Kwa nini wanawake wenye mafanikio huogopwa?
Jiunge MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Login MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Umesahau password yako?. Andika email yako hapo chini alafu bonyeza 'Reset'. Utapokea link katika email yako kwa ajili ya kutengeneza password mpya.
Tafadhali elezea kwa nini unahisi chapisho hili linapaswa kuripotiwa
Emmanuel Magessa
Upo ukweli kuwa wanaume wengi wanawaogopa wanawake wenye mafanikio. Hawa ni wanawake wenye kiwango kikubwa cha elimu, fedha, umaarufu au hata madaraka katika jamii. Hoja ya wanaume wenye mawazo haya ni ugumu wa kuwaongoza wanawake wanaowazidi kama alivyonieleza Godfrey, mwalimu wa sekondari jijini Arusha:
“Mwanawake akipata kitu anakuwa jeuri sana. Hawezi kukusikiliza tena na atataka awe huru kufanya mambo yake bila kuingiliwa.” Kwa mujibu wa Godfrey, uwezo wa kifedha na mafanikio kwenye maeneo mengine ya maisha mara nyingi humfanya mwanamke asiwe na utayari wa kuwa chini ya utawala wa mwanaume. “Huwezi kuishi na mwanamke anayejiona yuko juu yako na ukabaki salama. Hatokuwa tayari kukupa nafasi ya kuwa na sauti kwenye nyumba.”
Hitaji kubwa la wanaume wengi ni mamlaka. Wanaume wanapoingia kwenye uhusiano na mwanamke wanakuwa na shauku ya kuwa na sauti inayosikika bayana kukidhi dhana ya kichwa cha familia. Ili sauti hii iweze kusikika bara bara uwezo wa kifedha, kielimu, kimadaraka na hata umaarufu unakuwa na nafasi yake.
Kwa maana hiyo inapotokea mwanamke ameshindwa kuwa chini ya mamlaka yake, mwanaume huanza kujisikia hayuko salama kama anavyoeleza Dickson, karani wa benki mjini Moshi:
“Niliwahi kuwa na dada mmoja mwenye Masters wakati huo mimi nafanya shughuli zangu ndogo ndogo za kiujasiriamali na elimu yangu ya Diploma. Kaka nilikoma kuringa. Mule ndani tulikuwa na bunge lisiloisha. Kila ninachosema, bi mkubwa lazima apinge. Masters ikawa inashindana na Diploma sikuweza kuvumilia.”
Inavyoonekana…. endelea kusoma