Mambo gani ya kufanya wakati wa kutafuta kazi?
Jiunge MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Login MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Umesahau password yako?. Andika email yako hapo chini alafu bonyeza 'Reset'. Utapokea link katika email yako kwa ajili ya kutengeneza password mpya.
Please briefly explain why you feel this question should be reported.
Tafadhali elezea kwa nini unahisi chapisho hili linapaswa kuripotiwa
Please briefly explain why you feel this user should be reported.
Kumbuka haya mambo
Jenga utambulisho wako
Utambulisho wako ni kama kutangaza bidhaa uliyonayo sokoni. Kwa wewe unayetafuta kazi, bidhaa yako ni ujuzi ulionao, maarifa na fikra zinazokutambulisha kwa wengine. Ni muhimu sana kutafuta mazingira ya kutangaza bidhaa yako.
Fahamu zinakopatikana taarifa za ajira
Unalazimika kufuatilia kwa karibu vyanzo mbalimbali vya habari kupata taarifa za ajira. Zipo tovuti maalum zilizoandaliwa na watu na taasisi binafsi kwa minajili ya kusambaza habari za kazi. Serikali nayo, kwa mfano, inao ukurasa maalum uitwao http://portal.ajira.go.tz/ kukusaidia kupata taarifa za nafasi za kazi serikalini kila zinapotolewa.
Tengeneza mtandao
Mara nyingi tunatarajia kuwa nafasi za kazi hutangazwa. Lakini wakati mwingine kazi nyingi hasa katika sekta binafsi huwa hazitangazwi wazi wazi. Sababu ni kuwa waajiri wengi wana tabia ya kutafuta watu wanaoaminika, na wakati mwingine kwa kuelekezwa na watu wanaoeleweka.
Jitolee kufanya kazi bila malipo
Tumia muda wako wa mpito kujitengenezea uzoefu unaohitajika bila ajira rasmi. Jitolee kufanya kazi bila malipo. Tafuta taasisi zinazotoa huduma zinazolingana na ujuzi wako. Onesha nia ya kutafuta uzoefu. Kufanya hivyo kutakusaidia kuboresha taarifa zako za uzoefu, na hivyo kukuongezea sifa za kuajirika.
Andaa nyaraka zako vizuri
Vile vile, ni muhimu kuandaa barua za maombi kwa kila kazi utakayoomba. Kwa kawaida, barua ya kazi hubadilika badilika kuendana na mahitaji mahususi ya tangazo la kazi inayoombwa. Nyaraka zote hizi ni vyema kuandaliwa mapema ili iwe rahisi kuzirekebisha kukidhi mahitaji ya kazi inayombwa.
Punguza matarajio, usikate tamaa
Kuwa na matajirio ya kupata kazi nzuri yenye heshima ni jambo jema. Ndoto ni muhimu. Lakini, wakati mwingine, waweza kuanza na kidogo kinachopatikana kikuwezeshe kupata unachokilenga. Katika mazingira yenye ushindani mkubwa wa ajira, si busara kuchagua sana kazi.
Hii imeandikwa kwa ufupi, ukitaka kusoma kwa urefu zaidi tembelea hapa