Jiunge

Jiunge MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection

Unayo account ? Log In


Unayo account ? Log in

Log In

Login MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection

Jiunge Hapa


Umesahau Password?

Hauna Account, Jiunge Hapa

Umesahau Password

Umesahau password yako?. Andika email yako hapo chini alafu bonyeza 'Reset'. Utapokea link katika email yako kwa ajili ya kutengeneza password mpya.

Unayo account ? Log in

Tafadhali andika jina lako kamili.

Tafadhali andika E-Mail yako.

Please choose an appropriate title for the question so it can be answered easily.


Tafadhali elezea kwa nini unahisi chapisho hili linapaswa kuripotiwa

Sign InSign Up

1Sky

1Sky

1Sky Navigation

  • Blog
  • Wasiliana Nasi
  • Advanced Search
  • App

Mobile menu

Close
Uliza Swali
  • Home
  • Maswali
  • Points
  • Miongozo
  • Wasiliana Nasi
  • Advanced Search
  • App
Home» Maswali»Q 34477
In Process
Anonymous
Asked: January 10, 20202020-01-10T08:12:05+03:00 2020-01-10T08:12:05+03:00Biashara/Ujasiriamali, TRA

Masharti ya TRA yakoje katika kuanzisha biashara?

Masharti ya TRA yakoje katika kuanzisha biashara?
  • 1
  • 237
  • 0
  • Share
    • Share on WhatsApp
    • Share on Facebook
    • Share on Twitter
Jibu
  • Report

Jibu 1

  • Kura
  • Zamani
  • Mpya
  1. Salim Jumbe

    Salim Jumbe

    • Dar es Salaam, Tanzania
    • 0 Questions
    • 132 Answers
    • 0 Best Answers
    • 473 Points
    View Profile
    Salim Jumbe Proffesional
    2020-01-10T08:15:53+03:00Jibu - January 10, 2020 saa 8:15 am

    Kupitia tovuti yao wameandika hivi

    Mtu Binafsi

    Mtu binafsi awe mkazi au si mkazi anatakiwa kutembelea ofisi ya TRA ya mkoa au wilaya na kujaza fomu ya maombi ya Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN). Maombi yanaweza kufanywa pia kwa njia ya mtandao, hata hivyo mwombaji lazima afike ofisi za TRA kwa ajili ya kuchukuliwa alama za vidole pamoja na kupiga picha na kuweka saini.

    Baada ya kupata cheti cha namba ya utambulisho wa mlipakodi mwombaji atatakiwa kuomba leseni ya biashara kutoka ofisi za Biashara katika Wilaya, Manispaa, Jiji na Wizara ya Biashara na Viwanda kwa kutegemea aina ya biashara anayotaka kuanzisha.

     

    Hati ya Usajili:

    Mtu binafsi anaweza kuamua kusajili jina la biashara kwa wakala aliyepewa kazi hiyo na Wizara ya Biashara na Viwanda anayejulikana kama Mamlaka ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA). Jina lililosajiliwa linaweza kupatikana kabla au baada ya kutoa maombi ya TIN. Jina la biashara lililosajiliwa litaonyeshwa kwenye hati ya TIN pamoja na jina la mtu huyo ikionyesha jina la mmiliki wa biashara kama (T/A).

     

    Shirika (kampuni yenye dhima ya ukomo)

    Kuanzisha shirika kunahitaji mtu aombe kupatiwa Hati ya shirika kutoka Mamlaka ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA). Wahamasishaji wa kampuni wanatakiwa kuandaa na kuwasilisha hati  na Mkataba na kanuni za kampuni.

    Hati ya usajili wa shirika iambatishwe kwenye maombi ya TIN pamoja na Mkataba na Kanuni za Kampuni wakati mtu anapopeleka maombi TRA.

     

    Kampuni yenye dhima ya ukomo itaomba kupatiwa hati ya TIN kwa kujaza fomu za maombi kama ifuatavyo:

    • Maombi kwa ajili ya kampuni.
    • Maombi kwa ajili ya wanahisa/wakurugenzi, iwapo mkurugenzi yeyote kati yao ameshapatiwa hati ya TIN kwa madhumuni mengine anaweza kutoa maombi mengine. Namba ileile ya TIN itatumika.
    • Kwa wakurugenzi ambao si raia wanapaswa kutimiza masharti yote ya uhamiaji na kupata kibali cha biashara kutoka Idara ya Uhamiaji inayofanya kazi chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani.

     

         Ubia

    Wabia wanatakiwa kusajili kampuni katika ofisi za BRELA na kupata hati ya usajili ambayo inaonyesha namba na majina ya wabia pamoja na mgawanyo wa hisa zao.

    • Katika kutoa maombi ya TIN kampuni ya ubia itaomba kupatiwa hati kwa kuwasilisha nakala ya usajili waliyopata BRELA.
    • Kila mbia ataomba kupatiwa TIN, iwapo mbia yeyote tayari ameshapatiwa hati ya TIN kwa madhumuni mengine hatakiwi kutoa maombi mengine. Namba ileile ya TIN itatumika.

     

     Udhamini

    Udhamini ni mpango ambapo wadhamini wanamiliki mali lakini haihusishi ubia na kampuni.

    Amana inapaswa kusajiliwa kama kampuni katika ofisi za BRELA na kupata hati ya usajili ambayo inaonesha majina na anwani za wadhamini. Kila mdhamini anapaswa kuomba kupatiwa hati ya TIN, iwapo mdhamini yeyote kati yao akiwa ameshapatiwa hati ya TIN kwa madhumuni mengine hawezi kutuma maombi mengine. Namba ya TIN aliyo nayo itatumika.

     

    Shirika la msaada:

    Shirika hili litatambulika kama shirika la msaada kwa madhumuni ya masuala ya kodi baada ya kupatiwa kibali na Kamishna Mkuu. Mwombaji anatakiwa kupata nyaraka zote muhimu kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani.

     

    Tamko la Makadirio ya Mapato

    Utatakiwa kutoa tamko la makadirio ya mapato kwa ajili ya kufanyiwa makadirio  ya awali ya kodi kwa mwaka husika. Afisa wa kodi anaweza kukuhoji na kurekodi taarifa za biashara yako na taarifa zako binafsi katika ofisi ya TRA.

    • 0
    • Reply
    • Share
      Share
      • Share on WhatsApp
      • Share on Facebook
      • Share on Twitter
      • Report
Jibu swali hili

Jibu swali hili
Cancel reply

Chagua

Sidebar

Promo

  • Smartphone mpya ya Samsung kwa Tsh 220,000 Tu

  • Nafasi zote mpya za kazi zipo hapa

  • Tafuta vitu mtandaoni kwa lugha ya Kiswahili

  • Tafuta Ajira kiurahisi. Jaribu Sasa

  • Maswali Mengine

    • VAT Tanzania ni asilimia ngapi?

      • Majibu 2
    • Masharti ya kuanzisha duka la dawa yakoje?

      • Jibu 1
    • Taratibu za kiserikali za kuzingatia kabla ya kuanzisha redio au TV Tanzania ukoje?

      • Jibu 1
    • Nitaanza vipi kama sina mtaji wowote?

      • Jibu 1
    • Nawezaje kupata TIN kwa ajili ya biashara yangu?

      • Jibu 1
    • TIN namba ni nini?

      • Jibu 1
    • Nawezaje kutengeneza shampoo nikiwa nyumbani?

      • Jibu 1
    • Viwango vya kodi ya VAT vikoje?

      • Jibu 1
    • Kodi ya ongezeko la thamani(VAT) inatozwaje?

      • Jibu 1
    • Nini maana ya hisa?

      • Jibu 1

    Explore

    • Home
    • Maswali
    • Polls
    • Points
    • Watumiaji
    • Miongozo
    • App

    MojaSky

    Insert/edit link

    Enter the destination URL

    Or link to existing content

      No search term specified. Showing recent items. Search or use up and down arrow keys to select an item.