Maana ya kata ni nini?
Jiunge MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Login MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Umesahau password yako?. Andika email yako hapo chini alafu bonyeza 'Reset'. Utapokea link katika email yako kwa ajili ya kutengeneza password mpya.
Tafadhali elezea kwa nini unahisi chapisho hili linapaswa kuripotiwa
Neno kata lina maana nyingi.
1. (Kitenzi) pitisha kitu chenye makali sehemu fulani mfano kisu au mkasi kwenye kitu ili kukigawanya katika sehemu kadhaa.
2. (Kitenzi) ondoa sehemu ya kitu; tenga sehemu katika kitu. mfano kata mkono; kata tawi; kata mshahara.
3. (Nomino) ngazi ya chini ya utawala wa nchi. Kata ziko chini ya wilaya na kila wilaya huwa na kata kadhaa. Ndani ya kila kata kuna vijiji au kama ni kata ya mjini kuna mitaa ndani yake. Zanzibar kata huitwa “shehia”.
4. (Nomino) majani au kitambaa kilichoviringwa cha kuchukulia mizigo, kinachowekwa kichwani au begani.
5 (Nomino) chombo kinachotengenezwa kwa kutumia zaidi ya nusu ya kifuu cha nazi au kibuyu na kutiwa mpini, hutumika kwa kuchotea na kunywea maji, uji, pombe, n.k..