Nawezaje kufunga tatizo la “unfortunately app has stopped”?
Pinned
Jiunge MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Login MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Umesahau password yako?. Andika email yako hapo chini alafu bonyeza 'Reset'. Utapokea link katika email yako kwa ajili ya kutengeneza password mpya.
Tafadhali elezea kwa nini unahisi chapisho hili linapaswa kuripotiwa
1sky
Umewahi kukutana na ujumbe unaosema unfortunately app has stopped?. Najua ni wengi mliokutana na hili tatizo la unfortunately app has stopped katika simu zenu za mkononi[smartphone]. Kwa kufuata njia kama zilivyoelekezwa hapo chini utakua umetibu tatizo hilo la simu.
Fungua
SETTINGS>APPLICATION MANAGER>ALL APPS>OPTIONS>RESET APP PREFERENCES. Baada ya kubonyeza kwa kufuata mfululizo ulioonekana hapo juu itatokea kama hivi. Bonyeza reset apps.
Baada ya kufungua kama ilivyo hapo juu utachagua iyo application iliyokua stopped kwa kuibonyeza itafunguka alafu utabonyeza CLEAR CACHE>CLEAR DATA. Hapo application yako iliyokua inasumbua itakaa vizuri na kurudi kama ilivyokua mwanzo. Baada kubonyeza kama inavyoonekana hapo juu kwa kuanza na clear cache alafu ikifatiwa na clear data itaonekana kama hapo chini kwenye picha. Kisha bonyeza OK.

KUMBUKA:Hakuna application itakayofutwa zote zinabaki sawa sawa.