo dogo ndivyo watakavyohitaji uangalizi mkubwa zaidi

    imetoka kilimoboratz

    • 0
    • Reply
    • Share
      Share
      • Share on WhatsApp
      • Share on Facebook
      • Share on Twitter
      • Report
Jibu swali hili

Jibu swali hili
Cancel reply

Chagua
Captcha Click on image to update the captcha.

Adv

Sidebar

Uliza Swali

Promo

  • Usihangaike tena, Tumekuwekea Kampuni zote za kubet katika app moja! Jaribu Sasa

  • Beti kwa mara ya kwanza, ukishindwa unarudishiwa hela yako

  • Tafuta Ajira kiurahisi. Jaribu Sasa

  • Jifunze jinsi ya kubet kibingwa

  • Maswali yanayoendana

    • Mikonge hutumika kutengeneza nini?

    • Aina za buni ni zipi?

    • Karafuu ni nini?

    • Unaweza kunionesha ramani za mabanda ya kuku bora zaidi?

    Explore

    • Home
    • Maswali
    • Polls
    • Points
    • Watumiaji
    • Miongozo
    • App

    MojaSky | Designed by ChuiTec.

    Insert/edit link

    Enter the destination URL

    Or link to existing content

      No search term specified. Showing recent items. Search or use up and down arrow keys to select an item.