Masharti ya TRA yakoje katika kuanzisha biashara?
Jiunge MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Login MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Umesahau password yako?. Andika email yako hapo chini alafu bonyeza 'Reset'. Utapokea link katika email yako kwa ajili ya kutengeneza password mpya.
Tafadhali elezea kwa nini unahisi chapisho hili linapaswa kuripotiwa
Salim Jumbe
Kupitia tovuti yao wameandika hivi
Mtu Binafsi
Mtu binafsi awe mkazi au si mkazi anatakiwa kutembelea ofisi ya TRA ya mkoa au wilaya na kujaza fomu ya maombi ya Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN). Maombi yanaweza kufanywa pia kwa njia ya mtandao, hata hivyo mwombaji lazima afike ofisi za TRA kwa ajili ya kuchukuliwa alama za vidole pamoja na kupiga picha na kuweka saini.
Baada ya kupata cheti cha namba ya utambulisho wa mlipakodi mwombaji atatakiwa kuomba leseni ya biashara kutoka ofisi za Biashara katika Wilaya, Manispaa, Jiji na Wizara ya Biashara na Viwanda kwa kutegemea aina ya biashara anayotaka kuanzisha.
Hati ya Usajili:
Mtu binafsi anaweza kuamua kusajili jina la biashara kwa wakala aliyepewa kazi hiyo na Wizara ya Biashara na Viwanda anayejulikana kama Mamlaka ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA). Jina lililosajiliwa linaweza kupatikana kabla au baada ya kutoa maombi ya TIN. Jina la biashara lililosajiliwa litaonyeshwa kwenye hati ya TIN pamoja na jina la mtu huyo ikionyesha jina la mmiliki wa biashara kama (T/A).
Shirika (kampuni yenye dhima ya ukomo)
Kuanzisha shirika kunahitaji mtu aombe kupatiwa Hati ya shirika kutoka Mamlaka ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA). Wahamasishaji wa kampuni wanatakiwa kuandaa na kuwasilisha hati na Mkataba na kanuni za kampuni.
Hati ya usajili wa shirika iambatishwe kwenye maombi ya TIN pamoja na Mkataba na Kanuni za Kampuni wakati mtu anapopeleka maombi TRA.
Kampuni yenye dhima ya ukomo itaomba kupatiwa hati ya TIN kwa kujaza fomu za maombi kama ifuatavyo:
Ubia
Wabia wanatakiwa kusajili kampuni katika ofisi za BRELA na kupata hati ya usajili ambayo inaonyesha namba na majina ya wabia pamoja na mgawanyo wa hisa zao.
Udhamini
Udhamini ni mpango ambapo wadhamini wanamiliki mali lakini haihusishi ubia na kampuni.
Amana inapaswa kusajiliwa kama kampuni katika ofisi za BRELA na kupata hati ya usajili ambayo inaonesha majina na anwani za wadhamini. Kila mdhamini anapaswa kuomba kupatiwa hati ya TIN, iwapo mdhamini yeyote kati yao akiwa ameshapatiwa hati ya TIN kwa madhumuni mengine hawezi kutuma maombi mengine. Namba ya TIN aliyo nayo itatumika.
Shirika la msaada:
Shirika hili litatambulika kama shirika la msaada kwa madhumuni ya masuala ya kodi baada ya kupatiwa kibali na Kamishna Mkuu. Mwombaji anatakiwa kupata nyaraka zote muhimu kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani.
Tamko la Makadirio ya Mapato
Utatakiwa kutoa tamko la makadirio ya mapato kwa ajili ya kufanyiwa makadirio ya awali ya kodi kwa mwaka husika. Afisa wa kodi anaweza kukuhoji na kurekodi taarifa za biashara yako na taarifa zako binafsi katika ofisi ya TRA.