Nawezaje kufuta message niliyoituma WhatsApp?
Jiunge MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Login MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Umesahau password yako?. Andika email yako hapo chini alafu bonyeza 'Reset'. Utapokea link katika email yako kwa ajili ya kutengeneza password mpya.
Tafadhali elezea kwa nini unahisi chapisho hili linapaswa kuripotiwa
1sky
Mtandao maarufu wenye watumiaji wengi duniani unaojulikana kama Whatsapp siku za nyuma uliongeza chaguo linalokuwezesha kufuta ujumbe uliokwishautuma. Hii inaweza kukusaidia katika nyakati mbalimbali mfano kama ulikosea au usingependa uendelee kuonekana kwa mtu au kundi(group) ulilotuma.
Jinsi ya kufuta.
1.Ingia katika sehemu yenye ujumbe unaotaka kuufuta.
2.Shikilia kwa muda kdogo ujumbe unaotaka kuufuta mpaka uwe na kivuli(highlited).
3.Bonyeza alama ya kufuta inayoonekana upande wa juu.
4.Yatakuja machaguo matatu chagua DELETE FOR ME kama utataka ifutike kwako tu, chagua CANCEL kuahirisha au DELETE FOR EVERYONE ili kufuta kwako na kwa aliyetumiwa kama maneno yanavyojieleza katika lugha ya kiingereza.