Kama umewahi kujaza fomu mbalimbali mtandaoni unaweza kuwa ulikukutana na sehemu inayokutaka kujaza zip code au postal code hususa ni shughuli zinazohitaji malipo mtandaoni kama kununua ‘domain name’ na baadhi ya huduma za kusajili akaunti za email.

Zip/Postal Codes ni nini?

ZIP(Zonal Improvement Plan) code ni mfumo wa posta wa kutambua maeneo kwa kutumia fomati ya namba(tarakimu) tano(5) Tanzania mfumo huo haujaanza kutumika rasmi licha ya mpango kuwa tayari na kuwepo kwa zip/postal kodi hizo.

Zip/Postal Code ya eneo lako

Kwa sasa kodi za maeneo yote zinapatikana katika tovuti ya TCRA. Mfano kodi ya Kivukoni mkoani Dar es salaam ni 11101 kama inavyoonekana katika picha hapo juu. Kutafuta zip kodi ya eneo lako bonyeza >HAPA Pia unaweza kudownload pdf yenye maeneo yote ya Tanzania na posti kodi zake  >HAPA