Jiunge

Jiunge MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection

Unayo account ? Log In


Unayo account ? Log in

Log In

Login MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection

Jiunge Hapa


Umesahau Password?

Hauna Account, Jiunge Hapa

Umesahau Password

Umesahau password yako?. Andika email yako hapo chini alafu bonyeza 'Reset'. Utapokea link katika email yako kwa ajili ya kutengeneza password mpya.

Unayo account ? Log in

Tafadhali andika jina lako kamili.

Tafadhali andika E-Mail yako.

Please choose an appropriate title for the question so it can be answered easily.


Tafadhali elezea kwa nini unahisi chapisho hili linapaswa kuripotiwa

Sign InSign Up

1Sky

1Sky

1Sky Navigation

  • Blog
  • Wasiliana Nasi
  • Advanced Search
  • App

Mobile menu

Close
Uliza Swali
  • Home
  • Maswali
  • Points
  • Miongozo
  • Wasiliana Nasi
  • Advanced Search
  • App
Home» Maswali»Q 34740
In Process
Anonymous
Asked: January 19, 20202020-01-19T11:31:54+03:00 2020-01-19T11:31:54+03:00Kazi/Ajira

Nawezaje kufanya vizuri katika maswali ya interview ya kazi?

Nawezaje kufanya vizuri katika maswali ya interview ya kazi?
  • 1
  • 518
  • 0
  • Share
    • Share on WhatsApp
    • Share on Facebook
    • Share on Twitter
Jibu
  • Report

Jibu 1

  • Kura
  • Zamani
  • Mpya
  1. Salim Jumbe

    Salim Jumbe

    • Dar es Salaam, Tanzania
    • 0 Questions
    • 132 Answers
    • 0 Best Answers
    • 474 Points
    View Profile
    Salim Jumbe Proffesional
    2020-01-19T11:39:31+03:00Jibu - January 19, 2020 saa 11:39 am
    Jibu hili limerekebishwa.

    Vijana wengi wenye ufaulu mzuri wanaoomba kazi, hujikuta pasipokujua, wakifanya makosa madogo yanayowagharimu. Kwa kuwa umetumia muda wako kuandika barua, kuandika wasifu wako wa kazi, wakati mwingine kusafiri kwenda kuhudhuria usaili, ni muhimu kufanya maandalizi yatakayokuongezea nafasi ya kufanikiwa.
    Katika makala haya, tutaangazia baadhi ya maswali yanayoulizwa kwenye usaili wa kazi na namna unavyoweza kuyajibu.

    Mapokezi
    Unapokaribishwa kwenye usaili, jambo la kwanza ni kuhakikisha kuwa unatengeneza taswira ya mtu anayejitambua, mkomavu na mwenye nidhamu. Salimia jopo linalokupokea kwa tabasamu na salamu ya adabu yenye kuonesha kujiamini. Ikiwa ni lazima kushikana mikono na wanajopo, fanya hivyo kwa kujiamini.
    Unapojibu maswali, epuka kutikisa kichwa. Kukunja nne, kuegemea nyuma, au kuweka mikono kwa namna inayoonesha mamlaka, ni kutuma ujumbe hasi usiokusudiwa.

    Utambulisho
    Kumbuka kuwa usaili wako ulianza tangu jopo la usaili lilipopokea nyaraka zako. Kwa kiasi fulani, tayari wanayo taswira fulani kukuhusu. Una kazi muhimu ya kuwathibitishia kuwa hayo uliyoyaandika yana ukweli.
    Mara nyingi unapokaribishwa kwenye usaili, kiongozi wa jopo la usaili, atawatambulisha kwa wenzake. Anapofanya hivyo, ana lengo la kukufanya uwazoee wanajopo, utulie na usiwe na wasiwasi. Shukuru kwa utambulisho wao.
    Kiongozi huyo anaweza kukutambulisha wewe kwa jina lako na kukaribisha maswali. Mara nyingi swali linaloanza ni, ‘Tuambiwe wewe ni nani?’ ‘Karibu ujitambulishe…’
    Swali kama hili halihitaji utaje majina yako bali kufahamu mhutasari wako kikazi. Ingawa utakayoyasema yatatokana na uliyoyaandika kwenye wasifu wako wa kazi, mara nyingi hautarajiwi kurudia maelezo hayo.

    Ari na uwezo wako wa kazi
    Unaweza kuulizwa, ‘Kwa nini  unafikiri tukuchukue kwa nafasi hii?’, ‘Kwa nini unataka kufanya kazi na sisi?’ Watu wengi wanapoulizwa swali hili hufikiri wanachohitaji ni kujilinganisha na wengine kwa majina. Huna sababu ya kuwataja wengine kama namna ya kuonesha unavyofaa zaidi.
    Kwa swali kama hilo, kimsingi wanataka kuona kama unaielewa taasisi yao. Thibitisha kuwa umeitafiti taasisi kwa kina, na una uelewa wa huduma wanazotoa. Onesha unavyojisikia kuwa sehemu ya malengo mapana ya taasisi yao.

    Uzoefu wako huko ulikotoka
    Unaweza kuulizwa maswali mengi kuhusu uzoefu wako kazini. Ikiwa kwenye wasifu wako wa kazi ulionesha kuwa uliwahi kufanya kazi mahali na ukaiacha, unaweza kuulizwa swali, ‘Kwa nini uliacha kazi yako?’ au ‘Kwa nini unataka kuacha kazi uliyonayo?’
    Hili ni swali gumu. Mwuulizaji analenga kupima uaminifu wako na anataka kujua mambo gani hasa yanakuridhisha kazini. Kimsingi lengo sio kujua yaliyofanyika huko uliko (kuwa) bali kujua unavyoweza kumfaa. Hutakiwi kuzunguka kwa kutafuta sababu zisizo za kweli. Jibu kwa urahisi na uwazi lakini ukiwa makini.

    Matarajio yako kwa mwajiri
    ‘Unadhani tukulipe mshahara kiasi gani?’
    Hili swali linatafuta kujua vipaumbele vyako uwapo kazini. Ni kweli unatafuta kazi ili upate fedha uboreshe maisha yako. Lakini kuonesha kuwa ari na kujituma kwako kazini kunategemea na kiasi cha pesa unacholipwa ni kosa la kiufundi. Kosa hili linaweza kuwa kikwazo cha kukupa kazi.
    Unahitaji kuonesha ukomavu kwa kuelewa kuwa taasisi bora [kama hiyo unayotaka ikuajiri] zina utaratibu rasmi wa kuwalipa wafanyakazi wake. Mtu hulipwa kwa sifa alizonazo. Kwa uelewa huo, utapata alama za ziada.

    Uelewa wa mambo na ujuzi wa kazi
    Unaweza kuulizwa maswali yanayopima uelewa wako wa kawaida kwa mambo yanayofahamika. Lakini pia unaweza kuulizwa masuala ya moja kwa moja yanayohusiana na kazi unayoomba.
    Wakati mwingine, baadhi ya wasaili hutumia mtihani wa kuandika kujaribu kuthibitisha kama kweli una uwezo na ujuzi uliouonesha kwenye wasifu wa kazi.

    Malengo yako ya baadae
    ‘Unajiona ukifanya nini baada ya miaka 10 ijayo?’
    ‘Una malengo gani ndani ya miaka mitano ijayo?’
    Hapa unahitajika kuonesha ari ya kukua kiujuzi na kiweledi. Ongelea mipango ya kujifunza zaidi kufikia kwenye malengo makubwa yanayoendana na malengo mapana ya kitaasisi. Kuzungumzia malengo yasiyoendana na kazi unayoomba kutakupunguzia alama.
    ‘Umeomba kazi kwingine?’
    Wanahitaji kuwa na uhakika na maamuzi yako. Ni kweli inawezekana utakuwa umeomba kazi maeneo mengine. Lakini utaonekana mkomavu ukiweza kuonesha kuwa kazi hii unayosailiwa ndio chaguo la kwanza.
    ‘Utafanya kazi na sisi kwa muda gani?’
    Hapa wanataka kujua kama wewe ni mpitaji au la. Inawezekana kweli unaweza kuwa na mpango wa kufanya kazi kwa muda mfupi na utafute njia nyingine.
    Lakini kuonesha wazi kuwa unapita wakati hata kazi hujapata si busara. Onesha ungependa kufanya kazi kwa muda mrefu kadri utakavyohitajika.
    ‘Unaota kufanya kazi gani nzuri baadae?’
    Ukitaja kazi nyingine mbali na hiyo unayoomba, unaleta wasiwasi kuwa hutaridhika na kazi unayoomba. Ongelea mazingira ya kazi bila kutaja kazi mahususi. Mfano, kazi inayokufanya utumie vipaji vyako na ujuzi ulionao. Kazi inayokufanya ukue kiujuzi na kiuzoefu.

    Fursa ya kuuliza swali
    Kwa kawaida, baada ya kuulizwa maswali mengi,  kikao cha usaili kitahitimishwa kwa kukukaribisha kuuliza swali. Kama tulivyosema, kila swali lina maana. Unapoulizwa, ‘Je, una swali ungependa kuuliza?’ lengo ni kutaka kujua ulivyo na ari ya kufanya kazi na taasisi hiyo
    Usipouliza swali lolote, maana yake ama huna uelewa wa mambo mengi au huna ari ya kutosha. Uliza swali kuhusu taasisi hiyo. Waliuze wanatarajia nini kwa mtu atakaye pata kazi hiyo. Kadhalika, waweza kuulizia mambo yanayohusiana na fursa wanazoweza kutoa kukuza ujuzi wako kama mfanyakazi wao.
    Izo ni baadhi ya Aya tu Kwa urefu zaidi soma Hapa

    • 0
    • Reply
    • Share
      Share
      • Share on WhatsApp
      • Share on Facebook
      • Share on Twitter
      • Report
Jibu swali hili

Jibu swali hili
Cancel reply

Chagua

Sidebar

Promo

  • Smartphone mpya ya Samsung kwa Tsh 220,000 Tu

  • Nafasi zote mpya za kazi zipo hapa

  • Tafuta vitu mtandaoni kwa lugha ya Kiswahili

  • Tafuta Ajira kiurahisi. Jaribu Sasa

  • Maswali Mengine

    • Nawezaje kupenda na kufurahia kazi yangu?

      • Jibu 1
    • Mambo gani ya kufanya wakati wa kutafuta kazi?

      • Jibu 1
    • Kuna faida gani katika kujitolea?

      • Jibu 1
    • Mambo gani ya kuzingatia katika barua ya kuomba kazi?

      • Jibu 1
    • Mambo gani ya kuzingatia katika kuomba kazi serikalini kwa njia ya mtandao?

      • Jibu 1
    • Kozi zinazotambuliwa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) ni zipi?

      • Jibu 1
    • Ni masharti na vigezo gani vya kujiunga na mitihani ya Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania ...

      • Jibu 1
    • Ni mitihani gani inayoendeshwa na NBAA?

      • Jibu 1
    • Masharti ya kujiunga kufanya mitihani ya ATEC I ni yapi?

      • Jibu 1
    • Je nikiwa sina masomo matatu niliyofaulu vizuri (credit) katika elimu ya Sekondari, lakini napenda kujiunga katika fani ya uhasibu, nifanye ...

      • Jibu 1

    Explore

    • Home
    • Maswali
    • Polls
    • Points
    • Watumiaji
    • Miongozo
    • App

    MojaSky

    Insert/edit link

    Enter the destination URL

    Or link to existing content

      No search term specified. Showing recent items. Search or use up and down arrow keys to select an item.