Mafuta gani ni mazuri zaidi kupikia?
Jiunge MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Login MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Umesahau password yako?. Andika email yako hapo chini alafu bonyeza 'Reset'. Utapokea link katika email yako kwa ajili ya kutengeneza password mpya.
Tafadhali elezea kwa nini unahisi chapisho hili linapaswa kuripotiwa
Tafiti Nyingi : Mafuta ya mbegu za mimea ni chanzo cha Magonjwa Mengi ya Lishe

September 10, 2018 Dr Boaz Mkumbo kisukari, kitambi 1
Mafuta Yapi Yanafaa Kupikia? Wengi Hujibu “Mafuta ya Mbegu za Mimea (VEGETABLE OILS) Kama Alizeti,Pamba,Mahindi,Soya nk LAKINI yaweza Kuwa KIUNDANI jibu hilo halina Ukweli wowote kwa mujibu wa Tafiti nyingi sasa.
Mafuta ya Kupikia Ubora wake tangu mwaka 1977 yamekuwa yakipimwa kutokana na Uwezo wake wa Kuyeyuka na Kutokuwa na Cholestrol. Kwa hio yasiyo yeyuka kirahisi kama Mafuta ya Wanyama na nazi Yakaonekana ni MABAYA. na Yanayo Yeyuka kirahisi Kama VEGETABLE OIL yakawa mazuri. Kigezo Ni viwili tu (Hayana Mafuta yanayo ganda na Hayana Cholesterol). (1)
Tumekula hivyo Miaka na Miaka kwa Sababu ya NADHARIA ILIYOTUNGWA na Daktari maarufu duniani Ancel Benjamin Keys kuanzia miaka 1950s kwamba “Mafuta yanayoganda huongeza cholesterol na Hicho ni chanzo cha m/gonjwa ya moyo na Presha” Raisi wa marekani akabadilisha sera mwaka 1977 akishirikiana na Seneta wake George McGovern na Prof Mark Hegested kwamba “Vyakula vyote viwe Low fat”
Tukaanza Kula hivyo miaka 35 MALENGO YAO KIAFYA HAYAJATIMIA ILA KIUCHUMI YAMETIMIA. Magonjwa ya Moyo yanazidi Kupanda kwa kasi ya Ajabu ktk Jamii.
Kwa nini Hayakidhi Vigezo vya Kuwa mafuta ya kulinda afya yako?
Sababu ya Kwanza:
Tafiti zinaonesha wazi kwamba mafuta ya mbegu za mimea huwa hayastahimili moto,Ila kwa sababu ya bei poa wengi tunayatumia. Kibaya zaidi ili kubana matumizi Unakuta mtu anakaangia mafuta kwa Kuyarudia. Mfano. Leo ukakaangia nyama na kesho ukatumia kukaangia samaki kwa mafuta yale yale kitendo hicho unatengeneza sumu nyingi sana zenye athari kubwa mwilini.
Unapochoma mafuta hayo hutengeneza Sumu ziitwazo Aldehydes na Hydroxyperoxides ambazo huenda kuathiri sehemu ya kuta za mishipa ya damu na kuzuia mishipa ya damu isitengeneza Nitric Oxide. Ambapo NO husaidia Damu kutembea ktk mishipa kwa mgandamizo (Presha) salama. Sumu hizo Huzuia NO kutengenezwa na matokeo yake Mgandamizo ktk mishipa ya damu Kuongezeka kwa sababu kitendo cha mishipa ya damu Kusinyaaa na Kutanuka huathiriwa.
Nina wagonjwa Wengi tu ambao “Wakipunguza haya mafuta ya mbegu za mimea,Pumu,Presha kali, Kipanda uso,Magonjwa ya kuwashwa ngozi” Huondoka mara moja. Hii ina maana gani? Sumu hizi “Hutaleta vita ndani ya mwili” (2)
Sababu ya Pili
Kwa nini Mafuta ya Mbegu za Mimea (Vegetable oil) yanatuhumiwa kusababisha Kitambi,Kisukari,Magonjwa ya moyo,Pumu nk?
Mafuta haya yamepewa jina hilo haimaanishi yanatokana na Kabeji kisamvu au chainizi. Hapana..! Yanatokana na mbegu za Mimea kama Mahindi,Soya,Alizeti,Pamba nk neno “Vegetable oil” ni Jina maarufu “Kibiashara”. Mafuta haya pia yanatangazwa kwa kuwekewa neno “Cholesterol free” wakati tunajua kwamba Kwenye mimea huwa hakuna cholesterol huwa kuna “phytosterols”.
Ina maana “No Cholesterol ,Vegetable oil, Ni lugha ambazo makampuni yalilazimishwa na sera za Amerika wakati ule Richars Nixon anapisha Mwongozo wa kwanza wa Lishe mwaka 1977,Kwa kusaidiana na Seneta George McGovern na Prof Mark Hegsted (Harvard).
Mkakati wao ilikuwa ni Kuondoa Mafuta ya Wanyama Yote pamoja na Mafuta ya nazi na Mengine yote yakapewa jina hilo “Vegetable oil na Cholesterol free” Ili watu wayakimbilie kuwa yanawakinga na Magonjwa ya moyo.
Nadharia hio kuwa “Cholesterol ni kisabibishi cha magonjwa ya moyo, mwaka 1950s imegonga mwamba tangu ilipo pokelewa ilipingwa,Ikapitishwa kwa nguvu na bado hadi sasa Mvutano ni mkali na Ushahidi Upo wakutosha kwamba “Mafuta haya yanayo pambwa yanawezakuwa ndio sababu ya mlipuko wa magonjwa ya moyo na mengine mengi ya lishe”
Kabla ya Mwongozo huu Unaambiwa uwiano wa Omega 3 na Omega 6 ulikuwa 1:1 au 1:2 miaka 1920s. Haya ni mafuta ambayo hutengeneza viungo karibia vyote mwilini. Lakini Huwa hayatengenezwi na mwili hivyo upatikanaji wake ni Kupitia kula chakula chenye mafuta hayo.
Lakini Tafiti nyingi sasa zinaonesha kwamba miili yetu ukipima Uwiano kwenye damu wa omega 3 na omega 6 umefika 1:16.7-20 ina maana tumezidiwa kiwango cha mafuta haya ya Omega 6. (3)
Kiufupi: Omega 3 huitwa pia Alpha Linolenic Acid (ALA) na Omega 6 huitwa Linolenic Acid (LA). Omega 6(LA) hupatikana kwa wingi kwenye mbegu za Mimea kama Alizeti,Pamba,Soya,Mahindi Isipokuwa NAZI,MAWESE,na KOKOA. Ambapo Omega 3 (ALA) vyanzo ni Kijani kiwiti cha mboga za majani,Chia seeds,Almonds,Walnuts nk
Pia vyakula kama Samaki,Mayai,Nyama huwa vina Omega 3 ambayo ipo katika mfumo wa kutumika moja kwa moja (Haihitaji maboresho) mifumo hio ni EPA na DHA.
Kwa sababu Lishe yetu ya kila siku tunayofuata ni kwa mujibu wa Mwongozo wa Amerika 1977. Ambao sasa unaotumika ni latest 2015-2020.
Unahimiza kutumia “Vegetable oil” tangu mwaka 1977 hadi sasa.
Sehemu ya Kwanza Tuliona jinsi “Mafuta haya hayastahimili moto hasa ktk Kukaangia vyakula hutengeneza Sumu nyingi Hydroperoxides na aldehydes ambazo huhatarisha mwili wako kuwa katika msongo wa Sumu (Oxidative stress). Kwa sababu Kila tunachokula kimepikwa kwa Mafuta ya mbegu za mimea (Omega 6 rich oils) imetupelekea Uwiano wa Omega 6 m/Omega 3 kukwea sana na kuanza kuleta athari mbalimbali kibaolojia mwilini.
Unaambiwa:
Mwili unapo upatia mafuta mengi yenye uwiano mkubwa wa Omega 6 (LA) ambayo ni Vegetable oil, pale yanapotumika mwilini, hubadilishwa kuwa Arachidonic acid (AA) ambacho ni chanzo kikuu cha uzalishaji wa Prostaglandin,Prothrombin na Leukotines.
Nini Athari za Hivi?
Prostaglandin E2 huratibu kuvimba kwa mishipa ya damu, wakati Prothrombin hugandisha damu na kuifanya iwe nzito, na Leucotrine huvutia chembe nyeupe zije kwenye tukio na kuzishikilia ili Donge la mafuta litengenezwe kwenye mishipa ya damu. Kitendo hicho cha Kutengeneza Donge kitalamu ndio huitwa Artherosclerosis! HAYA NDIO MADHARA YA KULA KUPINDIKIA MAFUTA YA OMEGA 6 KULIKO OMEGA 3.
Baada ya kuona Jinsi mwili ukizidiwa na Uwiano mkubwa wa Mafuta ya Omega 6 unavyoweza Kupata Magonjwa ya Moyo, Pumu nk
Ila Pia Kadri kiwango cha Omega 6 kinavyozidi mwilini ndivyo utengenezwaji wa Viashiria vya mwili kuvimba (Mapigano ndani ya mwili) kuongezeka. Viashiria hivyo tumejadili ni Prostaglandin E2, Prothrombin A2 na Leukotrines vyote hivi vinakuhatarisha kupata magonjwa ya mashambulizi ya mwili, Mwili unapoteza mwelekeo pia kiutendaji Unaongezeka Uzito kwa kasi na kazi sana Kupungua, Pumu ya kifua,Pumu ya ngozi (Kuwashwa ngozi na kututumuka), Kipanda uso, Shinikizo la damu, Magonjwa ya moyo nk.
Vihatarishi hivyo vinakuhatarisha wewe damu inakuwa katika msukumo mkubwa (Prothrombin A2 hufanya mishipa ya damu kutokusinyaa vizuri,Damu kuwa nzito na Kuganda). Pia Mashambulizi haya yamehusishwa sana na matatizo ya Kupoteza Kumbukumbu katika Umri mdogo.
Unaambiwa kwamba Mwili huwa hauna uwezo wa kutengeneza Omega 3 wala Omega 6 tunategemea chakula. Na mwili hauna uwezo wa kubadilisha eti Kwa sababu umekula Omega 6 nyingi mwili ubadilishe upate Omega 3 hio hakuna. Kwa maana hio Uwiano na Wingi wa Omega 3 na 6 tunategemea kutoka kwenye Chakula na Ili Uweze Kuuzima Moto unaowaka na Upone magonjwa Tunatakiwa Tujikite kwenye Kuwianisha Omega 3 na Omega 6 kwenye Chakula tunachokula.
Mwili unapo Upatia Omega 3 nyingi na Ukaupunguzia Omega 6 hiki ndicho hufanyika:- Mwili wako unapokuwa unatumia vyanzo vya mafuta ya Omega 3 huwa lengo ni Kupata zao la mwili ambalo hutumika huitwa EPA na DHA (Nimefupisha)
Mfano: Kwenye Vyakula vya mimea kama Chia seeds, Almonds,Korosho, Mbegu za maboga, Walnuts nk tunapata Omega 3 lakini huitwa ALA (Alfa Linolenic acid). Tofautisha na Mbegu kama Alizeti,Pamba,Soya,Mahindi hutupatia mafuta ya omega 6 ambayo huitwa Linolenic Acid (LA). Mwili Unapokuwa Unatumia Mafuta ya omega 3 kutoka kwenye mimea (Alpha Linolenic Acid) Hubadilisha LA na Kupata zao liitwalo EPA na DHA. Wakati Mwili unapokuwa unatumia Omega 6 unatupatia prostaglandin,Prothrombin na leukotrines ambazo zikiwa nyingi hukuhatarisha na magonjwa
Baada ya Mwili Kujipatia EPA na DHA kutoka kwenye Vyanzo vya Vyakula vya Mimea na wanyama. Hivi ndivyo Hukukinga na Magonjwa ya Moyo:- 1. Hupunguza Uzalishaji wa kianzirishi cha kuvimba kwa mishipa ya damu Prostaglandin.
Unaambiwa kiafya Tumezidisha Matumizi ya Mafuta ya Omega 6 ndio maana Jamii inateseka na magonjwa ya mashambulizi ya mwili. Pia mafuta haya tunayatumia vibaya (Rejea somo No 1). Jitahidi Kupunguza Matumizi ya mafuta hayo na Kuongeza Vyanzo vya Omega 3 kama nilivyo vitaja katika somo hili.
Soma Kitabu cha Nuru ya Kisukari, #sayansiyamapishi utajifunza Mengi sana kwa nini watu wanapata mafanikio makubwa sana kiafya pale tu wanapoyatupilia mbali mafuta haya na kufuata ushauri ninao toa.
Kinyume kabisa na Mwongozo wa mwaka 1977 kwamba Cholesterol ndiye adui. Bali Kiwango kingi cha Omega 6, mafuta yasiyostahimili moto ndiye adui Namba moja wa mishipa ya damu. Tusipumbazwe na neno “Cholesterol free”
Mafuta ya Nazi, Mawese, Samli,Siagi,ng’ombe yanaweza Kuwa mbadala na yanaponya. Pia Ongeza matumizi ya karanga zenye Omega 3 nyingi.
REJEA ZA SOMO HILI:
KWA HISANI YA GOOGLE.
asante sana