Nataka kujua jinsi ya kutengeneza app nifanyeje?
Jiunge MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Login MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Umesahau password yako?. Andika email yako hapo chini alafu bonyeza 'Reset'. Utapokea link katika email yako kwa ajili ya kutengeneza password mpya.
Tafadhali elezea kwa nini unahisi chapisho hili linapaswa kuripotiwa
Calvin Mlay
Nitakisia kwamba app unayotaka kutengeneza ni ya simu ya Android mfano ni app zinazopatikana Google Play Store.
Apps huwa zinatengenezwa kwa kutumia lugha za kompyuta(programming languages) ili kutengeneza app hizo kwa njia inayotumika zaidi inabidi ujue lugha ya kutengenezea app hiyo, mfano apps za Android zinatumia lugha ya Java kwa kutumia programu maalumu ya kompyuta inayojulikana kama Android Studio(japo zipo nyingine pia). Kwa hiyo ili uweze kutengeneza app inabidi ujifunze kwanza kuprogram kwa kutumia lugha husika.
Pia kama utapenda kutengeneza bila kujifunza kuprogram au kumuajiri mtu unaweza kutumia app builders zitakazokuwezesha kutengeneza app bila kuwa na ujuzi wowote
Mfano wa hizo app builders ni
AppCreator24
Appery.io
Appy Pie
AppMachine
AppMakr
Ila kwa njia hii ili kutengeneza app ya maana mfano kwa ajili ya biashara yako itakubidi utumie zaidi pesa ukilinganisha na njia ya ku program mwenyewe.