Jiunge

Jiunge MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection

Unayo account ? Log In

Unayo account ? Log in

Log In

Login MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection

Jiunge Hapa

Umesahau Password?

Hauna Account, Jiunge Hapa

Umesahau Password

Umesahau password yako?. Andika email yako hapo chini alafu bonyeza 'Reset'. Utapokea link katika email yako kwa ajili ya kutengeneza password mpya.

Unayo account ? Log in

Tafadhali andika jina lako kamili.

Tafadhali andika E-Mail yako.

Please choose an appropriate title for the question so it can be answered easily.

Tafadhali elezea kwa nini unahisi chapisho hili linapaswa kuripotiwa

Sign InSign Up

1Sky

1Sky

1Sky Navigation

  • Blog
  • Wasiliana Nasi
  • Advanced Search
  • App

Mobile menu

Close
Uliza Swali
  • Home
  • Maswali
  • Points
  • Miongozo
  • Wasiliana Nasi
  • Advanced Search
  • App
Home» Maswali»Q 32669
In Process
Adv
Mhina m mkota
Asked: July 7, 20192019-07-07T17:54:59+03:00 2019-07-07T17:54:59+03:00Mapenzi

Mwanamke asie kua na upendo nitamjuaje

Mwanamke asie kua na upendo nitamjuaje
  • 1
  • 500
  • 0
  • Share
    • Share on WhatsApp
    • Share on Facebook
    • Share on Twitter
Jibu
  • Report
Adv

Jibu 1

  • Kura
  • Zamani
  • Mpya
  1. Jose Mandingo

    Jose Mandingo

    • Dar es Salaam, Tanzania
    • 0 Questions
    • 33 Answers
    • 0 Best Answers
    • 169 Points
    View Profile
    Jose Mandingo Advanced
    2019-07-24T06:51:45+03:00Jibu - July 24, 2019 saa 6:51 am

    Baadhi ni kama zifuatazo

    1 : Hataki kuambata na wewe katika matembezi na ikitokea anakuwa mtu wa masharti mara akuambie tangulia nakuja au pengine kutembea nawe kwa umbali.

    2 : Anapata kigugumizi kukutambulisha kwa rafiki zake na ndugu na inapotokea amebanwa hafikishi ujumbe kwa kiwango timilifu.

    3 : Haoneshi kubana matumizi kwa ajili ya maendeleao, kwake ni kufuja mali na anapokosa kupewa pesa ni mwepesi kulalamika na wakati mwingine kununa kabisa.

    4 : Anaahirisha mara kwa mara kukutana na wewe tena bila kukueleza sababu za msingi Au kukutungia uongo wa dhahili na kuusisitiza bila kuona aibu.

    5 : Anapokuwa akitoa maelezo ya mwanaume amtakaye sifa zake zinakuwa hayalingani na wewe. Anaweza kukuambia napenda kuishi na mwanaume mwenye gari au mwenye mwili mkubwa, sifa ambazo wewe huna!

    6 : Hacheki kwa furaha hata kama ukimchekesha haoneshi furaha ya moyoni. Tena mara nyingine anakuwa mkimya na mshiwishi mkubwa wa kuachana kutoka kwenye matembezi yenu ya jioni. “Aaah, mi nimechoka narudi nyumbani”

    7 : Anajaribu kukuunganisha na wanawake wengine na haoni vibaya anaposikia unamfukuzia mwingine badala yake anakutia moyo wa kuendelea na usaliti wako. Hana wivu kabisa.

    8 : Hajuti anapokukosea, mwepesi wa kujitenga, kutokuzungumza nawe na mwingi wa kukusukumia makosa hata kama yeye ndiye aliyekukosea.

    9 : Msambazaji wa habari za udhaifu wako na mtu asiyekusifia mbele za wenzake. Si balozi mwema kwa familia yake, haishi kukuponda mbele ya wazazi na ndugu zake.

    10 : Mwepesi wa kupokea na si wa kutoa mmiliki wa mali zako na mkumbatiaji wa mali zake pia. Msiri wa mipango yake na mtu anayependa kujua zaidi ya kwako kuliko wewe kujua yake.

    11: Hathamini uwepo wako na anakuchukulia kama mtu wa akiba. Hakumiss unapokuwa haupo, hahisi upweke wala hakukumbuki unapokuwa mbali naye.

    12 : Hakutii moyo unaposhindwa na mara nyingine hauzuniki nawe unapokuwa una shida,. Hachukui huzuni yako kama yake, hakufariji na hakusaidii kutatua kilichokwama.

    13 : Mhamasishaji wa uasi hasa wa watoto na ndugu, anayeweza kuchochea hisia za jamii ikuone mbaya, kukudharau na wakati mwingine ikutenge. Mwenezaji wa sifa zako mbaya.

    14 : Hakupi kipaumbele katika maamuzi, anajiona yeye ndiye wa kwanza na wewe ni mtu wa kufuata hata unapopinga hasitishi dhamira yake ya kutenda.

    15 : Humsisimui katika mambo ya faragha, anakuchukulia kama ndugu yake.

    16 : Hakuhudumii tendo la ndoa mpaka siku amependa mwenyewe. Ni mwingi wa sababu za kuchoka kusingizia ugonjwa na mwenye kuhisi kero ya kucheza nawe mchezo wa kikubwa.

    17 : Hazungumzii maendeleo yenu, mwepesi wa kushawishi ilivyopatikana viuzwe ili atimize hitaji lake. “Niuze simu yangu niende kuwaona wazazi, maana kuna sherehe ya motto huko!”

    18 : Hataki kuambiwa ukweli na anapotokea akaambiwa anajitetea kwa kumtaja mwanaume mwingine. “Mbona Shabani (si jina halisi) anamfanyia hili, hamfanyii hivi mkewe”

    19 : Hasamehe na kusahau. Kosa la mwaka juzi analijengea hoja.

    20 : Mwepesi wa kutoa kauli za kutengana na asiyeogopa kuachwa. “Kama vipi kila mtu akae kivyake maana naona unaniboa tu, unadhani nitashindwa kuishi bila wewe”

    nimeitoa jamiiforums

    • 0
    • Reply
    • Share
      Share
      • Share on WhatsApp
      • Share on Facebook
      • Share on Twitter
      • Report
Jibu swali hili

Jibu swali hili
Cancel reply

Chagua
Captcha Click on image to update the captcha.

Adv

Sidebar

Uliza Swali

Promo

  • Usihangaike tena, Tumekuwekea Kampuni zote za kubet katika app moja! Jaribu Sasa

  • Beti kwa mara ya kwanza, ukishindwa unarudishiwa hela yako

  • Tafuta Ajira kiurahisi. Jaribu Sasa

  • Jifunze jinsi ya kubet kibingwa

  • Maswali yanayoendana

    • Nawezaje kuzipata sms za mke wangu katika simu yangu ambazo zinatumwa na watu wake?

    • Nimfanyie nini mwanamke ili anipende?

    • Wanaume wanahitaji nini katika mahusiano?

    • Nawezaje kutokuwa na wivu kwa mpenzi wangu?

    • Aina gani za wanaume wa kuepuka katika mahusiano?

    • Sifa za mwanamke anayefaa kuolewa ni zipi?

    Explore

    • Home
    • Maswali
    • Polls
    • Points
    • Watumiaji
    • Miongozo
    • App

    MojaSky | Designed by ChuiTec.

    Insert/edit link

    Enter the destination URL

    Or link to existing content

      No search term specified. Showing recent items. Search or use up and down arrow keys to select an item.